Jumamosi, 17 Jumada al-awwal 1444 | 2022/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Hizb ut Tahrir / Malaysia: Sehemu ya Amali za Kampeni

Funga Viwanda vya Pombe, Kukabidhi Barua kwa Mamlaka za Miji

Baada ya majuma mawili ya kuendesha kampeni "Funga Viwanda vya Pombe", , Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) leo ilikabidhi waraka wa wazi kwa Mamlaka nyingi za Miji kote nchini, ikizisihi kwamba leseni zote za viwanda vya pombe na maduka, zifutiliwe mbali na kusitolewe leseni mpya kwao.

Kampeni hii ilifanywa kufuatia ongezeko la visa vya uendeshaji magari kwa ulevi, ambapo baadhi yake vilimalizikia kwa ajali mbaya zikihusisha waathiriwa wasio na hatia. Ilipokea majibu mazuri kutoka kwa Ummah, na hata iliungwa mkono na baadhi ya wasiokuwa Waislamu.

Katika waraka huu, Hizb ut Tahrir ilizikumbusha Mamlaka za Miji uharamu wa pombe katika Uislamu na makundi kumi yaliyo laaniwa na Mtume (saw) kuhusiano nayo, ambapo yamaanisha waziwazi kuwa uzalishaji na uuzaji wa pombe ni haramu kabisa. Mamlaka za Miji bila shaka hazikusazwa na dhambi hili kubwa, kwa "kuchangia" kwao katika visa vya uendeshaji magari kwa ulevi, kwa utoaji leseni kwa viwanda na maduka ya pombe.

Mamlaka za Miji nyingi zilipokea waraka huu na baadhi ya maafisa hata kuukaribisha na kufanya mazungumzo zaidi na ujumbe wa HTM juu ya kadhia ya uendeshaji magari kwa ulevi, viwanda vya pombe, na suluhisho lake. Lakini, HTM ilisisitiza kwamba ukaribishaji mzuri na mazungumzo pekee kamwe hayatatatua tatizo hili. Ni kwa kupitia uchukuaji hatua wa Mamlaka za Miji katika kufunga viwanda vyote vya pombe na kuharamisha uuzaji wa uchafu (Rijs) huo waziwazi ndio utakao tatua tatizo hili pekee.

Tangu kuanza kwa kampeni hii, HTM waziwazi inaeleza kuwa ajali mbaya zinazo sababishwa na madereva walevi zinatokana na utoaji leseni wa serikali kwa viwanda vya pombe, uagizaji pombe kutoka ng'ambo, na uuzaji waziwazi wa uchafu (Rijs) huu. Hivyo basi, suluhisho pekee la tatizo hili ni kuziondoa leseni zote na kukomesha utoaji wa leseni mpya.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Malaysia

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 25 Juni 2020 18:26

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu