Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  11 Rabi' I 1445 Na: BN/S 1445 / 02
M.  Jumanne, 26 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Masrah ya Mtume Mtukufu Muhammad (saw) Inawatazamia Wakombozi, Sio Wasaliti Watiifu
(Imetafsiriwa)

Chini ya kivuli cha uvamizi, ujumbe rasmi wa Saudia, ukiongozwa na Balozi Naif bin Bandar al-Sudairi, mjumbe wa ajabu, amewasili mjini Ramallah leo kuwasilisha nyaraka zake rasmi kwa Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas. Balozi huyo aliingia kupitia Daraja la Mfalme Hussein hadi Jericho na kisha akaelekea pamoja na ujumbe wake ulioandamana naye hadi makao makuu ya Jimbo huko Ramallah kukutana na Abbas.

Baada ya kuingia katika maeneo ya Palestina, balozi huyo aliandika tweet kwenye akaunti yake kwenye jukwaa la X, akisema, "Kutoka kwa Dola kipenzi ya Palestina, ardhi ya Kanaani, salamu za dhati, zikifuatana na mapenzi ya bwana wangu, Msimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu, na Mtukufu Mfalme Mtarajiwa."

Ziara hii ya Al-Sadairy inajiri katika muktadha wa mazungumzo yanayoendelea yakiongozwa na Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman na umbile la Kiyahudi, chini ya usimamizi wa Marekani, ili kuhalalisha mahusiano. Uhalalishaji huu wa mahusiano ulitangazwa na Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman katika mahojiano na Fox News. Ziara hii inasisitiza kiwango ambacho watawala hawa wameshuka ndani ya ushirikiano wa kina, hawaoni tena tatizo lolote na uhalalishaji wa wazi wa mahusiano na wale ambao wanaoikalia kimabavu Masrah ya Mtume Muhammad (saw) na wale wanaoua watu wa Palestina mchana na usiku, na wale ambao waloezi wao sasa wanaivamia Al-Aqsa na kuinajisi kila siku! Je! Hivi ndivyo mnavyouhami ushindi wa Al-Masjid Al-Haram na Masrah ya Mtume (saw)? Je! Vikosi vyenu vimeshindwa kulishambulia umbile la Kiyahudi kwa hata robo au humusi au ya ushuri ya mabomu mliyotumia kuiunguza Yemen, ili kuliondoa na kuisafisha Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na uchafu wake? Au je! Nyinyi ni vikaragosi tu vilivyotumiwa na mabwana zenu katika ikulu ya White House vile wanavyotaka na wakati wanapotaka?

Utawala wa Saudia hauna nia ya kupigana na Mayahudi au kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Masrah ya Mtume Muhammad (saw) na ardhi ambayo mchanga wake ulinyeshwa kwa damu ya Maswahaba, sio ardhi ya Kanaani kama ilivyoelezewa na al-Sudairi). Kwa kweli, serikali ya Saudia imekuwa ikifanya mahusiano kwa muda sasa na umbile la Kiyahudi, bali kwa siri. Kwa hivyo, Saudi Arabia haipingi kimsingi kuanzisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Kwa kweli, mfalme wake wa zamani, Abdullah bin Abdulaziz, alizindua Mpango wa Usaliti wa Kiarabu mnamo 2002, na Saudi Arabia mara kwa mara inathibitisha kujitolea kwake kwao.

Watawala katika nchi za Waislamu wanaonekana wamesahau kuwa Palestina ni nchi iliyobarikiwa, kama vilivyo viunga vyake, kama ilivyoelezwa katika Quran:

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Isra:1].

Ni jukumu la majeshi ya Waislamu kusonga na kuikomboa, kuitakasa kutokana na uchafu wa Mayahudi, badala ya kuipa Palestina kwa Mayahudi kwenye sahani ya fedha ya uhalalisha mahusiano, usalimishaji, na utiifu!

Palestina hakika itarudi safi na yenye baraka, kama ilivyokuwa kwa panga za majeshi yenye ikhlasi ya Waislamu yakiongozwa na Khilafah Rashida. Wataushinda mkusanyiko wa Mayahudi na washirika wao, na wataigeuza migongo yao kwa kukimbia. Hofu itajaza nyoyo zao kufikia hadi mahali ambapo mmoja wao atajificha nyuma ya jiwe, ambalo litaita, kama Mtume Muhammad (saw) alivyotoa bishara njema:«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ‏» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawauwa mpaka jiwe litasema: Ewe Muislamu huyu hapa Yahudi (amejificha nyuma yangu); basi njoo umuuwe.” Katika riwaya nyengine: «هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي» “Kuna Yahudi nyuma yangu.”

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيبًا]

“Na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51]. Na pengine hili litatokea hivi karibuni Bi idhnillah. Wakati huo, wale wanaojihusisha na uhalalishaji mahusiano na Mayahudi hawatakabiliwa na chochote isipokuwa aibu na adhabu kali.

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An'am: 124].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu