Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  25 Muharram 1438 Na: 1438 / 01
M.  Jumatano, 26 Oktoba 2016

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Upofu wa Moroko kwa Zama Zake Zilizo Pita na Mustakbali Wake

Mfalme Mohammed wa Sita wa Moroko amekamilisha ziara yake nchini Tanzania. Miongoni mwa mambo mengine, Rabat imeahidi kujenga msikiti mkubwa sana wa kisasa jijini Dar es Salaam na uga wa kisasa jijini Dodoma.

La kusikitisha, upeo wa sera ya kigeni ya Rabat ni duni mno, imejaa upofu na iko mbali na historia yake tukufu.

Ziara ya Mfalme huyo wa Moroko imekuja ndani ya muktadha wa maridhiano ya kusini kwa kusini na kutilia nguvu ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi. Kwani Moroko inaitaka Tanzania kuisaidia Moroko kurudi katika Muungano wa Afrika kama inavyo zitafutia kwa haraka kampuni zake kuwa ni fungamano lenye kuunganisha kati ya kampuni za kikoloni za Kimagharibi na rasilimali asili za Kiafrika. Moroko na Tanzania zilitia saini makubaliano ya mashauri 22 ya kiuchumi, kitamaduni, kitalii na kisiasa…

Moroko, kama zilivyo nchi zote za Waislamu, haina chochote kilichobakia kwake isipokuwa kuficha uovu wake na dhulma zake zilizo tokana na kubeba mtazamo wa Kimagharibi katika utawala na uchumi na juhudi zake za kueneza ushawishi wa kampuni za Mfalme huyo sawia na kampuni za Kimagharibi huku ikijificha nyuma ya ima kujidai kusimamia au kujenga misikiti mipya. Dori ya msikiti ni kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 (فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّهُ أَنْ تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ)

“Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.” [an-Nur: 36]

Kisha, vipi dola hiyo itajenga msikiti huku hukmu za Kiislamu zikiwa hazitekelezwi na hukmu za kikafiri ndizo zinazo tawala?

Zaidi ya hayo, ni lini ujenzi wa Msikiti umekuwa ndicho kipimo cha usahihi wa utawala na usahihi wa nidhamu zinazo tekelezwa katika dola na mujtama?

Je, Mfalme Hassan wa Pili, mtangulizi wa mfalme wa sasa hakujenga msikiti mkubwa jijini Casablanca, wa 13 kwa ukubwa duniani, ulio na mnara mkubwa zaidi kuliko msikiti wowote duniani, akitumia rasilimali na juhudi nyingi sana kwa miaka saba? Nini kilicho jiri baadaye? Je, Moroko na ulimwengu wa Waislamu uliamka na kuinuka kutokana na mporomoko na idhilali?

Moroko inaugua katika nyanja zote; watu wake wanaishi wakiteseka kutokana na ufukara, usimamizi mbaya, nidhamu fisadi ya mahakama, elimu inayo zorota, sekta ya matibabu iliyo poromoka, na rasilimali asili na utajiri ukizunguka miongoni mwa Mfalme na wale wanaomtumikia na kukumbwa na ulitima wa kiakhlaqi. Ni nchi ambayo iliwahi kuwa chimbuko la elimu na hadhara ikiwa na Chuo Kikuu cha zamani zaidi duniani cha Al-Qarawiyyin; haina ujasiri wa kutumia lugha ya Kiarabu katika kiwango cha Chuo Kikuu.

Ni aina gani hii ya idhilali iliyo jisababishia yenyewe? Bila ya kutaja dori ya Rabat katika vita vya Kimarekani dhidi ya ugaidi, ambavyo kiuhalisia ni vita dhidi ya Uislamu vinavyo tekelezwa kwa niaba ya dola za Kimagharibi na Marekani na ambavyo pia vinahatarisha maisha ya raia wake mwenyewe.

Mfalme wa Moroko amefanya ziara nyingi eneo la Afrika Kaskazini na sasa anafanya ziara kwa dola za Afrika Mashariki (Tanzania na Rwanda huku ziara ya Ethiopia ikifutiliwa mbali). Katika ziara zote hizi anaonyesha historia tukufu ya Uislamu ya watu wa Moroko pamoja na Afrika. Lakini, kuna tofauti kubwa kati ya yule anayebeba Uislamu kama uongofu kwa ulimwengu na yule anayebeba urasilimali, demokrasia na kuzifungulia milango nchi za Kimagharibi kuifuja Afrika.

Ni lini Moroko itaondoa pazia ya upofu wa historia yake, na historia yake jumla ya Kiislamu? Ni nchi ambayo iliukubali Uislamu uliowaunganisha watu, kisha wakawa ni watu waliobeba uongozi wenye nidhamu na chimbuko la ukombozi kwa Waislamu na wanadamu. Hata wasiokuwa Waislamu walitafuta usaidizi kwake kutokana na udhalimu wa watawala wao. Kama ambavyo wakaazi wa Uhispania akiwemo mkarimu Visigoth, Julian (mheshimiwa wa Ceuta) waliwashajiisha Waislamu kuikomboa Ibera kutokana na mateso na dhulma za Mfalme Roderic. Miongoni mwayo ilikuwa ni Roderic kumbaka binti ya Julian.

Kupitia nchi hii, Uhispania ilifunguliwa chini ya Tariq bin Ziad na Uislamu pia ukapanuka hadi dola nyingi za Kiafrika. Kinyume chake ni kuwa historia hii tukufu, na hali ya leo, tofauti yake ni kama ardhi na mbingu! 

Endapo Moroko ingeshikamana na historia yake tukufu, ingelikomboa eneo lililo salia la Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia Uislamu, lakini badala yake imeukumbatia urasilimali ulioifanya kipofu kutokana na historia yake tukufu, na kukimbilia tu kuhifadhi utawala wao tete na kujaza matumbo yao pekee. Bila shaka, mabadiliko kamili ya Kiislamu ndio yanayo hitajika ili kuirudia historia yetu.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu