Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  6 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 09 / 1443 H
M.  Jumapili, 05 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuwapiga Risasi Waandamanaji
Ndio Njia ya Madhalimu ya Kuhalalisha Umwagaji Damu Tukufu ya Muislamu
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 3/6/2022, watu kadhaa walijeruhiwa kutokana na risasi za moto zilizofyatuliwa dhidi ya waandamanaji waliokuwa na hasira wakipinga kupanda kwa bei ya umeme na kukatika kwa umeme kwa saa nyingi, katika mji wa Afrin viungani mwa Aleppo kaskazini.

Sambamba na matukio ya Afrin, maandamano mengine yalifanyika mbele ya Shirika la Umeme katika mji wa Jindires katika viunga vya Afrin, ambayo yalikumbana na risasi za moto zilizofyatuliwa kwa waandamanaji, na kusababisha majeraha. Huku mmoja wa waandamanaji akifariki kutokana na jeraha alilopata, kisha maandamano yakafuata katika maeneo tofauti tofauti.

Kuhusiana na matukio haya, ni muhimu kusisitiza yafuatayo:

Kwanza: Kukabiliana na vuguvugu la waandamanaji kwa risasi za moto, na vitisho vya majiji, vijiji na miji, na uasi wao wa wakati mmoja kuunga mkono harakati za watu wetu huko Afrin, kunaturudisha kwenye kumbukumbu zetu siku za mapinduzi ya kwanza, inathibitishia mfanano wa fikra za kihalifu na umoja wa mkabala wake licha ya tofauti ya wale wanaoyatukana, na umoja wa mapinduzi licha ya hila za maadui zake kulipasua eneo lake na kutofautisha baina ya maeneo yake.

Pili: Harakati za watu za kuondoa ukandamizaji wa mfumo wa makundi, makampuni ya kutengeneza faida na mengineyo inaashiria uhai wa watoto wa Ummah huu, na kwamba mapinduzi yangali yanawaka moto ndani ya nafsi zao.

Tatu: Harakati ya pamoja yenye utambuzi na ikhlasi ni harakati changamfu na yenye natija, tofauti na harakati ya mtu binafsi au harakati inayoegemezwa kwenye miitikio, na ni dhamana na ngome ya kutoyadandia au kuyadhibiti kutoka upande wowote ule.

Nne: Kuzusha matatizo na migogoro kusiwapurukushe wanamapinduzi kutokana na njia yao msingi, ambayo ni kuipindua serikali na kusimamisha utawala wa Uislamu. Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hii ndio kadhia nyeti ya Waislamu ambayo kwayo Waislamu wanapaswa kuichukulia kipimo cha uhai au kifo.

Tano: Matukio ya kuchomwa moto na uharibifu na kusababisha ufyatuaji risasi na mauaji ni jukumu la serikali ya Uturuki na mfumo wa vikundi, uliokosa mtazamo wa uchungaji, na kutawaliwa na mawazo ya ukusanyaji ushuru.

Sita: Mfumo wa vikundi unaonasibishwa na ujasusi wa serikali; Ni mshirika katika kutia shinikizo watu wavunje azma yao, na kuwatengenezea matatizo ya pembeni ili kuwavuruga kutoka katika lengo lao kuu la kuipindua serikali na kusimamisha utawala wa Waislamu.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Aina zote za nishati kama vile mafuta, gesi, umeme, maji, au vitu vyengine vinavyotumika mithili ya mafuta majumbani au viwandani... Haviruhusiwi kwa dola au wahusika wengine kuwapa watu binafsi, taasisi au makampuni, kwa sababu nishati ni miongoni mwa mali ya Ummah. Kutoka kwa baadhi ya Maswahabah walisema:

«غَزوْتُ مَعَ النَّبِيِّ ﷺ، فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ: النَّاسُ شُرَكَاءُ فِي ثَلاَثٍ: فِي الكَلأِ، وَالمَاءِ، وَالنَّارِ»

“Nilipigana vitani pamoja na Mtume (saw) nikamsikia akisema, “Watu ni washirika katika vitu vitatu: katika malisho, maji na moto” [Imepokewa na Ahmad na Abu Dawud]. Neno "moto" linajumuisha aina zote za nishati zilizotajwa hapo juu. Dola katika Uislamu inalazimishwa na Uislamu kutoa nishati hii na kuisambaza miongoni mwa watu na inachukua tu ada ndogo kutoka kwao ambayo haizidi gharama ili kuandaa usambazaji huu na si kwa ajili ya faida.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, nyumba ya Uislamu:

Aina za dhulma na uchovu unaofanywa kwa watu hausababishwi tu na ufisadi wa mfumo wa makundi na ufisadi wa serikali, taasisi na makampuni yao, bali ufisadi wa mifumo na sheria wanazotunga zinazowahakikishia uporaji wa fedha za Ummah kwa maslahi yao ya kibinafsi.

Mifumo na sheria zinazotekelezwa katika yale yanayoitwa maeneo yaliyokombolewa na katika nchi nyingine za Waislamu ni mifumo ya kirasilimali ya kisekula, iliyotungwa na wanadamu, inayotenganisha dini na serikali, watu wanatunga sheria kwa mujibu wa maslahi, matakwa yao na matamanio yao, kwa gharama ya maslahi na mateso ya watu, zinazopelekea kwenye dhiki, ufukara na ugumu wa maisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلاَ يَضِلُّ وَلاَ يَشْقَى، وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 123-124].

Kwa hiyo, ni wajibu kwa Waislamu wote, ikiwa wanataka radhi za Mwenyezi Mungu (swt), na kuishi maisha ya utu na furaha chini ya utawala wa Uislamu, mbali na taabu, ni lazima wafanye kazi pamoja na watenda kazi ili kubadilisha uhalisia mbovu na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kwa kutamatisha, tunatoa wito kwa wanamapinduzi wetu katika maeneo yote yaliyokombolewa kuwa katika ngazi ya ufahamu na tukio, ili waone hila za maadui zao na mitego yao ya kisiasa, ambayo juu yake ni suluhisho hatari la kisiasa na katiba ya kisekula ya kikafiri ilioundwa na Amerika kupitia ala na ufundi wake… na kushikamana na ahadi yao ya kuendeleza mapinduzi yao hadi mwisho na kuhifadhi mihanga ya mashahidi wao; kwamba matunda yake yawe ni utawala wa Uislamu pekee, licha ya matakwa ya wale wote wanaotafuta njia potofu, miongoni mwa maadui wa Uislamu na wapambe wao katika ardhi zetu. Katika hayo umo utukufu wa dunia  hii na neema ya Akhera, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Azza Wa Jal.

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu