Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 24 Jumada II 1446 | Na: BN/S 1446 / 18 |
M. Alhamisi, 26 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamlaka ya Palestina Yafuata Mbinu za Mashetani Kuhalalisha Uhalifu wake katika Kambi ya Jenin!
(Imetafsiriwa)
Mamlaka ya Palestina (PA) ilikusanya vyombo vyake vya habari na vipaza sauti vya wasemaji na nzi wa kielektroniki (wanyanyasaji wa mtandaoni wanaounga mkono serikali) ili kuchafulia jina kambi ya Jenin na watu wake na kuhalalisha umwagaji wa damu yao. Kisha, ilikusanya vyombo vyake na majambazi katika mji wa Khalil al-Rahman, na wachache wa wale walioitwa watu mashuhuri waliojiuza kwa PA kwa manufaa maovu, na wale ambao iliwatishia kutoka kwa wafanyikazi na walimu. Ilitumia wizara, shule zilizofungwa, na kukodi mabasi ili Jimbo la Khalil al-Rahman, mji na wilaya, ionekane kuwa pamoja nayo katika kumwaga damu ya watu wa kambi ya Jenin. Hii ijapokuwa inajua na wale walio nyuma ya kwamba Khalil al-Rahman, pamoja na watu wake na koo zake, hawawezi kukubali kwamba itoa nusu ya neno kumwaga tone la damu ya Waislamu. Kwa kitendo hiki kiovu, inataka kuleta mgawanyiko kati ya watu wa Palestina (kaskazini na kusini) chini ya pazia la uongo la uhalifu wake.
Mamlaka hii ya kihuni iliongeza jinai nyingine katika safu yake ya jinai, ili kunyamazisha sauti ya watu wa Palestina wanaokataa jinai zake. Ilikamata idadi ya wanachama kutoka Hizb ut Tahrir wiki hii, kutoka miji tofauti ikiwemo Qalqilya, Salfit, Tulkarm, Ramallah na al-Khalil, sawa na wale iliowakamata kutoka kwa watu wa Palestina. Iliwashambulia baadhi yao kwa kuwapiga, na haikuheshimu utukufu wa nyumba, wala haikuhifadhi heshima ya watu, wala haikuzuiwa na hadhi ya sheikh mtukufu au tabia ya kijana mtukufu. Bali ilienda mbali sana katika utovu wa adabu na kuvunja utu wa watu wa Palestina, hivyo ikaanza kuwarekodi baadhi ya watu iliowakamata huku wakiomba radhi kwa vyombo vya usalama kwa kutumia silaha na tishio la kuteswa, hivyo kuvunja miko yote ya damu, heshima na fedha za watu wa Palestina. Bali, ilizikanyaga sheria zao chini ya viatu vyake vilivyokiuka kambi ya Jenin kwa kisingizio cha kupigana na wale walioharamishwa!
[أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ]
“Tazama uovu wa wanavyohukumu!” [An-Nahl: 59]
Jinai za kuwakamata, kuwapiga na kuwatesa watu wa Palestina, wakiwemo wanachama wa Hizb ut Tahrir, zinatarajiwa kutoka kwa mamlaka ambayo inatekeleza mambo ya kinyama zaidi kuliko haya katika kambi ya Jenin. Yeyote atakayesubutu kuchoma nyumba, kunyima chakula na kuzingira watu, na kutumia silaha ya RPG - ambayo umbile la Kiyahudi halikuwaruhusu kuimiliki na kuitumia isipokuwa dhidi ya watu wa Palestina - kisha waue vijana na wavulana, na washambuliaji wao wawazuie watu kuwafikia wale waliowaua, kama jeshi la Kiyahudi linavyofanya mjini Gaza, yeyote atakayesubutu kufanya jinai zote hizi hatopata madhara katika kuwakamata watu wa Palestina, kuwatesa na kukiuka haki zao.
Mamlaka ya Palestina, kutokana na ukamataji huu, inataka tu kunyamazisha kila sauti inayokataa uhalifu wake, au tuseme jinai zake, na kuonyesha kwamba watu wa Palestina wanakubaliana na yale ambayo mikono yake imeyafanya, yaliyotiwa doa la uhaini na umwagaji damu, utiifu kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na wale walioinyakua ardhi iliyobarikiwa.
Uongo mbaya zaidi ni kwa Mamlaka ya Palestina kusema kwamba inaruhusu damu ya watu wa kambi ya Jenin kumwagika ili isiharibiwe kama Gaza. Hili linaibua msururu wa maswali ambayo hayamkanganyi mwenye akili:
Je! Mamlaka ya Palestina inawazingira watu wa Jenin, inabomoa nyumba zao, inawaua kwa njaa wanawake na watoto wao, na inawatumia wauaji wake kuwaua ili Mayahudi wasiwaue?!
