Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  14 Sha'aban 1445 Na: HTY- 1445 / 23
M.  Jumamosi, 24 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uamuzi wa Houthi wa Kuziainisha Marekani na Uingereza kama Maadui wa Yemen
(Imetafsiriwa)

Mehdi Al-Mashat, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa, alitoa uamuzi mnamo Jumatatu, 19/02/2024, kuziainisha Marekani na Uingereza kuwa nchi mbili zenye uadui dhidi ya Yemen. Uamuzi huo ulikuja baada ya kupitishwa kwa sheria katika Bunge la Wawakilishi jijini Sana'a, na muda mfupi baada ya kuainishwaji wa Mahouthi kama "kundi maalum lililoundwa la kigaidi la kimataifa."

Marekani na Uingereza zinapigana vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa amri ya Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu saba. Je, Mahouthi wametambua hilo baada ya Marekani kuwaainisha kama kundi maalumu la kigaidi la kimataifa?! Au hatua hii imekuwa ndio majibu?! Kinachoumiza sana moyo ni hamu ya Mahouthi ya kukwepa kumwaga damu yao katika Bahari Nyekundu, kwani kwa mujibu wa chaneli ya Al-Masirah, yenye uhusiano na Mahouthi, "wafanyikazi wa meli ya Uingereza ya Ruby Mar walifanikiwa kuondoka salama kwenye meli" (Taarifa ya saa 9:00 usiku, 19/02/2024), pamoja na msemaji wao rasmi, Mohammed Abdul Salam, akiiambia Reuters: "Operesheni zetu katika Bahari ya Shamu na Ghuba la Arabuni hazijasababisha kumwaga hata tone moja la damu" (Al-Thawra, 20/01/2024), wakati wamekuwa wakianzisha mashambulizi makali dhidi ya Yemen tangu 12/01/2024, na kusababisha umwagaji damu. Iko wapi kanuni ya kuheshimiana unayoizungumzia?! Wote wawili wanaliunga mkono umbile la Kiyahudi mchana na usiku, huku Waislamu wakishiriki katika vita vya mifarakano kati yao kwa wao kwa miaka mingi. Je, Waislamu wanatambua kosa lao hili kubwa la kutopigana na maadui wa Uislamu na Waislamu wanaowavizia Waislamu?! Ni kosa kubwa kwenu kudai kwamba kulenga kwenu meli za Marekani na Uingereza kunalenga tu kuondoa mzingiro wa Gaza!

Uadui wa Uingereza dhidi ya Uislamu na Waislamu umedhihirika tangu kushiriki kwake pamoja na Wazungu katika Vita vya Msalaba dhidi ya Bayt Almaqdis uvamizi wake wa ardhi za Waislamu, fitina zake, vita na uvunjaji wa Khilafah. Marekani, vivyo hivyo, kizazi cha Ulaya, na warithi wa Isabella na Fernando, "wafalme wa Castile na Aragon huko Andalusia," ambao waliwafuata Waislamu kote ulimwenguni tangu 1492, wakipigana na Waislamu katika Bahari ya Mediterania mnamo 1795, wakiungana na Wazungu dhidi ya Waislamu. Vita vya Kwanza vya Dunia, na kuondoka kwao kwa ukoloni baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kukoloni ardhi za Waislamu, na kufichuliwa na uongozi wao mwaka 2001 katika Vita vya Msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu chini ya jina la "ugaidi" hadi sasa. Wote wawili wanamiliki ardhi za Kiislamu kwa kupanua ushawishi wao wa kisiasa ndani yake, na wanashindana kupitia vibaraka wao ili kupanua eneo la kila mmoja.

Wajibu sio kushughulika na Marekani na Uingereza kwa vile wao ni makafiri wapiganaji wa kivitendo, na kuacha kukutana na wawakilishi wao huko Geneva, Stockholm, Kuwait, Sana'a, na Muscat, na kutokwenda kwao, badala ya kuamiliana nao kwa mujibu wa sheria za kimataifa na mahusiano ya kimataifa, kama ilivyo leo! Uadui dhidi yao unapaswa kuhusisha kukata mafungamano yote nao nchini Yemen: kisiasa, kiuchumi, kijeshi, na mengineyo. Je, fursa hiyo haikuwa nzuri miaka kumi iliyopita, na je haijarudi hivi sasa?!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surat Al-Ma’ida:51]

Mwenyezi Mungu amewaorodhesha watu katika kundi la Waislamu wanaomwamini Muhammad (saw) na Ujumbe Wake wa Mwisho, na makafiri wasiomuamini. Kisha, Akawagawanya makafiri katika wapiganaji kivitendo wanaoupinga Uislamu na kupigana na Waislamu, na wasio wapiganaji wa kivitendo ambao, kama watawala, hawaonyeshi uadui dhidi ya Uislamu na hawawapigi vita watu wake.

Tunapozungumzia Hizb ut Tahrir, ni Hizb inayotabanni mtazamo mpana wa kuamiliana na ulimwengu kwa jumla, ikianza na kuchunga mambo ya Waislamu na kuishia na kutangamana na wasiokuwa Waislamu. Kusimamishwa kwa Khilafah, inayolinganiwa na Hizb, kunawakilisha mfumo sahihi na mfumo wa utawala katika Uislamu, ambao unazitekeleza hukmu zake zote kwa ukamilifu na kuwaunganisha Waislamu. Haya ni mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu.

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Surat Aal-i-Imran:103].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu