Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  7 Rajab 1444 Na: 1444 / 23
M.  Jumapili, 29 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bila Dinari za Dhahabu na Dirham za Fedha za Uislamu, Sarafu Yetu Daima Itaporomoka Mbele ya Dolari. Utawala wa Dolari Unadumishwa na IMF, Mlinzi wa Mfumo wa Fedha wa Kimataifa wa Kimagharibi

(Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia masharti ya IMF, serikali ya Pakistan ilishusha ghafla thamani ya rupia kwa karibu rupia ishirini na tano, ambayo ni asilimia kumi ya thamani yake, na kusababisha dhoruba ya mfumko wa bei. Ongezeko kubwa la bei za umeme, mafuta na gesi linatarajiwa hivi karibuni, huku kukiwa na habari kwamba agizo la kutoza ushuru wa ziada wa bilioni 300 liko njiani. Ugumu huu wote wa kukandamiza ni utangulizi wa misheni inayotarajiwa ya IMF, kwa Uhakiki wake wa Tisa. Hatua hizi kali ni baada ya Waziri Mkuu, Shehbaz Sharif, kutangaza kujisalimisha kwa masharti yote ya IMF. Hivyo imethibitika kwamba chini ya mfumo wa kimataifa wa Magharibi, Pakistan kamwe haiwezi kusimama kwa miguu yake yenyewe, hata kama serikali elfu moja zitakuja na kuondoka!

Mfumo wa sasa wa kimataifa umeibiwa kwa ajili ya kuipendelea Magharibi. Unaipa Marekani na dolari yake faida isiyo ya haki juu ya mifumo ya kifedha ya nchi nyingine zote. Umeufanya udhalimu huu kuwa wa kitaasisi. Bila kuondolewa kwake, daima tutakuwa watumwa wa kupigwa wa mfumo huu wa Amerika. Mfumo huu unatunyang'anya ubwana wetu hatua kwa hatua. Unazitoa kafara hamu zetu nyeti, ambazo ni pamoja na Afghanistan, Kashmir na sera za ndani. Sasa inajumusisha kudhoofisha vikosi vya jeshi la Pakistan na kudhibiti mali ya nyuklia.

Khilafah ndiyo itakayomaliza ukiritimba wa dolari ya Marekani, kwa kutumia dinari ya dhahabu na dirham ya fedha, kwa biashara ya ndani pamoja na ya kimataifa. Sarafu thabiti ya Uislamu itamaliza mfumko wa bei uliokithiri na kuweka nidhamu ya kifedha. Kwa hivyo, yeyote anayeshirikiana na mfumo huu wa kimataifa kwa misingi ya usasa, au kuuza ndoto za uongo za mafanikio chini ya mfumo huu wa kikoloni, ni msaliti na kibaraka wa mfumo huu wa kimataifa, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Ni mfumo huu wa kimataifa wa Marekani ndio ulionyakua mito mitatu kutoka kwetu, ukaitenganisha Bangladesh, ukaisalimisha Kashmir baada ya Siachen, uliiruhusu India kujenga mabwawa kwenye mito yetu, ulituzuia kutekeleza Kulbhushan Yadav na kuhakikisha kuachiliwa huru kwa Abhinandan Varthaman. Unatulazimisha kulipa sehemu kubwa ya mapato ya ushuru kwa malipo ya riba. Benki ya Dunia ndiyo iliyoilazimisha Pakistan kukabidhi sekta ya uzalishaji umeme kwa sekta binafsi katika miaka ya tisiini. Hivi sasa, serikali haiwezi kumudu kuzalisha umeme wa kutosha, wala wananchi hawawezi kumudu ule unaopatikana. Ni dhahiri, hakuna wokovu kwa Pakistan chini ya mfumo huu wa kimataifa!

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Si China, Urusi, Ujerumani, Ufaransa wala Uingereza zitazouangamiza mfumo wa kimataifa wa Marekani. Zote ni washirika wa Amerika, wanaonufaika na mfumo wake. Mfumo wa sasa wa kimataifa ni lahaja ya hivi punde zaidi ya mfumo wa Magharibi, uliopangwa dhidi ya Uislamu na Waislamu. Mfumo huu utapinduliwa tu na askari wenye ikhlasi wa Dini hii, pindi watakaposimamisha tena Khilafah katika Ardhi za Kiislamu, hususan Pakistan. Khilafah ndiyo itakayounganisha Pakistan, Bangladesh, Afghanistan, Asia ya Kati na Mashariki ya Kati, na pia kwengineko, Afrika na Kusini Mashariki mwa Asia, kuwa dola yenye nguvu zaidi duniani. Ni Khilafah ndiyo itakayomaliza ukiritimba wa kifedha wa dolari ya Marekani kwa kutoa dinari ya dhahabu na dirham ya fedha, na kuwatengenezea njia walimwengu wote kuikataa dolari. Khilafah itauza mafuta na gesi kwa dhahabu na fedha pekee. Itakataa mikopo yote yenye riba. Itakuwa dola ambayo itakuwa na usalama wa chakula, usalama wa kawi na ulinzi imara. Khilafah itasimamisha ukuu wa Uislamu, na kuzika udhalimu wa mfumo wa kimataifa wa Marekani milele. Kwa hivyo, Enyi Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan, mnangoja nini? Toeni Nusrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah #TurudisheniKhilafah
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
أقيموا_الخلافة# كيف_تقام_الخلافة#
#YenidenHilafet #HakikiDeğişimHilafetle
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu