Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  14 Muharram 1442 Na: 01 / 1442 H
M.  Jumatano, 02 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Msururu wa kukamatwa kwa Mashababu wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah Syria; Na kampeni za Uzushi kwa Hizb kwenye Vyombo vya Habari Vilivyo Vitiifu kwa Dhalimu wa Al-Sham na Wengine katika Upinzani!

Hizb ut-Tahrir Yazindua Kampeni yake "HAPANA kwa uhalifu wa suluhisho la kisiasa, NDIO kuangusha kwa serikali na Kusimamishwa Khilafah"

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Syria ilizindua kampeni yake dhidi ya uhalifu wa suluhisho la kisiasa la Kiamerika mnamo tarehe 13/8/2020 M, na kuanza kuonya juu ya uhalifu huu mbaya; ambao utazalisha tena upya serikali ya dhalimu wa Ash-Sham; ili kumakinisha utumwa na kuboresha mashari ya utumwa katika hali bora zaidi! Hay'at Tahrir of Al-Sham Ukombozi, ambayo inadhibiti eneo la Idlib ilikataa isipokuwa kufichua ukweli wa dori yake iliyopangiwa; Na kwamba haikuwa isipokuwa ni chombo tu cha kutekeleza uhalifu huu baada ya kutekeleza masharti ya Mkataba wa Sochi na kuchukua ulinzi wa doria za Urusi kwenye barabara ya M4, ambapo ilifanya msururu ukamataji wa mashababu wa Hizb ut-Tahrir; Wakati ilipokuwa ikiendesha kampeni hiyo, mashababu wake watano walikamatwa huko Idlib. Ikafuata kukamatwa kwa wawili katika mji wa Binish; kisha wawili wakakamatwa katika mji wa Atma; na akawafuata mwingine mmoja baada ya maandamano ya wanawake kufanyika katika mji wa Atma kutaka kuachiliwa huru kwa wale wote waliokamatwa bila ya haki na kundi hilo, jumla ya wale waliokamatwa na Hay'at Tahrir al-Sham kuhusiana na kampeni hiyo; ni mashababu kumi, ambao wengi wao bado wamewekwa kizuizini hadi kufikia wakati wa kuandika taarifa hii.

Vyombo vingi vya habari viliangazia kampeni hii; ima vile vyenye kuegemea upande wa dhalimu wa Ash-Sham; ama vyenye kuegemea upande wa upinzani. Viliangazia mno habari hii kwa njia ya upotoshaji mwingi kila mmoja kwa mujibu wa mwelekeo wake; na kwa umbo ambalo linatumikia sera zake, bila ya kuzingatia usahihi na malengo ya uwasilishaji; au ukweli kuchunguzwa bila ya ubaguzi na bila ya mapendeleo, kuliangali jambo kama mapambano kati ya makundi mawili juu ya maeneo ya ushawishi; Bila kusahau kukidharau chama hiki wakati mmoja; kukinasibisha na msimamo mkali na ugaidi wakati mwingine; Na kukituhumu kwa kujaribu kuunda kikundi chenye silaha viungani mwa Aleppo magharibi.

Kwa hivyo ilikuwa ni lazima kwetu na katika hali hii kuuelezea Ummah wa Kiislamu kwa jumla na hususan watu wa Ash-Sham yafuatayo:

Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa kilichoanzishwa mnamo 1953 M na Sheikh Taqiu al-Din al-Nabhani, Menyezi Mungu amrehemu, lengo lake ni kuanzisha tena maisha ya Kiislamu; ambayo yalisimama baada ya kuangushwa kwa dola ya Waislamu (Khilafah); Katika mikono ya mhalifu Mustafa Kemal mnamo 1924 M.

Hizb ut-Tahrir alichukua njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo kwayo alisimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina Al-Munawwara; iliichukua kama njia yake, kisha ikaanza da'wah ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara yake njema; Na imeenea katika nchi nyingi za ulimwengu wa Kiislamu na kwengineko, na miongoni mwazo ni ardhi ya Ash-Sham, ambayo ilishuhudia mapinduzi dhidi ya mmoja wa madhalimu wenye nguvu katika enzi ya kisasa, kwa hivyo Hizb ut-Tahrir alifanya kazi kuunga mkono kuangushwa kwa madhalimu; Na ilijaribu kwa bidii kurekebisha njia kuelekea mwelekeo sahihi ili kujitolea kwa watu wa Ash-Sham kusipotee bure kwenye vichochoro vya makongamano ya kimataifa, na njama za nchi ambazo zinachukia Uislamu na Waislamu. Na ilikuwa mshauri mwaminifu na kiongozi ambaye hakuwadanganya na kamwe hatawadanganya watu wake, kwa hivyo alionya dhidi ya makongamano ya Geneva, Astana na Sochi, kama vile alionya juu ya pesa chafu za kisiasa matokeo yake yapo mpaka sasa, na alionya juu ya mapatano, mazungumzo na maeneo ya kuzuia ongezeka la mapambano, ambayo yalikuwa moja ya sababu za kupungua kwa kasi kwa Mapinduzi ya Ash-Sham, na pia ilionya juu ya dori ovu inayochezwa na serikali ya Uturuki, na Hizb sasa inaonya juu ya uhalifu wa suluhisho la kisiasa la Kiamerika ambalo litayaangusha mapinduzi ya Ash-Sham na kuhifadhi kuendelea kubakia kwa dhalimu wake.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Ua wa Nyumba ya Uislamu:

Kila mfuasi wa haki anajua; Kwamba yale yote ambayo Hizb ut-Tahrir ilionya juu yake tayari yametokea; Na kwamba ukosefu wa sikio lenye kusikia ndio sababu ya kile Mapinduzi ya Ash-Sham yamekifikia, kwani kila mwangalizi wa haki anajua kuwa mapambano ya Hizb ut-Tahrir hayako na vikundi vyenye silaha wala na watoto wengine wa Kiislamu. Badala yake, mapambano yake ni kwa Magharibi kafiri na vibaraka wake miongoni mwa watawala wa Waislamu, na ni mapambano yasiyopingika, wala hayana kujipendekeza ndani yake wala kubembeleza, ambapo imepelekea wabebaji ulinganizi kukamatwa, kuuawa na kushtakiwa katika magereza ya madhalimu, kiongozi wao akiwa ni dhalimu wa Ash-Sham, baba na mwana. Haya yanaandamana na kampeni za vyombo vya habari za kashfa, uzushi, kejeli na dharau, ambazo zote ni njia zinazotumiwa dhidi ya mitume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ، إِنَّ هَؤُلَاءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ، وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ، وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ)

“Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo * (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo * Nao wanatuudhi * Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.” [TMQ 26:53-56].

Hizb ut-Tahrir inatekeleza mapambano yake ya kisiasa dhidi ya Magharibi kafiri, ili kufunua na kufichua njama zote, na vile vile mvutano wake wa kifikra dhidi ya fikra na fahamu za kikafiri peke yake, na inatafuta nusra kutoka kwa watu wenye nguvu; yote haya, ni kwa kufuata njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na kuziweka hukmu za Uislamu katika upande wa utekelezaji. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(قُلْ هَذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ)

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.” [TMQ 12:108].

Na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu itabakia ameshikamana na fikra yake; imara katika njia yake; Yenye kufanya kazi pamoja na kwa ajili ya Ummah wake, mpaka Mwenyezi Mungu (swt) atukirimu sote kwa nusra ya dini yake, na kutimiza ahadi yake, na kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pindi aliposema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“kisha itakuwepo a Khilafah kwa njia ya Utume.”

 Ahmad Abdul Wahab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu