Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Dua na Unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Ajili ya Naveed Butt Mwenyezi Mungu Afariji Kutekwa Nyara Kwake

Mnamo Mei 11, 2022 M, itakuwa imepita miaka kumi tangu mbebaji mradi wa Khilafah, Mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, kutekwa nyara na magenge ya utawala wa Pakistan mnamo Mei 11, 2012 M na kufungwa kwake katika korokoro za vyombo vya siri vya ukandamizaji. Utawala huu wa kihalifu bado ungali unamnyima Naveed Butt mawasiliano ya aina yoyote na familia yake. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ﴿

Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.” [As-Sajdah: 22]. Hakika sisi tunachukua fursa ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhan wa mwaka huu 1443 H - 2022 M kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) na kumnyenyekea (swt) amfariji Ndugu Naveed Butt na amrudishe kwa familia yake, vipenzi vyake na hizb yake akiwa salama na mwenye mafanikio.

  Ijumaa, 14 Ramadhan 1443 H - 15 Aprili 2022 M

#FreeNaveedButt

- Dua kwa Ajili ya Naveed Butt -

Ewe Mwenyezi Mungu, Ewe Mwenye kufaraji hamu, mwenye kuondoa huzuni na muondoshaji wa dhiki, mwenye kuitikia dua ya masikini, mwenye rehema na mwenye kurehemu duniani na Akhera. Ee Mwenye zi Mungu, muachilie huru ndugu yetu, Naveed Butt, iimarishe nguvu yake, ondoa huzuni yake, ifariji hamu yake, ifariji dhiki yake, na uchukue haki yake, umlipe fidia bora zaidi, umuunganishe tena, na usitunyime kumuona.

Ee Mwenyezi Mungu, mtiishie viumbe vyako vyote kama ulivyoitiisha bahari kwa Musa (as), Ee Mwenyezi Mungu muokoe kutokana na taabu hii, kama ulivyomuokoa Sayyidna Yusuf (as) kutokana na vitimbi vya wenye vitimbi.

Ee Mwenyezi Mungu mlainishie nyoyo za viumbe kama ulivyomlainishia Daudi (as) chuma, Ee Mwenyezi Mungu, kuwa pamoja naye na umjaaliye kutoka kwako nguvu na ukwasi zaidi.

Ee Mwenyezi Mungu, hakika tunakuomba, ewe mwingi wa rehema, ewe ambaye hakuna gumu kwake dogo wala kubwa, mfanyie wepesi kifungo chake na umtoe kwetu salama, mwenye mafanikio, mwenye nguvu na mpendwa katika mwezi huu mtukufu, ee Mwenyezi Mungu imlipie kisasi wale waliomdhulumu, na usimamishe dola ya Kiislamu Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo amejitolea muhanga kwa ajili ya kuisimamisha, Naveed na wengi wa ndugu zake katika Hizb ut Tahrir kote duniani.

Allahuma Amin... Allahumma Amin... Allahumma Amin

Video kwa Anwani:

“Naveed Butt Alitekwa Nyara na Magenge ya Utawala wa Pakistan Mwaka 2012 M Machoni mwa Familia Yake”

- Alama Ishara ya Kampeni -

#FreeNaveedButt

Ili Kuzuru Ukurasa wa Angazo Maalum la Utekaji Nyara wa

Mhandisi Naveed Butt – Mwenyezi Mungu Amtoe katika Mateka

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan

Bonyeza Hapa

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu