Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  17 Shawwal 1444 Na: 12 / 1444 H
M.  Jumapili, 07 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Njama Mpya Inatayarishwa Dhidi ya Mapinduzi Yanayohitaji Kuingiliwa Upya na Ujasusi wa Hay'at Tahrir al-Sham
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili tarehe 7/5/2023, Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) alikamata idadi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria, akiwemo Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria, Ahmed Abdul Wahhab, Mjumbe wa Afisi ya Habari, Nasser Sheikh Abdul Hai, na baadhi ya wabebaji wa Dawah katika maeneo ya Idlib.

Ukamataji huu wa idara ya upelelezi ya HTS unajiri siku moja baada ya kukamatwa kwa mwanachama, Abd al-Razzaq Al-Masri Abi Al-Nour, katika mji wa Idlib.

Uvamizi huu wa huduma za kijasusi ni wa pili, baada ya uvamizi wake, ambao ulikuwa mwaka wa 2019, ambao wakati huo ulikuwa wa kutekeleza maamuzi ya Kongamano la Sochi, ambalo mhusika mkuu Uturuki alitia saini. Leo, uvamizi huu unakuja ili kutukumbusha kile kilichotokea, na kuthibitisha kwamba kuna awamu mpya ambayo ina nia ya kupinga mapinduzi kwa kuhalalisha mahusiano na utawala wa kihalifu na kufuata njia ya suluhisho hatari la kisiasa.

Hivyo basi, ilikuwa ni lazima, kwa mtazamo wao, kupunguza sauti ambazo zinaweza kusimama katika njia ya njama hii.

Watu wa mapinduzi na wajue kuwa uvamizi huu haukusudiwi wabebaji Dawah katika wanachama wa Hizb ut Tahrir na wenye kumiliki neno la haki pekee, bali ni ujumbe kwamba ambao itakuwa ndio hatima ya wale wanaozungumza neno la haki na wale wanaosimama katika njia ya utabikishaji wao wa maagizo ya mabwana zao.

Enyi Watu wa Mapinduzi: Mnakaribia hatua ya hatari katika maisha ya mapinduzi yenu, kichwa chake, kama tulivyowatajieni hapo awali, ni “kuhalalisha mahusiano na mapatano.” Ni wakati sasa wa nyinyi kuinuka na kusema ujumbe wenu kuhusu kile kinachotokea na kuzuia njama hii ovu inayo pikwa.

Ukamataji kama huo wa madhalimu kutawafanya tu wanachama wa dawah kuwa imara zaidi, na vitendo hivyo havitawavunja moyo katika kushikamana na neno la haki na kuamrisha mema na kukataza maovu, mpaka Mwenyezi Mungu (swt) aukirimu ulinganizi huu, wanachama wake na Ummah wetu wote kwa ushindi wa hivi karibu na kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hayo ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuyatimiza.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu