Jumamosi, 07 Rajab 1444 | 2023/01/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Jumada I 1444 Na: 1444 / 17
M.  Ijumaa, 25 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Takeni Kukomeshwa kwa Ushirikiano na Marekani, ili Kupata Fahari ya Majeshi Yetu, Ardhi Zetu na Dini Yetu

(Imetafsiriwa)

Uteuzi wa mkuu mpya wa jeshi kwa jeshi la Waislamu lenye nguvu zaidi duniani ulijiri wakati wa ukataji tamaa mkubwa. Tulishusha pumzi, tulipoona mwisho wa enzi chungu ya miaka sita ya Jenerali Bajwa. Kutufunga kwa ushirikiano na Marekani, Mafundisho ya Bajwa yaliharibu sifa ya wanajeshi, na kusababisha ukosefu wa utulivu na usalama juu yetu. Kuhusu njia ya kusonga mbele, hakuna yoyote zaidi ya kukomesha ushirikiano wote na Marekani, itakayoleta fahari ya majeshi yetu, huku tukipata kikamilifu uwezo mkubwa wa Pakistan.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Takeni kukomeshwa kwa ushirikiano na Marekani, ambao kwao Kashmir Iliyokaliwa kimabavu ilitelekezwa kwa India. Mafundisho ya Bajwa yaliondoa kabisa usaidizi wote wa Jihad huko Kashmir, na hivyo kusitisha ukamuaji mkubwa wa jeshi na uchumi wa India. Kuachana na faradhi ya Kiislamu ya Jihad kumeiweka India huru kuibuka kama mshirika wa Marekani dhidi ya mpinzani wa Marekani, China, kujipenyeza kwa kina ndani ya Afghanistan na kuanzisha kampeni ya kikatili dhidi ya ndugu zetu Waislamu nchini India, masikiti, hijab na heshima ya Mtume (saw).

Enyi Waislamu wa Pakistan! Takeni kukomeshwa kwa ushirikiano na Marekani, ambayo inadhoofisha Jeshi la Pakistan mbele ya India, kwa kutumia "vizuizi." Kwa kutii maagizo ya Marekani, Mafundisho ya Bajwa yalikuza simulizi ya "hakuna nafasi kwa vita". Mpango wa Marekani ni "kupunguza" uwezo wa jeshi lenye nguvu la Pakistan, kupunguza uwezo wake wa kijeshi na kinyuklia, huku ukiongeza kwa kasi ule wa India. Kwa kufanya hivyo, maafisa wetu wa jeshi sasa wamevunjwa moyo, kwa dhana potofu ya ubora wa kijeshi na kiuchumi wa India juu yetu.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Takeni kukomeshwa kwa ushirikiano na Marekani, ambayo iliwalazimisha mujahidina wa Afghanistan kufanya makubaliano, kwa ajili ya kuondoka salama kwa jeshi la Marekani lililoshindwa, huku ikiunasa uongozi wa Afghanistan ndani ya mfumo wa kiulimwengu wa Marekani. Ushirikiano na Marekani unahakikisha kwamba uhasama katika maeneo ya makabila yanayopakana na Afghanistan unachochewa, kwa kuweka njia ya anga ya 'Boulevard' kwa droni za Marekani kuwa wazi, juu ya vichwa vyetu. Wanajeshi wetu sasa wanajishughulisha sana kwenye mpaka wetu wa Magharibi, na kuifanya India kuwa na mshiko zaidi juu ya Kashmir Iliyokaliwa kimabavu na eneo hilo. Zaidi ya hayo, Mafundisho ya Bajwa yalitunyima nafasi ya kuiunganisha Pakistan na Afghanistan kama dola moja, na kutuimarisha dhidi ya India.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Takeni kukomeshwa kwa Raj mkoloni wa Kimarekani ambaye amekipa uhai chombo cha Amerika cha kutudhibiti juu yetu, mfumo wa Demokrasia. Mabwana wa Kiamerika wa Bajwa walishtushwa na kukua kwa ukataliwaji wa Demokrasia miongoni mwetu, pamoja na hamu yetu ya mfumo wa utawala wa Kiislamu, Khilafah. Mafundisho ya Bajwa yalihakikisha kwamba tunaelekeza nyuso zetu tena kwa Demokrasia iliyofeli, tukirefusha uhai wake. Kwa hivyo, utawala ulibadilika kutoka kwa PML-N hadi PTI, na kisha kurudi tena kwa PML-N, na kusababisha machafuko ya ndani. Kwa hakika, ushirikiano na Marekani unatunyima fursa ya kujiondoa katika Demokrasia, kwa kuhakikisha utawala kwa yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyateremsha.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Majeshi yao! Sisitizeni sasa juu ya kusimamishwa tena kwa Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itakomesha aina zote za ushirikiano na Marekani, ikiwemo Mafundisho ya Bajwa. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9]. Jueni kwamba chochote chini ya hiki, hali itakuwa ile ile.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu