Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 12/07/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 24 Dhu al-Hijjah 1444 H sawia na 12 Julai 2023 M

Hukmu ya Qur'an Tukufu kwa Dola Hasimu Zinazokinajisi Kitabu cha Mwenyezi Munguﷻ


Mwenyezi Mungu ﷻ ameamrisha,

[وَإِن نَّكَثُواْ أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُواْ فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُواْ أَئِمَّةَ الْكُفْرِ إِنَّهُمْ لاَ أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ]

“Na wakivunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na wakatukana Dini yenu, basi piganeni na waongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha.” [Surah At-Tawbah: 12]. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu ﷻ ametuamrisha kuwapiga vita viongozi wa makafiri wanaoichafua Dini yetu. Je, mataifa ya kibepari ya Kimagharibi, ikiwemo Sweden, sio viongozi wa makafiri? Ikiwa kuna amri ya kupigana dhidi ya viongozi wa kikafiri, basi ni upi unapaswa kuwa msimamo wa Imam anayeongoza Ummah, kwa wale wanaounga mkono kuvunjiwa heshima Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ, Mola wa Wanadamu wote? Hakuna hata mmoja kati ya madhalimu waliowekwa juu ya ardhi za Waislamu, wanaodai kuwa viongozi wa watoto wa Ummah, mwenye ujasiri wa kuchukua hukmu ya Qur'an juu ya suala hilo. Ni Khalifa pekee, kiongozi wa Khilafah kwa Njia ya Utume, ndiye ambaye atakayewawajibisha viongozi wa ukafiri, na kulazimisha mikono na ndimi zao ovu zitulie tuli.

18 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 06 Julai 2023 M

Uongozi wa Pakistan Unafeli kwa Sababu ya Fikra zake za Kisiasa Zimefungika katika Kambi za na Mirengo ya Kimataifa

Mnamo tarehe 3 Julai 2023, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alizungumza juu ya "kuboresha eneo letu la kimkakati." Hata hivyo, jitihada za kuthibitisha manufaa kwa Marekani ni kazi bure. Vipaumbele vya kimkakati vya Marekani kwa kanda vimebadilika. Marekani inapanua mipaka ya ushirikiano wa kimkakati na India. Inaipatia India silaha kali, ambayo ni tishio kubwa kwa usalama wa Pakistan. Umma wa Kiislamu una mradi pekee wa kimkakati wa kukabiliana na muungano wa Marekani na India. Ni Khilafah ndiyo utakayounganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati, na kwingineko. Itaanzisha mfumo mpya wa dunia ambao unahakikisha utawala wa Uislamu.

19 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 07 Julai 2023 M

Taarifa ya Pamoja kutoka Marekani na India ni Shambulizi la Moja kwa Moja kwa Usalama wa Pakistan

Mnamo tarehe 4 Julai 2023, Waziri Mkuu wa Pakistan alisema, "Suluhisho la matatizo yetu ya pamoja linatokana na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani ya kanda." Walakini, agizo la kikanda ambalo Marekani inaanzisha linahujumu usalama wa Pakistan. Taarifa ya Pamoja kutoka Marekani na India inahakikisha upeanaji silaha za kisasa kwa India. Teknolojia ya kijeshi iliyotolewa kwa India sio tu itatumika dhidi ya China pekee, lakini pia italenga Pakistan. Hapo awali, betri za mfumo wa ulinzi wa kombora wa S-400, zilizotumwa na Urusi, ziliwekwa kwenye mipaka na Pakistan. Vile vile itakuwa kweli kwa teknolojia ya kijeshi ya droni, ambayo ingelenga "magaidi" ndani ya Pakistan. Uongozi wa sasa wa kisiasa na kijeshi "utalaani" tu ukiukaji wowote wa ubwana wa eneo pekee. Njia pekee ya kukabiliana na utaratibu mpya wa kikanda wa Marekani ni kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

20 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 08 Julai 2023 M

Masharti ya FATF Yalikuwa ni Matwaka ya Dola ya Kibaniani, Yaliyokubaliwa na Watawala wa Pakistan

Ni wazi kutokana na Taarifa ya Pamoja kutoka Marekani na India kwamba hatua za kuchukuliwa dhidi ya Pakistan na FATF zilikuwa matakwa ya Dola ya Kibaniani. Dola ya Kibaniani ilihitaji sana kuvunjwa kwa muundo wa Jihad huko Kashmir. Matokeo yake, Jeshi la India liliikamata Kashmir kwa nguvu mnamo 2019, bila upinzani. Uongozi wa kijeshi ulichukua jukumu la moja kwa moja la kutekeleza matakwa ya FATF ili kuhakikisha kujisalimisha kwa Kashmir. Uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Pakistan ndio wawezeshaji wa Modi. Ushirikia kati ya Marekani na India ni dhidi ya China, kama ilivyo dhidi ya Waislamu wa eneo hili. Hatuna chaguo ila utumwa katika mfumo wa sasa wa kimataifa. Chaguo hili halikubaliki kwa wanajeshi na watu wa Pakistan! Ni wakati sasa wa kuanzisha mfumo mpya wa kimataifa, chini ya Khilafah kwa Njia ya Utume.

21 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 09 Julai 2023 M

Ni Wakati sasa wa Uamuzi. Kujisalimisha kwa Dola ya Kibaniani au Utawala wa Uislamu kupitia Khilafah

Mnamo tarehe 4 Julai 2023, Waziri Mkuu aliilaani India kwa "kujishindia alama za kidiplomasia." Walakini, yanayofanyika ni zaidi ya kujishindia tu alama. Mbali na ushirikiano katika silsila za usambazaji viwandani, na ushirikiano wa majini na usalama kuhusu Indo-Pasifiki, Burma, Pakistan, Taliban na Ukraine, Marekani itaisaidia India kuunda droni na injini za ndege, miongoni mwa teknolojia nyingine za juu za kijeshi. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Lazima mukatae kuwa dola kibaraka wa India. Ikabilini India, itangazeni sera ya kijeshi kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na zuieni uwasilishaji wa mafuta na gesi kutoka Ardhi ya Waislamu hadi India! Mnajua kwamba uongozi muoga na unaoiunga mkono Marekani hauwezi hata kufikiria kufanya hivyo. Kwa hiyo, wang’oeni watawala hawa. Toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

22 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 10 Julai 2023 M

Khilafah ndiyo Itakayoikomboa Kashmir Inayokaliwa kwa Mabavu, Sio Umoja wa Mataifa

Mnamo tarehe 6 Julai 2023, Afisi ya Mambo ya Nje ilisema, "Jammu na Kashmir ni eneo linalotambulika kimataifa, ambalo mwelekeo wake wa mwisho utafanywa kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa." Kuipa mamlaka taasisi yoyote ya kikoloni juu ya mambo ya Waislamu, maana yake ni kukwepa utiifu kwa Mwenyezi Mungu ﷻ. Kwanza, watawala wa Pakistan walisalimisha ardhi, kisha maji na hatimaye Waislamu wa Jimbo la Jammu na Kashmir mnamo Agosti, 2019. Taasisi za kikoloni zinalinda tu maslahi ya dola kubwa. Mpangilio wa demokrasia ya kiliberali ya kisekula ndio sababu ya ukiukwaji wa utu wa binadamu katika Dola ya Kibaniani. Utawala wa Kiislamu ulihakikisha amani na ustawi kwa kanda hii kwa karne nyingi. Khilafah katika Njia ya Utume itaikomboa Kashmir Inayokaliwa kwa mabavu kupitia Jihad kutoka kwa vikosi vyake vya kijeshi na kuregesha amani na ustawi wa kikanda.

23 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 11 Julai 2023 M

Khilafah Itakata Mahusiano Yote na Mataifa Hasimu, Kama Urusi

Mnamo tarehe 7 Julai 2023, lango jipya la biashara liliwekwa huku lori la kwanza kabisa la Urusi likivuka kuingia Pakistan. Watawala wa Pakistan wanaikaribia Urusi, licha ya uadui wake kwa Waislamu. Watawala wa Pakistan walipuuza mabomu ya pipa na yenye kemikali ya napalm ambayo Urusi iliyarusha juu ya vichwa vya waumini huko Ash-Sham. Hawazingatii malipo fidia yanayosubiriwa ambayo Urusi bado haijaulipa Umma wa Kiislamu, kwa uharibifu wa nchi nzima, Chechnya, ardhi ya waumini. Walifumbia macho uungwaji mkono wa Urusi kwa makruseda Waserbia wenye chuki, ambao waliwachinja Waislamu na kuwabaka wanawake wasafi wa Kiislamu. Hawazingatii jinai zinazofanywa na Urusi dhidi ya Waislamu ndani ya Urusi yenyewe na katika dola jirani za Asia ya Kati. Pia wanapuuza kile Urusi inachofanya kupitia mamluki wake wahalifu katika nchi nyingi za Kiislamu za Kiafrika na Asia.

24 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 12 Julai 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu