Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  6 Sha'aban 1445 Na: 1445 / 16
M.  Ijumaa, 16 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wale Walioiacha Gaza Kufa Hawawezi Kusimama Dhidi ya Uvamizi
(Imetafsiriwa)

Baada ya miaka 12, Rais Erdogan alifanya ziara rasmi nchini Misri na kukutana na Rais wa Misri Sisi. Viongozi hao wawili walitia saini taarifa ya pamoja kuhusu marekebisho ya vikao vya Baraza la Ushirikiano wa Kimkakati wa Ngazi ya Juu. Katika hotuba yake kwenye mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika baada ya mikutano kati ya wajumbe hao wawili, Rais Erdogan alitoa kauli zifuatazo: “Hatutaki kuona mizozo, mivutano au migogoro yoyote barani Afrika, Mashariki ya Kati au kwengineko katika jografia ya jamaa yetu. Kwa hivyo, tumedhamiria kuongeza mazungumzo yetu na Misri katika ngazi zote ili kuweka amani na utulivu katika eneo letu. Rais alisema katika hotuba yake kwamba "wataendelea kushirikiana na kusimama katika mshikamano na ndugu na dada zetu wa Misri ili kukomesha umwagaji damu huko Gaza." Akiongeza kuwa, "Kupunguzwa kwa watu wa Gaza hakukubaliki kabisa. Tunakaribisha na kuunga mkono msimamo thabiti wa Misri kuhusu suala hili. Utawala wa Netanyahu lazima ujizuie kupanua mauaji yake hadi Rafah. Katika hotuba yake kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Erdogan alisema kwamba "hawapaswi kuruhusu wazimu kama huo ambao unaweza kusababisha mauaji ya halaiki."

Ziara ya Rais Erdogan nchini Misri na mkutano wake na Sisi zinaonyesha kwamba anakubali mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013 na usimamizi wa Sisi wa mapinduzi hayo kuwa halali. Wakati huo huo, hali hii inadhihirisha kwamba Erdogan haamini katika demokrasia anayozungumzia kila mara, na kwamba anapuuza matakwa ya watu ambao anatakiwa kuwathamini sana. Ziara hii inachukuliwa kuwa ni usaliti kwa Waislamu waliouawa katika Viwanja vya Nahda na Rabaa na damu kumwagika. Pia, Erdogan ambaye jana alimwaga machozi kwenye televisheni kwa ajili ya Waislamu waliouawa na waliopanga mapinduzi, leo amemtaja Al-Sisi, muuaji wa Asmaa El-Beltagy kuwa ni ndugu yake! Erdogan, ambaye alisema kamwe hata keti meza moja na Sisi, ambaye alimhukumu Mohamed Morsi na marafiki zake jela, alijidanganya tena na kuwahadaa Waislamu kwa kusema kwamba alifanya ziara hii kwa ajili ya amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati!

Ziara hii, ambayo ilikuja ndani ya mfumo wa uhalalishaji mahusiano, haikuwa kwa maslahi ya Uturuki, Misri, au watu wa Palestina, bali kwa maslahi ya Marekani hasa. Kwa sababu viongozi hao wawili kwa mara nyengine walithibitisha kwamba watafanya kazi kwa maslahi ya Marekani katika eneo hilo kupitia mikutano ya Baraza la Ushirikiano wa Kimkakati wa Ngazi ya Juu iliyofanyiwa marekebisho. Kadhalika, viongozi hao waliotuma ujumbe kwamba wataendeleza ushirikiano na mshikamano ili kukomesha umwagaji damu huko Palestina hawakuficha aibu yao siku ya shambulizi la mabomu katika mahospitali lililofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi, ambalo halikusaza hata jiwe mjini Gaza na kuuawa karibu Waislamu 30,000. Kwa kuthamini kazi na juhudi za Sisi, ambaye aliufunga mpaka wa Rafah kwa miezi kadhaa na kuwalaani watu wa Gaza kwa njaa na umasikini, si kingine bali ni huzuni na dhulma kwa watu wa Palestina na Waislamu wote. Erdogan kwa mara nyingine tena alionyesha ugumba wake kwa kuomba msaada kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kusitisha vita huko Gaza, na alionyesha kwamba msemo "dunia ni kubwa kuliko nchi tano" ni maneno matupu tu.

Enyi Waislamu! Misri na Uturuki ni nchi mbili ambazo zinafanya kazi kwa maslahi ya kikanda ya Marekani na ni watiifu kwao. Kwa sababu hiyo, ziara ya Rais Erdogan nchini Misri na kukutana kwake na kiongozi wa mapinduzi Sisi, si kwa ajili ya maslahi ya Gaza wala watu wa Palestina, bali ni kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi maslahi ya Marekani. Kwani nchi hizi mbili zinasubiri kwa hamu kumalizika kwa vita vya Gaza ili kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu. Kwa sababu hii, wanamshikilia Netanyahu peke yake, na sio umbile la Kiyahudi, linalowajibika kwa ukatili na mauaji ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku 130. Pia wanaendelea kurudia "mpango wa suluhisho la dola mbili" ambao Marekani iliwafanya waukariri. Wale walioiacha Gaza kufa hawawezi kusimama dhidi ya uvamizi huo, kwa hivyo musidanganywe na uwongo wao na musiingie kwenye mtego wao. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِنْ لَا يَشْعُرُونَ]

Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.” [Al-Baqara 2:12].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu