Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  8 Jumada II 1445 Na: 1445 / 26
M.  Alhamisi, 21 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kulazimisha Demokrasia kupitia Mkono wa Chuma, na Siasa za Kitambulisho cha Kitaifa, Zimeifanya Baluchistan kuwa Wasiwasi wa Kibinadamu, Kisiasa na Usalama

(Imetafsiriwa)

Mkasa wa kifo wa hivi karibuni wa Balaach Mola Bakhsh, kijana wa Kibaluchi kutoka Turbat, katika mapambano ya kisilaha, yaliyowekwa na Idara ya Kupambana na Ugaidi, umesababisha hasira kubwa, na kilio cha umoja kote nchini. Familia ya mwathiriwa, pamoja na wengine wengi, wameanzisha kikao cha amani, kikiongezeka hadi kuwa maandamano makubwa ya muda mrefu kuelekea Islamabad, katika kulaani vikali. Tukio hili linaloumiza moyo sio kesi ya pekee. Badala yake, ni dhihirisho baya la maswala ya kina ya kimfumo, ndani ya muundo wa sasa wa dola ya kitaifa, unaotekelezwa na serikali ya shirikisho.

Mfumo huu ambao ulikusudia kumfungamanisha vitambulisho tofauti vya rangi, lugha, na vitambulisho vya kieneo, umefeli vibaya. Vitambulisho vya kitaifa vinawafungamanisha watu pamoja juu ya vitambulisho vya rangi, kanda, lugha au kabila. Hili linaunda vitambulisho vingi ndani ya mipaka ya nchi moja. Linaifanya jamii kugawanyika katika misingi mingi ya makosa. Serikali ya kitaifa, na mfumo wa shirikisho, inajaribu kuviunganisha vikundi hivi vyenye vitambulisho tofauti chini ya mamlaka moja ya shirikisho. Kiasili, ni jukumu lake kuhakikisha haki, upatikanaji wa rasilimali, uhuru wa mikoa, na ulinzi wa kitambulisho cha ndani au kikanda.

Walakini, kivitendo, mfumo kama huu unaendelea kung’ang’ana na usambazaji wa rasilimali, uhuru wa mikoa, kulinda haki, na ulinzi wa kitambulisho. Kung’ang’ana huku kwa kuendelea hatimaye hupelekea kubeba hisia mbaya kwa vikundi vingi, ndani ya umbo la shirikisho, ambayo ndiyo yanayofanyika kwa sasa huko Baluchistan. Kifo cha kutisha cha Balaach Mola Bakhsh, na kutoeshwa kwa nguvu kwa wanaume wengi wa Baluch, kwa kweli ni matumizi ya mkono wa chuma ili kudumisha mamlaka ya serikali, na kusimamia matatizo yanayosababishwa na mfumo wenyewe dhalimu wa shirikisho.

Dola ya Pakistan inajaribu kuunda umoja wa kitaifa kupitia nguvu ya kikatili ili kuficha kufeli kwake. Inahusika na upoteaji wa maisha ya Waislamu wasio na hatia na mzozo unaokua kati ya serikali na makabila ya Baluch. Hii husababisha upoteaji wa damu ya Waislamu yenye thamani katika pande zote. Hii ni kudhoofisha nguvu na uwezo wa Waislamu, kutoa fursa kwa maadui kupanga njama dhidi yetu.

Kwa kuongezea, mfumo wa Kidemokrasia,huku ukijitahidi kuwakilisha walio wengi, umetelekeza sauti, na mahitaji, ya jamii za wachache. Ubaguzi huu unazidisha mgawanyiko. Unavisukuma vikundi vya wachache kuelekea mielekeo ya kujitenga, kutafuta kujitawala wenyewe, ambapo wao pia wanaweza kushikilia faida ya kiidadi. Harakati za kujitenga huko Baluchistan ni matokeo ya moja kwa moja ya mfumo wa kidemokrasia wa serikali.

Ni muhimu kutambua kwamba mshikamano wa kweli wa kijamii hauwezi kulazimishwa kupitia ukandamizaji. Wakati unaweza kutoa utiifu na usalimishaji wa muda mfupi, hauna sifa ya kukubalika na mwendelezo thabiti. Umoja wa jamii ni kupitia makubaliano ya jamii juu ya mtazamo wa maisha. Pia ni kupitia utabikishaji wa mfumo unaotokana na mtazamo huu juu ya jamii. Unatoa kitambulisho kimoja kwa jamii nzima ambayo huvuka rangi, lugha na kabila. Ili kudumisha umoja katika dola yoyote, inahitajika kuwa na jamii yenye umoja. Dola haipaswi kuzalisha jamii tofauti tofauti zilizojegwa juu ya vitambulisho tofauti. Hapo basi itajaribu bila kufanikiwa kuziweka jamii hizi pamoja, mithili ya mfumo sasa wa serikali ya shirikisho.

Suluhisho la kadhia ya Baluchistan liko katika muundo wa Dola ya Khilafah. Inatoa muundo wa mabadiliko kutoka kwa mitego ya mfumo wa sasa. Ndani ya Khilafah, fahamu za walio wengi na wachache hupoteza umuhimu katika maswala ya serikali. Ummah mzima unashiriki katika uchaguzi wa Khalifa.

Sheria ndani ya Khilafah inavuliwa kutokana na Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume. Sheria ndani ya Khilafah haiamriwi na ukuu wa walio wengi, au idadi kubwa ya wapiga kura. Njia hii ya Uislamu inalinda watu wa jamii zengine, lugha au mikoa kutokana na ushawishi usiofaa wa kabila, lugha au mkoa mwengine. Kwa kuongezea, mshikamano wa kweli wa kisiasa unaweza kupatikana tu kupitia utabikishaji wa mfumo wa kijamii na kiuchumi wa Uislamu. Uislamu hutumika kama nguvu isiyo na kifani ya kuunganisha, yenye kuvuka mipaka ya jamii, lugha, na mipaka ya eneo.

Enyi Maafisa Wanyoofu katika Jeshi la Pakistan!

Katika harakati za kutafuta umoja na uongofu, hebu na tujiepushe na maafa ya kupigana sisi kwa sisi, na kumwaga damu ya Waislamu, juu ya mistari batili ya kitaifa iliyochorwa na wakoloni. Huu ni wito wa kuungana na ndugu zetu jasiri wa Baluch, kusimama pamoja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Badala ya kuyatoa kafara maisha kwa sababu ya utaifa, hebu na tujitahidi kwa kusudi la juu na bora zaidi, kuuawa shahidi katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), huku tukipigana na majeshi ya uvamizi huko Palestina na Kashmir. Kumbukeni mafundisho ya Mtume wetu mpendwa Muhammad (saw) ambaye alisema,

»الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ ، وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ«

“Muislamu ni yule ambaye Waislamu husalimika kutokana na ulimi wake na mkono wake, na muhajir (mhamiaji) ni yule aliyeyahama yale aliyoharamishiwa na Mwenyezi Mungu.” [Bukhari]

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pia amesisitiza,

«لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا ولا تَبَاغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبِعْ بَعْضُكم على بَيْعِ بعضٍ، وكُونوا عبادَ الله إخوانًا، المسلمُ أخُو المسلمِ لا يَظْلِمُهُ ولا يَخْذُلُهُ ولا يَكذبه ولا يَحْقِرُه»

“Msihusudiane, wala msipandishiane bei, wala msichukiane, wala msipeane migongo, wala msidandiane biashara baina yenu, badala yake, kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu moja. Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu, wala hamtelekezi, wala hamdanganyi, wala hamdharau.” [Muslim]

Katika nyakati hizi ngumu, ambapo Ummah unakabiliwa na mizozo na ugomvi wa kindani, na vile vile uvamizi na ukandamizaji kutoka kwa vikosi vya nje, Nusrah yenu (msaada wa nyenzo) kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume inabeba thamani kubwa mno. Hiyo pekee ndiyo inayoweza kutuelekeza kuelekea umoja na uongofu wa kindani, na kuvisaga saga vikosi vya nje vya uvamizi. Mradi huu Mtukufu wa Khilafah unavuka mipaka na utaifa. Unalenga kuwaunganisha Waislamu, na kutokomeza fitna ya mapigano ya ndani kati yetu wenyewe. Khilafah itadhamini haki za Waislamu wa Baluch, na vikundi vyote. Italeta amani na ustawi kwa maeneo yote ya Waislamu, kupitia baraka ya Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu