Alhamisi, 07 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  26 Ramadan 1445 Na: HTY- 1445 / 28
M.  Ijumaa, 05 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Mnaweza Kubadilisha hadi Mfumo wa Dhahabu na Fedha Badala ya Kujidanganya kwa Kubaki kwenye Mfumo wa Fedha wa Kulazimishwa?
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 20 Ramadhan 1445 H, sawia na 30/3/2024 M, Gavana wa Benki Kuu jijini Sana'a, Hashim Ismail, alifanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo alitangaza kutolewa kwa sarafu mpya ya riyal 100 kuchukua nafasi ya noti ya riyal 100 iliyoharibika iliyotolewa naye. Matumizi ya sarafu mpya yalianza kutumika mnamo Jumapili, Ramadhan 21, 1445 H. Vituo vitafunguliwa kwa ajili ya ubadilishanaji kile kilicho mikononi mwa watu kwa sarafu hiyo mpya. Kwa mujibu wa kukiri kwa gavana wa benki hiyo, sarafu hiyo mpya ilitolewa kulingana na viwango vya juu zaidi vya kimataifa, yaani si kwa mujibu wa Shariah, na ni tofauti kubwa iliyoje kati ya hizo mbili!

Kwa hivyo, Mahouthi wanaendelea kutabikisha mfumo wa fedha uliokumbwa na matatizo mengi, ambayo ni mfumo wa fedha wa kibepari - ambao wanadai kuwa wameubadilisha - wanaendelea kutumia fedha za karatasi za lazima ambazo hazina uhusiano na dhahabu au fedha, na pia sio badali yazo. Ni pesa zenye thamani ya jina iliyoamuliwa na benki inayozitoa, na hivyo kutoa sheria inayohitaji watu kuamiliana nazo. Haina thamani ya dhati zaidi ya tu nguvu ya sheria. Pesa za karatasi za kulazimishwa zisizo na thamani ya dhati (fiat) hupoteza pesa za watu, na kupunguza mara kwa mara thamani yake ya ununuzi. Ikiwa watu wawili, mmoja wao ataweka dinari 10 za dhahabu, na mwengine aweke sawa na pesa ya kulazimishwa ya karatasi, na kurudi baada ya miaka ishirini, watapata nini? Dinari zitahifadhi thamani yake, na pesa ya karatasi za fiat zitapoteza thamani yake.

Kwa nini Mahouthi wasihamie kwenye mfumo wa pesa wa fedha za dhahabu, na kutoa karatasi zinazoziwakilisha, ambazo watu wanazisambaza na wanaweza kubadilishana kwenye benki kwa dhahabu na fedha wakati wowote wanapotaka?

Pesa inafafanuliwa kama kitu ambacho watu wamekubali kutumia kama bei ya bidhaa na mishahara kwa juhudi na huduma, na ambayo bidhaa, juhudi na huduma zote hupimwa. Ni njia ya kubadilishana, na Uislamu umeifafanua kuwa ni pesa za dhahabu na fedha. Iliweka kiwango (nisab) ya zakat juu ya dhahabu na fedha, ikaharamisha kuhodhi hazina yao, na ikaunganisha sheria za pesa za damu (diya) kwazo, na kukatwa mkono wa mwizi. Dinari ya dhahabu ni sawa na gramu 4.25, na dirham ya fedha ni sawa na gramu 2.975. Hati za dhamana, hisa, au mfano wake hazizingatiwi kuwa ni pesa. Kuna aina mbili za pesa:

Pesa za chuma na karatasi, pesa za karatasi ni zile zinazochukuliwa kutoka kwa karatasi badala ya dhahabu au fedha, au kufinikwa kwa dhahabu au fedha, au kwa zote mbili, zilizofinikwa kikamilifu au sehemu yake, au sio badali kwazo wala kufinikwa nazo.

Mfumo wa fedha unapata jina lake kutokana na asili ya sarafu ya msingi inayotumiwa ndani yake. Ikiwa sarafu ya msingi ni dhahabu, inaitwa mfumo wa dhahabu au msingi wa dhahabu, na ikiwa thamani ya kipimo cha msingi cha fedha haina uhusiano uliowekwa na dhahabu au fedha, mfumo huu unaitwa mfumo wa fedha wa kulazimishwa, na hiki ndicho kinachoendelea leo katika dola hizi.

Kurudi kwa muamala wa pesa kwa msingi wa dhahabu na fedha kutasaidia kuizuia kutokana na mishtuko ambayo sarafu zenye nguvu zaidi zinakabiliwa nayo siku hizi, na kurudi kwa pesa za dhahabu na fedha hakuepukiki, ili utulivu uweze kuregeshwa kwa wananchi baada ya fedha zao kupotea. Mojawapo ya matokeo mabaya zaidi ya mabadiliko ya thamani ya sarafu ni mfumko wa bei wa fedha unaosababisha kushuka kwa thamani ya fedha na udhaifu wa uwezo wake wa kununua, ambao unasababisha kupanda kwa bei, mdororo wa biashara na kudorora kwa ukuaji kwa ujumla, na juu ya hayo, ukiukaji wa hukmu ya Shariah. Matatizo haya kwa hakika ni janga la kiuchumi linalozikumba nchi, kuchosha uchumi wao, kuharibu mali zao, na kuweka rehani utashi wao kwa wengine hasa ikiwa nchi ni ndogo na dhaifu, ili kurudi kwenye kiwango cha dhahabu, sababu zilizosababisha kuachwa na sababu zilizosababisha kuzorota kwake lazima ziondolewe. Hizb ut Tahrir imetabanni muelekeo wa kivitendo wa kushughulikia matatizo haya, ambayo Dola inayokuja ya Khilafah itatekeleza hivi karibuni, Mwenyezi Mungu Akipenda, na imeeleza vipengele vya kifedha katika kitabu “Mali katika Dola ya Khilafah”.

Mfumo wa uchumi wa kibepari - ambao unatabanni mfumo wa lazima wa pesa za karatasi - ni janga kwa ulimwengu mzima, umekandamiza watu katika kila kitu kinachotokana nao. Migogoro ya mara kwa mara inayoikumba dunia imeibuka, ambayo hivi karibuni zaidi ni mgogoro wa 2008. Ni wakati sasa wa Waislamu kurudi kwenye mfumo wao wa kiuchumi, pamoja na mifumo mingine ya maisha: kisiasa, kijamii na mengine chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mtume (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu