Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  12 Shawwal 1445 Na: HTY- 1445 / 30
M.  Jumapili, 21 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Imarati (UAE) Yaunda Kikosi cha Mamluki, ambacho Baadhi yake Kitafanya kazi nchini Yemen na Sudan!
(Imetafsiriwa)

Uchunguzi uliochapishwa na gazeti la Ujerumani Deutsche Welle mnamo tarehe 14/04/2024 uliisifia UAE kama kituo cha mamluki barani Afrika na Mashariki ya Kati, haswa Yemen na Sudan. Gazeti la Ufaransa, Online Intelligence lilifichua tangazo hilo, ambalo lilisambazwa kwa wanajeshi wa zamani katika Kikosi Maalum cha Ufaransa. Gazeti hilo lilieleza kuwa uchunguzi ulionyesha kuwa tangazo hilo ni la Kampuni ya Ushauri wa Kijeshi ya Manar, ambayo inaendeshwa na afisa wa zamani wa Kikosi Maalumu cha Ufaransa chenye uhusiano na Abu Dhabi. Jarida la Ufaransa lilisema kwamba mtu anaweza kuhitimisha kutokana na tangazo hilo kwamba UAE inataka kuunda vikosi vyake vya bora vya kigeni, labda vinavyojumuisha idadi ya wanajeshi kati ya 3,000 na 4,000, kufikia katikati ya 2025. Jaribio la kwanza la Abu Dhabi lilikuwa mwaka 2009 kuunda brigedi ndani ya Imarati yenye wanachama 800 na Erik Prince, mwanzilishi wa Blackwater.

Imarati, mtoto wa Waingereza, ambayo idadi ya jeshi lake ni 65,000, ilianza kutumia mamluki wa kigeni mwaka 2016 ilipokodi mamluki kutoka kampuni ya American Spear Group kuwaua watu 160 ambao hawakutii amri yake, wakiwemo maimamu, wahubiri wa misikiti, wanasiasa, wanajeshi, na wanasheria wa Aden, baada ya UAE kuingia nchini humo kuwafukuza Mahouthi mnamo Agosti 2015. Ushirikiano uliendelea kati ya maafisa wa Marekani na maafisa wa Imarati, kama shirika la Reuters lilivyofichua mwaka wa 2019 kwamba UAE ilikuwa inataka kuanzisha vitengo vya vita vya kielektroniki. Gazeti la Washington Post pia liliripoti mwaka 2022 kwamba UAE inaendelea kulipa mishahara kwa maafisa wa zamani wa kijeshi wa Marekani badala ya kutoa huduma na ushauri. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, Sipri, mwaka 2023, hali ya makampuni ya ulinzi ya kijeshi ya kibinafsi imeongezeka tangu 2003, tangu kuanzishwa kwa Blackwater na dori yake chafu katika uvamizi wa Iraq.

Leo, Abu Dhabi inaonekana katika hali mbaya zaidi, inapoanzisha kikosi cha mamluki kuhudumia miradi ya kikoloni ya Uingereza nchini Yemen na Sudan. Ama kwa Yemen, kutekeleza mauaji zaidi yaliyoanza mwaka 2016 ili kuunga mkono mipango ya Uingereza, kukabiliana na kuzuia mipango ya Marekani. Na nchini Sudan kusaidia nguvu za uhuru na mabadiliko ambazo zilizibwa pumzi na mizozo ya jeshi la Marekani; Al-Burhan na Hamidati; vilevile Somalia, Libya na kwingineko.

UAE inafanya hivi ili kumtumikia bwana wake, Uingereza, na kuwa sambamba na mipango ya Marekani katika Mashariki ya Kati. Inadaiwa na Waingereza uaminifu kamili na utiifu, kama mataifa yote mengine ya Ghuba, isipokuwa Saudi Arabia, ambayo inafuata utawala wa Marekani wakati wa enzi ya Salman na mwanawe ... Kwa hivyo, kugongana dhahiri katika sera yake ni matokeo ya mistari mipana iliyochorwa na Uingereza kwa ajili yake kwa kuungwa mkono na watu masekula na wanamgambo wa Kiislamu wanaopinga. Aidha, UAE inatekeleza sera maalum na za kina za Uingereza, na hiyo, UAE, mara nyingi huifanyia kazi Uingereza kwa safu ya nyuma ya vibaraka wa Marekani katika kanda hii, na hutoa huduma zake kwa Uingereza kutoka maeneo hayo.

Hivi ndivyo serikali tawala katika nchi za Kiislamu zinavyonyauka na kuoza baada ya kujiondoa katika utawala wa Uislamu na kuubeba kwa wasiokuwa Waislamu, na kujihusisha na mipango ya maadui wa Uislamu na Waislamu, kama vile Imarati ambayo imekuwa kimbilio la wasiokuwa Waislamu ambao idadi yao inazidi idadi ya watu wao, na wanajenga makanisa, masinagogi na mahekalu ya Kibaniani ya ushirikina kwa ajili yao, na kuanzisha majeshi ya kutumikia ukafiri na watu wake, na dhidi ya Uislamu na watu wake katika Bara Arabu! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[الأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْراً وَنِفَاقاً وَأَجْدَرُ أَلاَّ يَعْلَمُواْ حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللهُ عَلَى رَسُولِهِ وَاللهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ * وَمِنْ الأَعْرَابِ مَنْ يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَماً وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ وَاللهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ]

“Na katika Mabedui hao wapo wanao fikiri kuwa wanayo yatoa ni gharama ya bure, na wanakungojeleeni mambo yakugeukieni. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” [At-Tawbah 9:98]. Kazi na matarajio ya Waislamu itanasilia katika kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi na kuilingania kwa Waislamu ili kuitikia ulinganizi huu mtukufu wa kufikia haki na kuifagia mipango miovu dhidi ya Uislamu na Waislamu. 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu