Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  11 Jumada I 1444 Na: 1444 / 04
M.  Jumatatu, 05 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuharakisha Mahusiano Kati ya Serikali ya Uzbekistan na Marekani Kwaongeza Hofu ya Urusi
(Imetafsiriwa)

Serikali ya Urusi ilijibu hadharani kuimarisha uhusiano kati ya serikali ya Uzbekistan na Marekani. Hii ilikuwa wakati wa ziara ya Spika wa Jimbo la Duma la Urusi, Vyacheslav Volodin, huko Uzbekistan, ambayo ilianza Novemba 27, na katika tangazo rasmi la mwisho wa ziara hiyo lililowekwa kwenye tovuti ya Jimbo la Duma la Shirikisho la Urusi. Taarifa hiyo ilisema kuhusu ziara ya mara kwa mara ya Marekani nchini Uzbekistan: “Wamarekani wanakuja wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini tabasamu la mbwa mwitu linaonekana ... kwa hivyo itakuwa wazi ni nani aliyekuja.” Kwa kuzingatia hatari kubwa ambayo Marekani inaitokeza kwa Asia ya Kati, hasa Uzbekistan, ilisemwa: “Watu nchini Uzbekistan ni wenye hekima, wanajua kusoma na kuandika, wanaelewa kile ambacho ahadi hizi zinaweza kupelekea.” Baada ya ziara ya Volodin kumalizika mnamo 1 Disemba, Waziri Mkuu wa Urusi Mikhail Mishustin alizuru Uzbekistan mara moja. Mbali na maoni ya Volodin, pia alizikashifu nchi za Magharibi. Pia aliisihi Uzbekistan kujiunga na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Eurasia inayotawaliwa na Urusi haraka iwezekanavyo. Alizungumza kuhusu haja ya muungano wa gesi kati ya Urusi, Kazakhstan na Uzbekistan ambao Putin aliupendekeza hivi majuzi.

Ni wazi kutokana na hili kwamba wasiwasi wa Urusi unaongezeka kuhusiana na kushadidishwa uhusiano unaolenga kuimarisha ushawishi wa nchi za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, katika Asia ya Kati, hasa nchini Uzbekistan, kupitia ziara za maafisa wa ngazi mbalimbali. Kama tulivyosema katika taarifa zetu za awali, ilitarajiwa kwamba Marekani na nchi nyingine za Magharibi zingechukua fursa ya kujishughulisha kwa Urusi na Ukraine. Baada ya hili kuthibitishwa kivitendo, muitiko wa Urusi leo umekuwa jambo la kimaumbile, na ingali inaiona Asia ya Kati kama shamba lake na inaamiliana nayo kwa ubwana, na bado haijaachana na madai yake ya kuwa dola kubwa yenye nguvu. Bado haijaacha madai yake ya kuwa dola kubwa yenye nguvu. Ndio maana taarifa rasmi baada ya ziara ya Volodin nchini Uzbekistan ilitolewa kwa sauti kubwa na kwa vitisho. Urusi imeonyesha hofu yake kubwa ya kuongezeka kwa ushawishi wa Marekani na Magharibi katika eneo hilo, inayozingatia kuwa ni lake. Hofu yake ilionyeshwa katika onyo lake kali kwa Uzbekistan.

Dola za kigaidi kama vile Urusi na Marekani ambazo zinaijaza dunia vita na machukizo mengine zinalenga kuiingiza nchi yetu ndani ya duara lao la ushawishi na hivyo kuwafanya watu wetu kuwa watumwa na kupora mali zetu. Na haijalishi Urusi au Magharibi inaongozwa na Marekani au wengine, kwani sisi Waislamu hatutarajii mema kutoka kwao. Watawala wetu walionyakua madaraka kwa nguvu hawana jambo jengine zaidi ya kuwaridhisha wakoloni makafiri na kushikilia viti vyao vya ufalme kwa muda mrefu. Ndio maana sisi Waislamu hatupaswi kughafilika na ulaji njama kati ya dola kubwa na watawala wetu ambao wamekuwa vibaraka wao. Na hatuna budi kufahamu kwamba mabadiliko ya kweli yatatokea tu kwa kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, na kwamba ni Khilafah pekee ndiyo itakayotukomboa kutoka katika utawala wa wakoloni wa makafiri na kutulinda kutokana na ukandamizaji na unyanyasaji wao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu