Jumatano, 06 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  2 Muharram 1445 Na: 1445 / 01
M.  Alhamisi, 20 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwaka Mpya wa Kiislamu Una Ujumbe Mzito wa Kimfumo, na Sio Jambo la Kisherehesherehe Tu

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kuingia mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1445 Hijria ambapo kwa mara ya kwanza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar rasmi imeifanya siku ya tarehe mosi Muharram kuwa siku ya mapumziko, huku Waislamu katika siku hiyo wakifanya amali mbalimbali za kuupokea na kuuadhimisha mwaka huo. Sisi katika Hizb ut Tahrir Tanzania licha ya kushiriki kikamilifu pamoja na Ummah katika baadhi ya amali hizo za kuupokea mwaka huo, tungependa kuweka bayana yafuatayo:

  1. Ni kutokana na busara, upeo wa Kiislamu na uoni mpana wa kisiasa ndio uliwafanya Maswahaba (ra) ndani ya mwaka 16 Hijria chini ya Khalifa Umar Khattaab kuwafikiana kwa umoja wao (ijmaa) kuasisi kalenda ya Kiislamu lakini pia kulichagua tukio la ‘Hijra’ kuwa ndio nukta ya kuanzia kuhesabu kalenda hiyo.
  2. Uteuzi wa maswahaba wa tukio la ‘Hijra’ kuwa nukta kianzio ya Kalenda ya Kiislamu ni kwa sababu ni kutokana na tukio hilo (Hijra) Waislamu waliweza kuasisi dola yao ya mwanzo ya Kiislamu, wakatoka katika hali ya unyonge na udhalili na kuja katika nguvu/izzah na mamlaka yaliyowawezesha kutekeleza Uislamu kivitendo baada ya kukosa chombo cha kuutekelezea ndani ya Makka kwa kukosa mamlaka. Hivyo, ‘Hijra’ ni mstari uliochora baina ya maisha ya awali ya Waislamu chini ya utawala wa Dar ul Kufr (dola ya kikafiri) ndani ya Makka kuelekea katika maisha matukufu na ya utawala adhimu wa Kiislamu wa Dar ul Islam ndani ya Madina.
  3. Uteuzi wa maswahaba wa tukio la ‘Hijra’ walidhamiria kugandisha ufahamu na kutukumbusha mpaka Siku ya Kiama juu jukumu la kuwa na Dola moja ya Kiislamu. Na pale itakapokosekana Umma una uwajibu na jukumu la kufanya ulinganizi, kutafuta Nusra ili kuirejesha tena dola hiyo.
  4. Tukio la ‘Hijra’ libebwe ufahamu wake kwa mtazamo ulio sawa na kwa usahihi wake. Lisioneshwe tukio hilo kuwa Mtume (saw) alihama Makka kwa uoga au akawe mkimbizi ndani ya Madina, ukaachwa kando ukweli kuwa Mtume (saw) wakati anafanya ‘Hijra’ tayari alikwishafikia makubaliano na viongozi wa Madina kumpa nusra na kukabidhiwa hatamu za uongozi ndani ya Madina. Hivyo, (Mtume Saw) aliwasili Madina akiwa tayari ni kiongozi aliyetarajiwa kuwasili. Aidha, tukio la ‘Hijra’ lisiangaziwe katika upande mmoja tu wa kimiujiza miujiza kama yaliyojiri katika pango, miujiza kwa Ummu Maabad, Suraqa nk. Hapana shaka miujiza hiyo tunaikubali na kuiamini kwa kuwa ni sehemu ya aqida yetu. Lakini nukta muhimu zaidi ya roho na uhalisia wa ‘Hijra’ ni kuleta mabadiliko ya Kiislamu. Hili ndilo funzo mama na nyeti (la Hijra) ambalo Ummah unastahiki kukumbushwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuuruzuku Ummah wetu ufahamu sahihi wa tukio hili nyeti na adhimu. Pia Tunamumba aujaalie mwaka huu 1445 Hijria, uwe mwaka wa Nusra na Ushindi  kwa kurejeshwa tena Khilafah Rashida kwa Manhaji/njia ya Utume - Amiin

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir

Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu