Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  3 Rajab 1444 Na: HTY- 1444 / 11
M.  Jumatano, 25 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu wa Yemen: Huu ni Mwezi wa Rajab ambao kwao Uislamu Uliingia Nchini Mwenu Basi Inukeni na Mfanye Kazi Kuirudisha katika Uhalisia wa Maisha Yenu
(Imetafsiriwa)

Watu wa Yemen husherehekea Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Rajab kila mwaka, tukio muhimu kwao, ambalo ni kuingia kwa watangulizi wao katika Uislamu. Ndani yake wanatoa sifa na shukrani zao kwa Mwenyezi Mungu kwa neema ya Uislamu. Mji mkuu Sana'a, eneo la Al-Janad katika Jimbo la Taiz, eneo la Zabid katika Jimbo la Al-Hodeidah, pamoja na Tarim jijini Hadramout ndio mikoa mingi zaidi ya Yemen kusherehekea tukio hili kutokana na hadhi ya kidini na kihistoria ya maeneo haya, ambayo yanafungamana na kuingia kwa Uislamu Yemen. Imam Ali bin Abi Talib (radhi za Allah ziwe juu yake) alifika Sana'a kama mjumbe wa Mtume Mtukufu (saw) kuwalingania watu wa Yemen kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu, ambako alifanya kazi ya kuasisi Msikiti Mkuu jijini Sana'a. Imesimuliwa kwamba, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alipofika Sana'a, alitoa khutba kwa makabila ya Hamdan, wakakusanyika sehemu ambayo sasa inaitwa Soko la Al-Halaqa, kaskazini mwa Msikiti Mkuu katika Sana'a ya Kale. Waliathiriwa na ujumbe wake na kusilimu, na Hamdan wote wakasilimu kwa siku moja. Swahaba mtukufu Muadh bin Jabal, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, naye alifika katika eneo la Al-Jund, na akaasisi Msikiti wa Al-Jund huko. Abu Musa al-Ash’ari, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alifika kwenye viunga vya Tihama na akajenga Msikiti wa al-Ash’ari huko Zabid.

Wakati huo, Yemen iligawanyika kati ya vikosi vya kikabila: Himyar, Hadhramaut, Kinda, na Hamdan, na kati ya utawala wa Kifursi jijini Sana'a na Aden na viunga vyake, na kati ya eneo la Najran la ushawishi wa Kihabeshi wa Kirumi, ambalo ni eneo walipokuwa Wakristo wa Najran. Migawanyiko hii ilimalizika tu kwa Uislamu, ambao watu wa Yemen waliingia kwa ujumla kwa njia ya amani na kwa makundi kati ya mwaka wa sita wa Hijra na mwaka wa wajumbe katika mwaka wa kumi wa Hijra. Pamoja na hayo, watu wa Yemen waliritadi kutoka kwa Uislamu baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambacho kilipelekea Khalifa Abu Bakr As-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutuma majeshi matatu nchini Yemen, na matokeo yake ni kwamba watu wake warudi tena katika Uislamu, baada ya wengi kuuawa, na wale aliowakidhia Mwenyezi Mungu kuwafanyia wema wakaregea katika Uislamu, na baada ya hapo watu wa Yemen wakaanza kukusanyika pambizoni mwa fahamu ya Umma na sio fahamu ya kabila au ukoo, na mwanzo wao baadaye ukawa katika kueneza Uislamu, huku wakitoka na ufunguzi wa Kiislamu katika jeshi la Amr ibn Al-Aas na majeshi mengine. Wengi wao waliishi Ash-Sham na nchi mbalimbali za Kiislamu. Andalusia ni shahidi wao kwa makasri yale yanayoitwa kwa majina yao, kama vile Kasri la Hamdan huko Granada, Kasri la Khawlan huko Seville, Kasri la Yassab na mengineyo. Idadi ya Maulamaa wenye elimu wao inashuhudiwa nchini Iraq, Ash-Sham na Andalusia, miongoni mwao kundi la wanazuoni kama vile Kadhi Amir bin Sharahil Al-Sha'bi, Masruq Al-Hamdani, Talha bin Ma'raq Al-Hamdani. Al-Yami, Ibrahim Al-Nakhai Al-Madhaji, Al-Ashtar Al-Nakhai na wengineo. Maarufu zaidi kati yao ni Malik bin Anas Al-Asbahi, Imamu wa Sunnah, Kadhi Ayad Al-Hasabi, Abd Al-Rahman Al-Ghafiqi, mmoja wa viongozi mashuhuri, na Mansour bin Abi Amir Al-Ma'afari mtawala wa Andalusia.

Enyi Watu wa Iman na Hekima: Haya ndiyo waliyoyatolea mababu zenu kwa Uislamu, basi je nyinyi mumetoa nini kwake?!

Mumeuweka Uislamu nyuma ya migongo yenu, na kuubadilisha na hukmu za kafiri Magharibi - mfumo wa kijamhuri wa kisekula, wa kidemokrasia - kama mfumo wa maisha na njia ya maisha, kisha mkazidisha uadui baina yenu, mnapigana baina yenu, damu yenu inatiririka baina yenu kwa dhulma katika kuwatumikia maadui zenu, na mnajisalimisha kwa watawala wanaowapeni adhabu kali, wakikuhukumuni kwa yale asiyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na wanaitoa mali ya nchi yenu kwa kafiri Magharibi ili waifurahie huku mukiwa na njaa! Basi, baada ya yote haya, mumeachana na lipi katika maelezo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusu nyinyi na wazee wenu katika Hadith iliyopokelewa na Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«أَتَاكُمْ أَهْلُ الْيَمَنِ هُمْ أَرَقُّ أَفْئِدَةً وَأَلْيَنُ قُلُوباً، الْإِيمَانُ يَمَانٍ وَالْحِكْمَةُ يَمَانِيَةٌ»

Wamekujieni watu wa Yemen ambao wana vifua vyepesi na nyoyo laini, Imani ni ya Yemen na hekima ni Yemen”?!

Lazima mutoke kule muliko. Kimsingi mnapaswa kuwa wabebaji wa Dini ya Mwenyezi Mungu kama alivyokuamrisheni, wala msiwe kama alivyosimulia Ibn Omar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, akasema: Nimesikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«إِذَا تَبَايَعْتُمْ بِالْعِينَةِ، وَأَخَذْتُمْ أَذْنَابَ الْبَقَرِ، وَرَضِيتُمْ بِالزَّرْعِ، وَتَرَكْتُمْ الْجِهَادَ، سَلَّطَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ ذُلّاً لَا يَنْزِعُهُ حَتَّى تَرْجِعُوا إِلَى دِينِكُمْ»

“Mnapouza chochote kwa mkopo, kwa sharti kuwa mutakinunua tena kwa bei ya chini (al-'Einah), mukashikilia mikia ya ng’ombe, na mukaridhia mazao, na mukaachana na Jihad, Mwenyezi Mungu atawasaliti kwa udhalilifu juu yenu ambao hatauondoa mpaka murudi kwenye dini yenu.”

Munastahiki hilo, basi inukeni na mushirikiane na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili mupate kheri ya dunia na Akhera na neema zake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu