Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 24 Dhu al-Hijjah 1441 | Na: 1441/14 |
M. Ijumaa, 14 Agosti 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ardhi Iliyo Barikiwa Iko katika Miadi ya Kukombolewa
Usawazishaji Mahusiano wa Imarati ni Ukurasa Mweusi Ulioongezwa katika Kurasa za Watawala Makhaini!!
(Imetafsiriwa)
Imarati na umbile la Kiyahudi zimekubaliana kuasisi mahusiano kamili ya kidiplomasia baina yao, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyo tolewa na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Benjamin Netanyahu, Mfalme Mtarajiwa wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed Al Nahyan na Raisi wa Amerika Donald Trump. Bin Zayed alisema kwa mawasiliano na Trump na Netanyahu, kuwa ramani ya barabara ya ushirikiano wa pamoja iliafikiwa, ili kuasisi mahusiano baina ya pande mbili yaliyoafikiwa, na chini ya makubaliano hayo, nchi hizi mbili zitabadilishana mabalozi na kushirikiana katika nyanja tofauti tofauti, ikiwemo usalama, elimu na afya. Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi aliyasifu makubaliano hayo kuwa ya kihistoria, na kusema kwamba Imarati itawekeza viwango vikubwa ndani ya umbile la Kiyahudi, na kusisitiza kwamba makubaliano hayo hayafuti mpango wa uunganishaji, na kwamba amejitolea kuyatabikisha kwa kushirikiana na utawala wa Amerika pekee, na sera ya umbile lake kuhusu Ukingo wa Magharibi haitabadilika.
Makubaliano haya mapya ya khiyana yanakuja kudhihirisha hali ya watawala ambao wamezitawala shingo za Ummah wa Kiislamu, kwa watawala wa Imarati, kama watawala wengine wa Waislamu, ni vyombo duni tu mikononi mwa maadui wa Ummah wa Kiislamu, wanaotabikisha maagizo yao pasi na kusita au aibu. Kupitia maongezi ya simu, watawala hawa wa Imarati wanaingia rasmi katika kilabu cha wasawazishaji hadharani mahusiano na umbile la Kiyahudi, bila ya aibu yoyote wanajiunga na kundi la wanaotambua uhalali wa uwepo wa umbile la Kiyahudi juu ya sehemu kubwa ya Ardhi Iliyo Barikiwa, na kusawazisha mahusiano nalo licha ya udhalimu na kiburi chake chote, kana kwamba umbile hili la Kiyahudi halikikalii kibla cha kwanza katika vibla viwili na Msikiti wa tatu Mtukufu baada ya Misikiti Miwili Mitukufu, na eneo alilopaa Mtume (saw) kwenda mbinguni (Masra)!
Watawala wadhalilifu wa Imarati hawakuweza kuzisitiri nyuso zao hata kwa masaa, huku mshirika wao mpya, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, akitangaza kuwa amejitolea katika swala la uunganishaji na kwamba hataachana nalo na kwamba lingalipo katika ajenda ya serikali yake. Na kwa tangazo hili umbile la Kiyahudi kwa haraka linaangusha kisingizio duni cha watawala wa Imarati, ambacho kiliwakilishwa kwa msemo wa usawazishaji mahusiano kwa badali ya kuondolewa kwa uunganishaji na kupanuliwa kwa ubwana juu ya Ukingo wa Magharibi! Hii ndio hatma ya kila haini wa dini yake. Fedheha hapa duniani na adhabu ya kesho Akhera ni kali zaidi na yenye kudhalilisha.
Watawala wa Waislamu ni gora moja katika khiyana; wale ambao wanasawazisha na kuasisi mahusiano hadharani, na wale wanaotoa wito wa suluhisho la dola mbili, uhalali wa kimataifa na maamuzi ya kimataifa kama msingi wa kutatua kadhia ya Ardhi Iliyo Barikiwa. Suluhisho la dola mbili linalopigiwa debe na watawala na Mamlaka ya Palestina, au Mradi wa khiyana wa Waarabu au maamuzi ya kimataifa yote yanapeleka katika natija moja ya khiyana, kuipoteza na kuisalimisha sehemu kubwa ya Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina kwa badali ya kijidola dhaifu ambacho kazi yake ni kulinda uwepo wa Mayahudi na kuwahangaisha watu wa Palestina na kuwazuia uhuru wa kutembea au kuwaoanisha kithaqafa ili wasiwe ni kikwazo kwa umbile la Kiyahudi na mustakbali wake wa kuishi salama ndani ya Ardhi Iliyo Barikiwa, kama lengo la masuluhisho yote ya kikoloni.
Wapatanishi waliokubali uhalifu huu au wale wanaojidai kuupinga kupitia vyombo vya habari na kuusifu kuwa uhaini, wote wanakubali uhaini, wanakubali kutambua uhalali wa umbile la Kiyahudi, na kushirikiana na kuwasiliana nalo wakati mmoja kisirisiri, na wakati mwengine kidhahiri. Mradi wa Kiarabu umependekeza usawazishaji kamili wa mahusiano hadharani kwa badali ya kijidola dhaifu katika baadhi tu ya Palestina, na upinzani wao ni sawa na upinzani wa Sadat, aliyetia saini Makubaliano ya Camp David, kwa kuyasifu makubaliano wakati huo kama khiyana, kisha punde baadaye amani ya muda mfupi na mvamizi katika mipaka ya 1967 ikawa ndio matakwa ya Mamlaka ya Palestina na watawala, na kazi ya kupata hili ikawa ni mapambano na mshikamano wa kudumu! Hivyo wao wamekuwa makhaini zaidi kushinda Sadat!
Watawala wa Imarati, kama walivyo watawala wote wa Waislamu, wanajiwakilisha wao wenyewe pekee kwa kuziuza nafsi zao kwa shetani kupitia uwakala wao kwa wakoloni wa Kimagharibi, na Ummah umejitenga nao. Ummah unaoishi kwa Qur'an na Surah al-Israa unaona ukombozi wa Palestina kama suluhisho la kadhia ya Ardhi Iliyo Barikiwa, suluhisho halali ambalo ililiona eneo la Hattin wakati shujaa Salah al-Din alipowafagia Makruseda, na utaliona tena uhalisia wake wakati majeshi ya Ummah yatakapoinuka na kunguruma tena kunyanyua bendera ya Uislamu juu ya kuta za Jerusalem na majumba ya Ardhi Iliyo Barikiwa, na kuling'oa umbile la Kiyahudi milele.
Kadhia ya Ardhi Iliyo Barikiwa ni kadhia ya taifa tukufu la zamani ambalo liliibuka na ushindi katika vita vikuu juu ya ardhi, likiwashinda Makruseda eneo la Hattin na kuwavunja vunja Mongoli eneo la Ain Jalut, na litainuka tena na ushindi na kuichukua tena Ardhi Iliyo Barikiwa na nchi yote, na Ardhi Iliyo Barikiwa haitabakia kuwa kadi ya kura mikononi mwa Trump au yeyote mwengine ambayo kwayo anajipatia mafanikio duni ya kisiasa, kupitia kuwaagiza watawala wa Imarati kuasisi mahusiano na umbile la Kiyahudi. Ni kadhia ya taifa linalo tafuta kurudisha mamlaka yake kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume hapo ndipo Trump na makundi yake atakaposahau minong'ono ya mashetani, na hivyo kung'oa ushawishi wake na wafuasi wake makhaini miongoni mwa watawala wa Waislamu na kuirudisha Ardhi Iliyo Barikiwa kuwa kifua cha Ummah wa Kiislamu.
Khiyana hizi za hadharani na pale ambapo kadhia ya Palestina imefikia inaweza tu kukomeshwa kupitia kusonga kwa majeshi ya Ummah wa Kiislamu na viongozi na maafisa wake kuikomboa Ardhi Iliyo Barikiwa na kuling'oa umbile la Kiyahudi na watawala makhaini wanaopanga njama dhidi ya Ummah huu na kadhia zake. Hakuna ukombozi kwa Masra hii na hakuna mwamko kwa Ummah huu chini ya watawala wanaotii maagizo ya maadui wa Ummah na kuyatabikisha kwa dhati na ikhlasi na kuyapigia debe kana kwamba wao ni wanachama wa kampeni ya uchaguzi ya Trump!
Ummah haupaswi kunyamaza, bali unahitajika kusonga mbele ili kumaliza zama hizi zisizo za kawaida katika maisha ya Waislamu na kuondoa ukungu ili jua la Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume lichomoze. Khilafah ambayo haitawaacha Trump na vibaraka wake miongoni mwa watawala kupita patupu.
[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً]
“Na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: |