Je, Mamlaka ya Palestina inataka kuwapokonya silaha na kuwanyang'anya silaha zao ili kuwalinda dhidi ya mnyakuzi na walowezi wake, na kisha kuwalinda watu wa Palestina?!
Je, uchokozi wa Gaza na uharibifu wake hauambatani na simulizi ya mhalifu, umbile nyakuzi la Kiyahudi ambalo linahalalisha uhalifu wake huko Gaza kwa njia ile ile ambayo Mamlaka ya Palestina inahalalisha uhalifu wake huko Jenin?!
Je, mujahidina wa Gaza ndio wa kulaumiwa, au ni mamlaka ya Palestina kulaumiwa, ambayo rais wake alishutumu operesheni ya Oktoba 7, 2023?!
Au tawala na nchi ndizo za kulaumiwa kwa kuwaangusha watu wa Gaza na mujahidina wake, na hata kuwasaidia Mayahudi dhidi yao, na kuwapa kila walichoweza kuwaua?!
Au ni majeshi ya kulaumiwa kwa kuwaacha watu wa Gaza kati ya uvamizi wa Mayahudi, usaliti wa watawala, na njama za Mamlaka ya Palestina, na kutosonga kwenda kuwanusuru, na kuikomboa ardhi ya Uislamu, ardhi ya Israa na Miraj?!
Je, Mamlaka ya Palestina inawalaumu watu wa Algeria kwa sababu walitoa mashahidi zaidi ya milioni moja dhidi ya mkoloni kafiri wa Kifaransa, au inamtia hatiani Omar Mukhtar, nembo ya Jihad katika Maghrib ya Kiarabu?
Kabla ya hili, Mamlaka ya Palestina inapaswa kutwambia: Je, inamlaumu nani kwa uharibifu wa Lebanon katika miaka ya 1980? Je, inalaumu asili yake (PLO) na kuwaondolea Mayahudi hatia ya uhalifu na mauaji yao huko?! Je, Mamlaka ya Palestina haioni kwamba Mayahudi na walowezi wao wanakula Ukingo wa Magharibi, bila kuacha ardhi pasi na kuigusa, bila kuacha nyumba pasi na kuibomoa, na bila kuacha mti pasi na kuuchoma moto? Vipi itapata ridhaa ya Mayahudi ambao Mwenyezi Mungu (swt) amesema kuhusu wao:
[أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِنَ الْمُلْكِ فَإِذاً لَا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيراً]
“Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.” [An-Nisa: 53]. Au je, ni kwamba nchi na watu wake waliuzwa kwa msingi wa dhana ya ahadi ya Shetani?
[يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُوراً]
“Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu.” [An-Nisa: 120] Hii ndiyo hali ya walio khasirika duniani na Akhera. Bila shaka hii ndiyo hasara iliyo dhahiri.
Tunawaambia wajumbe wa Vyombo vya Usalama: Mayahudi hawataishi katika Ardhi hii Iliyobarikiwa, wakati Mwenyezi Mungu (swt) ametuahidi, akisema:
[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]
“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra: 7]
Na Mtume wake (saw) ametuahidi vita vya ukombozi. Hakuna dhalimu atakayeishi muda mrefu katika nchi hii, sio Mayahudi wala wenye Mamlaka hawatabaki humo. Hii ni ahadi ambayo si ya uongo. Je, hamuoni kwamba wahalifu wakubwa walikimbia na kuwaacha wafuasi kukutana na hatima yao? Ni kwa manufaa ya nani mnamfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini? Munawaua ndugu zenu kwa manufaa ya nani? Je, ni kwa manufaa ya nani munakuwa chombo mikononi mwa maadui zenu? Mtajiokoaje kesho na yule mliyemuua mwanawe, au kumpiga baba yake, au kumkamata nduguye? Je, hakuna funzo kwenu katika utawala wa Bashar?! Vile vile tunakukumbusheni kuwa dhulma ni giza Siku ya Kiyama, basi itakuwaje ikiwa dhulma ni kumwaga damu iliyoharamishwa, ambayo kuvunjwa kwa Ka’aba kwa Mwenyezi Mungu ni dhulma ndogo kuliko hiyo?! Na vipi ikiwa jinai hiyo ni kuisaliti ardhi ya Israa na Mi'raj na watu wake?
Tunarudia hili kwenu, acheni kutumia silaha zenu na nguvu zenu dhidi ya Palestina na watu wake, hilo ni bora kwenu hapa duniani na kesho Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) asema
[إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ * يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَى وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ]
“Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu * Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!” [Al-Qamar: 47-48]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: |