Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  3 Jumada I 1444 Na: HTS 1444 / 14
M.  Jumapili, 27 Novemba 2022

 Hotuba ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Uliofanywa na Hizb katika Taasisi ya Taiba ya Vyombo vya Habari

yenye kichwa: “Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba inayosuluhisha Migogoro, yenye Kuleta Makundi yote pamoja, na Kuwauidhi Maadui”

 (Imetafsiriwa)

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Na rehma na amani zimshukie mjumbe aliyetumilizwa kama rehma kwa walimwengu, bwana wetu na kipenzi chetu Muhammad (saw), kiongozi wa Njia Iliyo Nyooka, na ahli zake watukufu na maswahaba zake, na anayefuata njia yake na akafuata nyayo zake mpaka Siku ya Kiyama.

Waheshimiwa mliohudhuria, Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Nikiregelea yale yanayoendelea katika ulingo wa kisiasa nchini Sudan, katika suala la majaribio ya kutatua mgogoro wa utawala; mgogoro huu wa muda mrefu ambao umeihafifisha nchi yetu kwa miongo kadhaa, huku ikiteseka chini ya minyororo yake, wakati nguvu za kisiasa zikibakia, katika miongo yote hii, mateka wa yale ambayo wakoloni walipanga kuhusiana na mifumo ya serikali, siasa, uchumi na mengineyo.

Leo, waheshimiwa mliohudhuria, wafuatiliaji na watazamaji, tunasimama pamoja nanyi mbele ya kesi ya kipekee ya fikra zenye maadili nje ya sanduku la uhalisia wa kuhuzunisha katika kuchunguza tatizo kwa kina, na kutafuta masuluhisho ya kimsingi ya mgogoro wa utawala na utupu wa katiba ambao nchi yetu inaupitia.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, tunawasilisha kwa kila mtu anayehusika na maslahi ya nchi na watu, rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah yenye ibara 191, ambayo ina hukmu jumla, mfumo wa serikali, mfumo wa kiuchumi, mfumo wa kijamii, sera ya elimu, na sera ya kigeni, kupitia muundo jumla na maelezo yafuatayo:

Kwanza: Kama Waislamu, msingi wa rasimu ya katiba, ambayo ndiyo sheria msingi ya dola, lazima ujikite kwenye imani ya Umma; aqida tukufu ya Uislamu.

Hivyo basi, kifungu cha kwanza cha rasimu ya katiba ya dola ya Khilafah kinasema kwamba “imani ya Kiislamu ndio msingi wa dola, hivyo hakuna kitakachoweza kuwepo katika umbile lake, chombo chake, uwajibikaji au kila kitu kinachohusiana nayo, isipokuwa kwa kuifanya imani ya Kiislamu msingi wake.”

Pili: Vifungu vya katiba hii vinatokana na ijtihad sahihi kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake (saw), na yale waliyoyaongoza kwa mujibu wa makubaliano (Ijma) ya maswahaba, na kipimo cha Sharia, yaani, ni hukmu za Sharia, na sio maoni ya mwanadamu, kama ilivyo katika katiba zinazopendekezwa zote bila tofauti.

Tatu: Rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah inatatua mzozo unaoendelea kwa hukmu za Wahyi Mtukufu, kama:

A) Mamlaka ni ya Ummah, kwani humchagua mtu ndani yake ambaye anakamilisha masharti ya mkataba wa Khilafah, na kuweka kiapo cha utiifu kwake kama Khalifa kwa Waislamu, na Amir wa waumini waliomo ambaye kwaye sheria ongofu ya Mwenyezi Mungu inatekelezwa miongoni mwao.

B) Waislamu wana haki ya kuanzisha vyama vya kisiasa ili kuwawajibisha watawala, au kupata madaraka kupitia Ummah, kwa sharti kwamba msingi wao uwe ni aqida ya Kiislamu. Vyama hivi ndivyo vinavyomhisabu mtawala kwa msingi wa Uislamu iwapo atapotoka kwenye njia au kushindwa kusimamia mambo. Haki ya kuhisabu haiko kwa vyama vya kisiasa pekee, bali kwa raia vilevile. Hivi ndivyo Uislamu unavyomdhamini kila mtu.

C) Kazi ya jeshi ni kufanya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kulinda yai la Uislamu na mipaka ya Waislamu, na halina uhusiano wowote na utawala kwani ni jeshi lenye silaha. Bali, ni haki yake kutoa kiapo cha utiifu kwa Khalifa wa Waislamu, kwa kuzingatia wanachama wake kama raia wa dola. Idara ya Kijeshi hushughulikia mambo yote yanayohusiana na nguvu za kisilaha, ikiwemo jeshi, polisi, vifaa, misheni, na kadhalika. Idara hii ni sehemu ya dola, na kiongozi wake anaitwa Amir wa Jihad. Jeshi la Waislamu ni jeshi moja, haijalishi lina vitengo vingapi, na liko chini ya uongozi wa Khalifah.

Nne: Rasimu ya katiba ya Khilafah inazileta pande zote pamoja kwa vipengee vifuatavyo:

A- Haitaruhusu ushawishi wowote wa makafiri wakoloni katika nchi yetu, kama ilivyo leo, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ametukataza kuwapa makafiri mamlaka juu ya Waislamu, na Mola Mtukufu akasema:

(وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً)  

wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa 4:141]. Na akasema:

(لَا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ)  

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao [Aali’Imran 3:28].

B- Sera ya mambo ya nje katika dola ya Kiislamu imejikita katika kubeba Dawa’a ya Kiislamu, na nchi huamiliwa ipasavyo. Kwa hivyo, nchi za kihakika za kikoloni kama vile Amerika, Uingereza na Ufaransa, na nchi zenye ulafi katika nchi yetu, kama vile Urusi, kihukmu zinachukuliwa kuwa ni nchi za kivita, kwa hivyo tahadhari zote lazima zichukuliwe juu yao, na hairuhusiwi kuanzisha uhusiano wowote wa kidiplomasia nazo. Pia hairuhusiwi kwa mtu binafsi, chama, kambi, au kikundi chochote kuwa na uhusiano na nchi yoyote ya kigeni hata kidogo, uhusiano na nchi ni umefungwa kwa dola pekee.

Tano: Kuregeshwa kwa maisha kamili ya Kiislamu, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo rasimu yake ya katiba inaweka mwamko wa kweli kwa msingi wa Uislamu, inawaudhi maadui, kwa sababu inachukua hatua na kuuongoza ulimwengu kutoka kwao kama ilivyokuwa wakati Umma wa Kiislamu ulipokuwa na Khilafah kwa msingi wa hukmu za Uislamu, hivyo uliikomboa dunia kutoka katika ukandamizaji wa dini batili, na kuwazunguka kwa uadilifu na rehema ya Uislamu, na kuwatoa walimwengu kutoka katika dhiki ya dunia hii hadi kwenye upana wa dunia na akhera, hivyo Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu urudi kama alivyotaka Mola wetu Mtukufu. Mwenyezi Mungu asema:

(كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ)

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Ali’Imran 3:110]

Kwa kumalizia: Tunawasilisha rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah kwa Ummah mzima, kwa viongozi na waheshimiwa wa Ummah, wanasiasa, na wanafikra, waisome, watabanni fikra zake, na waitabikishe kivitendo, ili Mwenyezi Mungu atubariki kwa rehema na baraka zake. Na kutoka kwa askari ambao ni watiifu kwa imani yao na Ummah, Hizb ut Tahrir inaomba ikabidhiwe mamlaka ili kuiweka katiba hii na mfumo mzima wa sheria na kanuni ambazo hizb imeitabanni kutoka kwa Uislamu mtukufu, katika utabikishaji wa kivitendo.

(هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ)

Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.” [Ibrahim: 14:52]

Wassalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu