Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  12 Sha'aban 1444 Na: HTY- 1444 / 16
M.  Jumamosi, 04 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Msaada wa Kifedha ndio Sababu ya Kuongeza Njaa na Utegemezi kwa nchi za Magharibi
(Imetafsiriwa)

Kongamano la nchi wafadhili kwa Yemen, lilioandaliwa na Sweden na Uswisi kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, lilimalizika jijini Geneva mnamo Jumatatu, Februari 26, na ahadi ya nchi 31 na mashirika ya kimataifa ya kutoa msaada wenye thamani ya dolari bilioni 1.2, kutumika kuepusha tishio la njaa na kuwasilisha misaada kwa mamilioni ya Wayemeni waliokimbia makaazi yao kutokana na vita na wamechoshwa na njaa na maradhi bila ya kuwepo matumaini yoyote ya kumalizika kwa vita ambavyo vimekuwa vikiharibu nchi hiyo tangu mwaka 2014. Lakini kiasi kilichoahidiwa katika kongamano hilo kilipungua azma ya Umoja wa Mataifa, ambayo inataka kukusanya dolari bilioni 4.3. Hata hivyo, shirika hilo la kimataifa linatumai kuwa kiasi hicho kitapanda hadi dolari bilioni 2 kabla ya mwisho wa wiki hii.

Vita nchini Yemen vinavyoongozwa na Marekani na Uingereza vimesababisha kila aina ya magonjwa na mikurupuko. Kutokana na utapiamlo na njaa, watoto 400,000 wanakabiliwa na madhara yake kati ya watu milioni 21 ambao hawapati chakula cha kutosha, vinywaji na huduma za matibabu. Kisha Umoja wa Mataifa, unaotengeneza ugonjwa huo na kutengeneza dawa, unakuja kucheza mziki wa upande wa misaada ya kibinadamu ili kufikia kile ambacho wafadhili na waundaji wa shirika hili wanataka, kwa maslahi ya Magharibi Kafiri iliyoianzisha na kufikia maslahi yake kupitia hata kama makongamano haya na mengine kama haya hayana muunganiko na upande ya kibinadamu. Madhumuni ya vitendo hivi ni ukoloni ili kudumisha ushawishi juu ya Yemen kwa nchi zinazoipigania, pamoja na kupora utajiri wa Yemen unaowatosha watu wake na zaidi, lau si kwa kuwepo watawala vibaraka walioiwezesha Marekani na Uingereza kupora mali hizo za kaskazini na kusini mwa Yemen, ambazo kama zingetolewa kwa hazina za serikali za Sana'a na Aden, zingewatosheleza watu wa Yemen, na zingeongeza mapato kutokana na mafuta, gesi na bandari, pamoja na yale wanayolazimishiwa watu kwa dhulma katika suala la kodi, ushuru, zakat - ambayo inachukuliwa kutoka kwa watu kwa njia ya haramu - na wakfu na vyanzo vyengine vya mapato vinavyoonekana na vilivyofichika ambavyo watu wengi hawavijui, lakini Mwenyezi Mungu anavijua. Pamoja na upekee wa Mahouthi katika maeneo yao ya udhibiti wa ada na mirabaha wanayolazimishiwa watu kwa majina mengi, ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremshia mamlaka, watakuwa na majuto kwa wale watakaoyachukua Siku ya Kiyama, nao wataungua ndani ya moto.

Kanuni ya kibepari iliyotabanniwa na nchi za Magharibi ni sababu ya moja kwa moja ya umaskini na kuenea kwa njaa na magonjwa barani Afrika na nchi nyingi za Amerika ya Kusini na Asia, pamoja na Yemen, ambapo Benki ya Dunia, taasisi ya kikoloni inayoongozwa na Marekani, ilitajwa na Meneja Mkurugenzi wake wa Uendeshaji, Axel van Trotsenburg, mnamo 18/01/2023 kwamba: “...zaidi ya watu milioni 130 wanaweza kusukumwa kwenye umaskini uliokithiri na mabadiliko ya tabianchi,”  Magharibi, basi, inawajibika kuongeza idadi ya masikini, kwa sababu inawajibika kwa mabadiliko ya tabianchi. Yote ambayo dunia inateseka kwayo katika umaskini, njaa, ukosefu wa dawa, huduma za afya na elimu n.k yanasababishwa na mfumo dhalimu wa kibepari unaotekelezwa duniani na kutawalishwa na dola zake kuu za kikoloni, makampuni yao, taasisi zao za fedha, na sarafu zao ndani yake, kushusha thamini sarafu za wengine na kuzijaza madeni ya riba.

Ni dhahiri kwamba misaada hii katika historia yake yote haikufikia manufaa ya watu wa Yemen, bali ilipata maovu yake kupitia njaa na utegemezi zaidi, na bado watu wa kawaida nchini Yemen hawatambui ukubwa wa hatari ya kutoa misaada kwao, lakini unyenyekevu wao unawaambia kwamba wamefaidika na misaada inayotolewa na nchi za Magharibi kupitia Umoja wa Mataifa. Ama watawala na baadhi ya watu wanaowazunguka wanatambua uzito wa wanayoyafanya, lakini kwa upande wao wanajisifu kwa kufanya sehemu ndogo ya maslahi kama vile kujenga baadhi ya shule na madaraja na kuendesha mambo ya serikali katika mustakbali wa karibu, na kuviacha vizazi vijavyo kukabili kile ambacho mikono yao imekiharibu.

Kwa jumla, misaada ni ukoloni wa kiuchumi wenyewe ambao hautofautiani sana na ukoloni wa kisiasa na kijeshi, kwa sababu matokeo yake ni yale yale, ambayo ni kuongeza utegemezi kwa nchi za Magharibi na kuwatia minyororo watu kuahirisha mabadiliko sahihi kwa misingi ya Uislamu. Umma hautakombolewa kutokana na vikwazo vilivyouzunguka isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi, ambayo wakati wake umewadia baada ya utawala wa kutenzwa nguvu kukaribia kuangamia kwake na kupinduliwa serikali yake. Mtume (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu