Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  20 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 04
M.  Jumatano, 23 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wafungwa 31 wa Zamani wa Kisiasa Wanakaribia Kufika Mahakamani
(Imetafsiriwa)

Kulingana na habari tulizopokea kutoka kwa vyanzo vya kuaminika, huku mahakama ya rufaa ya wafungwa 15 wa zamani wa kisiasa ikifanywa huko Tashkent, kesi nyengine kubwa iko karibu kuanza, wakati huu ikiwa na watu 31. Hawa ni wanachama ambao hapo awali walikaa zaidi ya miaka 20 katika magereza ya utawala dhalimu wa Karimov, ambapo walikamatwa, kama vile wafungwa 23 wa zamani wa kisiasa, kwa mashtaka ya uongo. Wengi wao ni wanachama ambao walikamatwa katika mikoa tofauti ya nchi na kuhamishiwa mji mkuu. Hii inafanya idadi ya wafungwa wa zamani wa kisiasa ambao wamekamatwa, kuchunguzwa na kuhukumiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kufikia 54. Hivi majuzi, wanachama hawa 31 waliombwa kutia saini hati ya mashtaka iliyotolewa dhidi yao. Ndiyo, tunapokea taarifa kama hizo kuwahusu kutoka tu kwa vyanzo vichache vya ndani. Si vyombo vya habari vya ndani wala vya nje ya nchi, ambavyo havipitwi na hata matukio madogo zaidi nchini Uzbekistan, wala mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kibiashara, ambayo yanafanya kazi katika uwanja wa haki za binadamu, yalitaja. Umbile lao halisi lilidhihirika zaidi wakati wa matukio haya.

Mtu yeyote asiyependelea upande wowote anayeijua Hizb ut Tahrir hawezi kujizuia kushika ukosi wake (kwa kupinga) anaposikia tuhuma hii. Pia walishtakiwa chini ya vifungu sawa vya lazima; 159, 242 na 244 vya Kanuni ya Adhabu ya serikali. Lakini ushahidi uliotolewa dhidi yao katika hati ya mashtaka sio tu wa jinai, ni upuzi. Kwa mfano, washtakiwa wanafanya taaluma ya aina gani, iwe wanawaona ndugu zao kwenye harusi, mahali wanapokutana na kuzungumza na watu wengine. Vile vile imetajwa kuwa walikuwa na shauku ya kufanya amali zinazochukuliwa kuwa ni faradhi na zinazopendekezwa katika Uislamu, kama vile kushiriki katika kuwasaidia masikini, kuunga mkono fikra ya kurudisha Khilafah na kuishi kwa mujibu wa Uislamu. Lakini kwa mtazamo wa Uislamu, matendo yote haya ni elimu ya kawaida. Lakini kwa vile mfumo unaotekelezwa na serikali ya Uzbekistan si wa Kiislamu, unawachukulia wanachama hawa kama wahalifu, na wanashtakiwa ili kuwahadaa na kuwaharibia sifa zao mbele ya Waislamu wetu.

Ni muhimu pia kuzingatia kwamba mnamo Julai mwaka huu, Rais Mirziyoyev alifanya uamuzi wa kuwakumbuka mababu zetu ambao walikandamizwa na serikali ya Usovieti. Jambo la kushangaza ni kwamba, wahasiriwa wa utawala wa kikomunisti karne moja iliyopita wanakumbukwa, huku wahasiriwa wa serikali ya Karimov ya umwagaji damu, ambao walinyongwa kwa ukandamizaji na mateso ya kikatili, serikali hii haiwajali kabisa. Kinyume chake, utawala huu dhalimu unajaribu kuwatia jela vijana wa Kiislamu waliotoka katika kinu dhalimu cha utawala huu, wakiwa dhaifu kimwili, kwa miaka mingi zaidi. Kwa kweli, ikiwa viongozi wa serikali wangekuwa na uadilifu, wangewaheshimu waliokandamizwa kwa dawa kwa ajili ya majeraha ya mwili na kisaikolojia waliyotiwa gerezani. Baya zaidi wanachama hao walituhumiwa kwa uongo kufadhili na kuunga mkono ugaidi. Hivyo basi, je, tutayaitaje mahusiano yanayoendelea na umbile la kigaidi la Kiyahudi linalowaua ndugu na dada zetu Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na kulitambua kuwa ni dola?! Na kwa vile serikali ya Uzbekistan inalinda ubalozi wa umbile hilo lililolaaniwa na haifikirii hata kukata mahusiano ya kisiasa na kiuchumi nalo, je, kwa hakika huu sio msaada kwa ugaidi?!

Tuna wasiwasi mkubwa kwamba kesi ya wanachama hao 31 itakuwa sawa na kesi ya awali ya wanachama 23. Pia, hukumu zilizosomwa katika mahakama hii zimeandaliwa mapema, na mahakama inafanywa tu kwa ajili ya macho ya watu pekee. Wanachama hao hivi karibuni walitoa ushahidi wao mbele ya Mahakama ya Rufaa kwamba waliowahoji waliwaambia wazi kuwa wao ndio watatoa uamuzi huo, sio mahakama. Bila shaka, kufungwa tena kwa wanachama hawa waliodhulumiwa ni amri kutoka kwa duara za juu zaidi za kisiasa, ambazo zinalenga kuzifurahisha dola za kikoloni kama vile Urusi, hakuna shaka juu ya hilo. Kwa hiyo, tunaionya sana serikali ya Uzbekistan dhidi ya kulaaniwa na kina mama, wake, watoto, jamaa na familia za wanachama hawa! Kwani, matokeo ya kujihusisha na kitendo cha kinyama cha kuwafunga na kuwakandamiza watu wasio na hatia kwa jina la kuwaridhisha maadui zetu si lolote ila aibu na dhambi. Kesho Akhera mtapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na mtakuwa kuni za Moto wa Jahannam! Tunarudia tena kwa watu wetu Waislamu, msikae kimya kuhusu dhulma ya utawala huu usio na mipaka, na tumieni nguvu na uwezo wenu wote kuwasaidia wale wanaofanya kazi ya kutafuta ukweli na haki! Vyenginevyo, mateso haya yatatokea kwa kila mmoja wenu kwa njia moja au nyengine. Mtume wetu Mtukufu (saw) amesema: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ الْمُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً مِنْ عِنْدِهِ، ثُمَّ لَتَدْعُنَّهُ فَلَا يَسْتَجِيبُ لَكُمْ» “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake! Lazima muamrishe mema na lazima mukataze maovu, au Mwenyezi Mungu atakaribiwa kukuleteeni adhabu kutoka kwake, kisha mtamwomba, lakini hatakujibuni.” [Imesimuliwa na Ahmad]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu