Jumatatu, 23 Sha'aban 1445 | 2024/03/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  13 Safar 1445 Na: HTY- 1445 / 03
M.  Jumanne, 29 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katikati ya Mvutano wa Nchi za Kikoloni juu ya Ushawishi nchini Yemen ni Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume Pekee ndiyo Itakayomaliza Mateso ya Watu wa Yemen
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumatano, maandamano maarufu yalianza kwa siku ya pili mfululizo katika Jimbo la Aden. Waandamanaji walifunga barabara katika vitongoji vya Mansoura na Sheikh Othman. Maandamano hayo yalijumuisha majimbo jirani ya Lahj na Abyan, juu ya hali mbaya ya maisha na kuongezeka kwa bei za juu, pamoja na kukosekana kwa huduma msingi kama vile umeme, maji, na huduma za afya, ambazo zimeyasibu Majimbo hayo kusini mwa Yemen kwa miaka mingi.

Ni ushahidi wa kufeli kwa wanasiasa wa sasa walio madarakani huko Aden na Majimbo ya kusini; Kutoka kwa serikali ya Maen Abdul Malik, wanamabadiliko, na harakati za mapinduzi - ambao huahidi watu mazuri lakini sio chochote bali ni watetezi wa uovu – kuchunga mambo ya watu na kukidhi mahitaji yao ya msingi ya maisha ya staha, kama usalama, nyumba, chakula, mavazi, elimu, na madawa, na kutoa umeme na maji. Pindi uchungaji sahihi wa mambo ya watu ulipokosekana chini ya mfumo wa Kiislamu, na kuingia uchungaji wa nchi za kibepari za wakoloni wa Magharibi zinazoshindana juu ya Yemen, juu ya uporaji wa rasilimali zake, ilisababisha mateso kwa watu, na vyama vya siasa nchini vilichukua kama njia kufanya biashara ndani yake kufikia malengo yao.

Watu wanashangazwa na ukosefu wa umeme katika nchi inayozalisha mafuta na gesi, ambayo uzalishaji wake ni karibu na mapipa milioni moja kwa siku ya mafuta ghafi meusi. Yaligunduliwa na kuzalishwa na kampuni za mafuta ya kigeni kusafirisha kwenda nchi zao. Hawakuruhusu usafishaji wa bidhaa zake kukidhi mahitaji ya nchi, badala yake walishibisha mahitaji yao kwa bidhaa za mafuta kutoka kwao, hii ndio sera ya kikoloni. Hii inafuatwa waziwazi na kampuni hizi kusini mwa Yemen, kwa idhini ya watawala wake.

Vivyo hivyo, huduma zengine hazipo kwa watu kwenye mfumo wa kibepari, hawapewi kwao kama huduma, lakini badala yake hutolewa kwao kama bidhaa. Yeyote anayeweza kuimudu ataipata, na mtu yeyote ambaye haweza, haihitajiwi na yeye. Nchi yao ina utajiri wa maji na kilimo, na bahari zao zina zaidi ya kilomita elfu za ufuo. Jua linaangaza mwaka mzima na upepo uko wa kutosha.

Baraza la Rais na Baraza la Mpito yanafurahiya maisha ya anasa. Hawana njaa au kiu kama walivyo watu, hawasibiwi na kiu inayowasibu watu kutokana na ukosefu wa maji baridi, au joto na giza la kupotea kwa umeme. Watu hawa wako wapi na maneno ya Amiri wa Waumini na Khalifa Muongofu wa Waislamu, Umar bin al-Khattab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, katika mwaka wa al-Ramada: “Nitakuwa mtawala kiasi gani mimi ikiwa nitashiba na watu wana njaa”?! Aliishi kwa kula mafuta, na alijipigia marufuku kula Siagi, hivyo akaligonga tumbo lake kwa vidole vyake viwili na akasema: “Nguruma unavyotaka, naapa kwa Mwenyezi Mungu, sitakula siagi hadi watu waile.”

Maumivu haya yote na huzuni zinazozunguka watu kutoka pande zote yanapaswa kuwa sababu ya kufikiria kuhusu mabadiliko msingi ambayo wenyeji wa mbinguni na wenyeji wa ardhini wameridhika nayo, mabadiliko ambayo yanawaondoa watawala madhalifu. Katikati ya uhalisia huu mchungu, tunatoa wito kwa watu wa Yemen kufanya kazi na sisi ili kusimamisha utawala wa Uislamu chini ya kivuli cha Dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kwa utambuzi na ufahamu, kwa maana tuna mradi wa mwamko kwa msingi wa Uislamu. Je! Mfumo wa Bwana wa Walimwengu una hekima, uzuri na uadilifu ulioje. Hebu watu wetu nchini Yemen na wabadilishe mfumo wa kibepari kwa mfumo wa Uislamu, ili waweze kuishi maisha mazuri, ambayo kwayo mtawala hachukui fursa ya kuishi kianasa yeye binafsi na kuwazuia wengine. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ]

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbiya: 106].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu