Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  2 Muharram 1446 Na: 01 / 1446 H
M.  Jumatatu, 08 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera ya Serikali ya Kisekula nchini Uturuki inayokula Njama Dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham ndiyo Sababu ya Kulipuka kwa Kiota cha Mapinduzi katika Ukombozi
(Imetafsiriwa)

Kauli za maafisa nchini Uturuki kuhusiana na maridhiano na utawala uliopitiliza na kufunguliwa kwa mipaka kwa ajili ya maandalizi ya uhalalishaji mahusiano na utawala huo, na vitendo vinavyouandama vya ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wa Syria hasa wa Kayseri ni matokeo ya kimaumbile ya maneno ya uchochezi dhidi ya watu wa Syria, wakimbizi wanaoukimbia utawala wa Assad, na wanasiasa nchini Uturuki, wawe wenye mamlaka au wa upinzani, yote haya si lolote bali ni kuonyesha sura halisi ya utawala wa Uturuki, ambao unatekeleza mpango wa Marekani katika eneo hilo kufikia kile wanakiita suluhisho la kisiasa na kurudisha yale mabaki ya mji uliokombolewa kwenye kumbatio la utawala wa kihalifu.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashirika ya habari, Kayseri alishuhudia kuvunjwa na kuchomwa kwa idadi kubwa ya mali za watu wa Syria, mashambulizi na vitisho vya kuuawa. Hii iliambatana na majaribio ya kulazimisha maeneo ya mapinduzi kufungua vivuko na utawala wa kihalifu jijini Damascus. Haya yote yalizua hisia kali katika maeneo yaliyokombolewa na vuguvugu la watu wenye nguvu dhidi ya sera ya njama ya serikali ya Uturuki, ambayo ukweli wake ulionekana wazi kwa watu wote wa mapinduzi.

Kilichotokea na kitakachotokea kwa watu wa Syria kimsingi kinatokana na utawala wa kihalifu wa Assad, kwa ushirikiano na utawala wa Uturuki, ambao umefanya kazi kubwa kwa miaka kadhaa kuua ari ya mapinduzi miongoni mwa watu na kukomesha mapinduzi na kuyakabidhi kwa utawala wa uhalifu...

Kilichotokea hivi karibuni nchini Uturuki kinalaumiwa utawala wa Uturuki, unaoongozwa na Erdogan, ambaye alitangaza katika mpango wake wa uchaguzi kwamba iwapo atashinda, atatekeleza mpango wa kuwafukuza Wasyria waliofukuzwa na kuwapeleka nchini kwao, ambao unaendana na kauli za upinzani nchini Uturuki dhidi ya Wasyria Ambayo ilisaidia kuendeleza matamshi ya chuki na tabia ya chuki ya ubaguzi wa rangi. Uhamisho pia ulianza kwa njia isiyo ya haki na ya kiholela, kwa wengi wa wale walio na ukaazi wa muda na wale ambao hawana.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alisema: “Muungano wa upinzani na utawala nchini Syria utakuwa jambo zuri na utaunda kikosi cha kukabiliana na SDF.” Msimamo wa utawala nchini Uturuki ulionekana pale Erdogan aliposema, “Hakuna mzozo kati yake na Rais Bashar, na kwamba wana uhusiano wa kifamilia, na hakuna kinachowazuia kukutana hivi karibuni.” Haya yote yalizua hali ya shinikizo kwa watu na kuongeza mvutano katika kiota cha mapinduzi, ambayo yalihamishwa kutoka kwenye nyumba zake na ndugu zake waliuawa, na makumi ya maelfu ya watu ambao wangali wanasota katika jela za kifo na mateso.

Haya yote yalitokea baada ya utawala wa Uturuki kucheza dori ya mdanganyifu na kusaidiwa katika hilo na viongozi walioajiriwa ambao walichukua udhibiti wa shingo za watu na kuwanyang'anya uamuzi wao na kumkabidhi mwalimu ambaye naye angeyakabidhi mapinduzi kwa utawala wa jinai katika kile kinachoitwa “suluhisho la kisiasa” hatari kwa mtindo wa Marekani.

Enyi watu wa Syria: Kuasi kwenu dhidi ya dhulma na dhidi ya siasa zinazokula njama dhidi yenu kumethibitisha mizizi ya ari ya mapinduzi ndani ya nafsi zenu, kama ilivyothibitisha uwezo wenu mnapoinuka na kufanya maasi, basi tumieni fursa hiyo na mufanye kazi ya kuregesha uamuzi wa mapinduzi yenu uliyoibiwa kwenu na wadhamini waliokula njama na zana zao kutoka kwa viongozi wa mfumo wa makundi.

Enyi Wanamapinduzi Wanyoofu: Ukweli kuhusu utawala wa Uturuki na ukweli kuhusu zana zinazohusiana nao kutoka kwa viongozi wa makundi umedhihirika kwenu... Hebu harakati zenu maarufu ziwe mbali na hamasa zinazokinzana na Uislamu, na mbali na mifarakano ya kibaguzi inayochukiza. Bali, zifanyeni ziwe harakati zenye baraka na ufufuaji wa mapinduzi ili kusahihisha mkondo na kuchukua uongozi wa kisiasa wa dhati na makini ambao utakuongozeni kuelekea kuupindua utawala wa kihalifu jijini Damascus na kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kuwa chanzo cha izza, ushindi, na kuwaunganisha Waislamu nchini Syria, Uturuki na katika nchi nyengine za Kiislamu kama ndugu waumini chini ya dola moja ambayo hakuna nafasi ya madai ya ubaguzi wa rangi wa Kijahiliyah (zama kabla ya Uislamu), lakini ambapo kila mmoja atakuwa ni ndugu wanaopendana na wanaoshirikiana katika kheri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ]

“Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.” [Al-Mu'minun 23:52]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu