Jumatatu, 04 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  9 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 03
M.  Jumatano, 05 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuwa "Mzayuni Mkubwa" Kunamaanisha kuwa kama Putin na Kusaidia Uvamizi Kikatili na Haramu

(Imetafsiriwa)

Katikati ya uchumi unaofeli, mfumko wa bei wa tarakimu mbili, viwango vya rehani vinavyoongezeka, bili za juu za kawi, mabadiliko ya kodi, kupanda kwa deni, mgogoro wa pesa za mfuko wa pensheni, vita nchini Ukraine, sarafu inayoshuka thamani, ongezeko la uhamiaji na idadi inayodidimia ya wapiga kura, Waziri Mkuu mpya wa Uingereza (na labda nusu ya baraza lake la mawaziri) alipata wasaa wa kujitokeza kwenye hafla ya kando ya CFI kwenye dhifa ya kongamano lao la chama ambapo alijitangaza kwa fahari kuwa "Mzayuni mkubwa." Wengine katika hafla hiyo pia waliitaka Uingereza kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem. Pia alisema kwamba Uingereza itafanya kazi na washirika wake ili kuizuia kwa pamoja Iran kupata silaha za nyuklia.

Ingawa nyingi ya kauli hizi sio mpya, kwa hakika Waziri Mkuu wa sasa kama Waziri wa Mambo ya Nje alitoa kauli nyingi kama hizi, ni muhimu kusisitiza mambo yafuatayo:

Kuwa "Mzayuni mkubwa" inamaanisha kwamba unaunga mkono uvamizi katili wa umbile la Kizayuni wa karibu miaka 75. Uvamizi ambao hata ripota maalum wa Umoja wa Mataifa na mashirika kadhaa ya haki za binadamu ya Magharibi yameutaja kama "mfumo wa ubaguzi wa rangi." Ni unafiki wa kipekee kulaani uvamizi katili wa Putin kwa Ukraine na kisha kufumbia macho kile kinachotokea kwa watu wa Palestina. Kwa hakika kukosekana kwa kauli zozote kuhusu masaibu ya Wapalestina katika hafla hiyo kunaonyesha wazi wazi sio tu ukosefu wa huruma kwa binadamu, bali ubaguzi mkubwa na upendeleo katika ngazi ya kitaasisi.

Nini kingine tutarajie kutoka kwa utawala wa Uingereza iliyounda tatizo la umbile la Kizayuni, ikalichonga eneo hilo na kisha ikachochea vita miongoni mwa raia wake wa zamani. Kuvunjwa kwa Khilafah (Ukhalifa), Tangazo la Balfour na Sykes-Picot vilikuwa vipengee muhimu sana katika historia ya kuchosha ya kikoloni ya Uingereza.

Wengi katika utawala wa Uingereza ni wepesi kulaani upinzani wa Wapalestina: wakiuita ugaidi, lakini wanasahau kwa urahisi kwamba umbile lenyewe la Kizayuni lilianzishwa kwa vurugu za magaidi wa Stern na Irgun, mauaji ya wanajeshi wa Uingereza katika Hoteli ya King David na mauaji ya kikabila ya Wapalestina 700,000.

Ni dhahiri kwamba uungaji mkono wa Waingereza kwa umbile la Kizayuni hautokani na "maadili ya pamoja ya kidemokrasia" (tukiweka kando kwa sasa kwamba fahirisi ya EIU inaiita dola ya Kizayuni "demokrasia yenye dosari" na mashirika ya haki za binadamu yanaiona kama "dola ya ubaguzi wa rangi"); bali imejikita imara ndani maslahi ya kibiashara, kiuchumi na kiteknolojia ambayo yanawanufaisha tu 1% ya kipote cha matajiri. Isitoshe Uingereza ina historia ndefu ya mahusiano ya karibu na biashara na mataifa kidikteta ndani ya Ghuba.

Mjadala kuhusu kuhamisha balozi hauhusiani na nembo, majengo, wala maeneo. Ni sehemu ya jaribio la kuendelea la umbile la Kizayuni kuhalalisha uvamizi wake haramu kufuatia Makubaliano ya Abraham. Jerusalem sio mji mkuu wa umbile la Kizayuni, lakini ni moja ya miji mitakatifu zaidi duniani, eneo la kibla cha kwanza na mahali ambapo Mtume Muhammad (saw) alisafiri usiku kabla ya kupaa mbinguni (Isra na Miraj).

Unafiki wa kuendelea wa Magharibi juu ya nani anapata silaha za nyuklia hauzeeki. Kuishutumu Iran huku ikifumbia macho silaha zake wenyewe kubwa za nyuklia na zile zinazomilikiwa na umbile la Kizayuni kunaweza kusikika kuwa jambo la kuaminiwa jijini Birmingham, lakini kunakabiliwa na dhihaka na kejeli katika sehemu kubwa ya dunia.

Kwa hivyo Waislamu wanapaswa kujibu vipi?

Ni muhimu kutofautisha kati ya Uzayuni na Uyahudi. Ni muhimu kutambua kwamba Uzayuni una uhusiano mdogo sana na Uyahudi. Wengi wa viongozi wa awali wa Kizayuni walikuwa wapagani, wakati Wayahudi wengi waliojitolea katika Uyahudi wanapinga kikamilifu malengo ya Uzayuni.

Dola ya Kiislamu inayotabikisha Shariah ya Kiislamu, ingawa inapinga vikali Uzayuni na uikaliaji kimabavu Palestina, kwa hakika inalinda haki za Mayahudi za kutekeleza imani yao. Ukweli ni kwamba wanachuoni mashuhuri wa Kiyahudi wanataja jinsi Uislamu ulivyowaokoa Mayahudi (k.m. Wasserstein katika Mkusanyiko wa Matukio ya Kihistoria ya Kiyahudi 2012); kwanza kutoka kwa Warumi wa Byzantino na kisha kutoka kwa Baraza la Kuhukumu Wazushi la Uhispania. Khilafah ya Kiuthmani iliwapa hifadhi salama na hata kuwapa dori mashuhuri za kijamii. Ukweli usiofurahisha kwa wengi katika utawala wa Uingereza ni kwamba Waislamu na Mayahudi hawajatendeana uadui mbaya kwa muda mrefu wa miaka elfu mbili iliyopita, kama ilivyokuwa kwa Ukristo na warithi wao wa kisekula huko Magharibi ambao wamewalaumu Mayahudi ima kwa kumuua Masihi, kwa kuwa wa jamii duni au kwa kuwa na ushawishi usiofaa juu ya uchumi wao. Hakukuweko na mauaji ya kinyama yaliyofanywa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa namna ambayo wengi wa nchi za Magharibi wanasimama na watu wa Ukraine, Waislamu wanapaswa kusimama na watu wa Palestina katika wakati wao wa shida. Tunahitaji kusimama kidete kutetea suluhisho la Kiislamu la eneo hili na kusimama dhidi ya mashinikizo ya wanasiasa na vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo kinafiki kabisa vinajumuisha kutotambuliwa kwa uvamizi wa Kizayuni katika ufafanuzi wao wa misimamo mikali; mara kwa mara kuwatupia tuhuma za chuki dhidi ya Mayahudi wale walio dhidi ya Wazayuni.

Waislamu wanapaswa kutambua kwamba kujaribu kubadili msimamo wa utawala wa Uingereza ni kazi bure bila dola ya Kiislamu. Hili ni suala la siasa za kijiografia na kwa hivyo linahitaji ufundi wa serikali na makadirio ya nguvu. Hivyo basi, inabakia kuwa muhimu kuzibadilisha tawala dhalimu zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu, ambazo ima zinajihusisha na maneno matupu, kutia saini mikataba haramu, au kutofanya lolote kuwasaidia watu wa Palestina. Dola hizi zina uwezo wa kutosha katika upande wa watu, uchumi, nishati, miundombinu na rasilimali za kijeshi ili kukomesha dhulma na kuikomboa Palestina hivi sasa, lakini zinakosa imani, ujasiri na utashi wa kisiasa.

Kwa hiyo Waislamu lazima wanusuru kazi ya suluhisho la Kiislamu kwa Palestina: Khilafah kwa njia ya Utume. Ni kielelezo ambacho kitaleta uadilifu wa kweli katika eneo hilo, kuwabadilisha madhalimu na madikteta katika ulimwengu wa Kiislamu, kuikomboa ardhi inayokaliwa kwa mabavu, kutupilia mbali minyororo ya ukoloni, kukomesha dhulma na kuweka mfumo juu ya ulimwengu wa Kiislamu utakaowaruhusu Waislamu, Mayahudi, Wakristo na wengineo, kuishi kwa amani pamoja. Bila kujali kile kinachosemwa na Wazayuni ndani ya utawala wa Uingereza: historia na sheria za Uislamu ni ushuhuda wa wazi juu ya hili.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. [Al-Anfal:24]

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu