Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Ramadan 1442 Na: 1442 / 70
M.  Jumapili, 02 Mei 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Kipindi cha Mwezi Uliobarikiwa wa Ramadhan, Wito wa Kuachiliwa Huru Naveed Butt, Mtetezi Halisi wa Khilafah, Aliyetekwa Nyara Tangu Mnamo 11 Mei 2012

(Imetafsiriwa)

Enyi Watu wa Nguvu na Ushawishi! Tunatoa wito kwenu mtumie nguvu na ushawishi wenu kuhakikisha kuachiliwa huru kwa kaka yenu mheshimiwa, Naveed Butt. Tunatoa wito kwenu kama watoto watiifu wa Umar al-Farooq (ra) na Hamza (ra), bwana wa mashahidi, ambao waliuimarisha ulinganizi wa Uislamu kwa nguvu na ushawishi wao, wakipata radhi ya Mwenyezi Mungu (swt).

Naveed Butt anajulikana vyema kwetu sote kama kiongozi mwaminifu, mtetezi wa Khilafah kwa Njia ya Utume (saw) na msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan. Ndugu yetu mheshimiwa Naveed alikamatwa mnamo 11 Mei 2012 na majambazi wa watawala wakati huo, utawala wa Kayani-Zardari. Mnamo 11 Mei  2021, itakuwa imetimu miaka 9 kamili ya ukandamizaji kwa muumini ambaye uhalifu wake pekee ni kusema kwamba Mola wake ni Mwenyezi Mungu (swt) peke yake. Katika mwezi huu uliobarikiwa wa Ramadhan, na thawabu zake nyingi kwa walio wema, tunatoa wito utoe kwenu kunyanyua kesi yake na kutaka aachiliwe huru, ili mwaka wa kumi wa uonevu usipite. Tunatoa wito kwenu mumsaidie Naveed katika mateso yake na mateso ya familia yake, huku tukikukumbusheni maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye amesema,

«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ»

“Yeyote anayempa afueni muumini kutokana na tatizo miongoni mwa matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atampa afueni kutokana na tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama” [Muslim].

Enyi Watu wa Nguvu na Ushawishi wa Pakistan miongoni mwa Wanachuoni, Waandishi wa Habari, Wanasheria au Jumuiya ya Biashara kati ya Wengineo! Nguvu zetu, ushawishi, hadhi na fadhila sio chochote isipokuwa neema ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo inaweza kuchukuliwa kutoka kwetu wakati wowote. Hakika, nguvu zetu, ushawishi, hadhi na fadhila ni amana ambazo tutahesabiwa na Mwenyezi Mungu (swt). Huku maisha yetu yanavyokaribia mwisho wake usioweza kuepukika, ni wakati muafaka kwamba tuwekeze nguvu na ushawishi wetu katika mahali pazuri, katika kumtumikia Mwenyezi Mungu (swt) na kwa kudhihiri kwa Dini Yake. Tutawekeza uwezo wetu katika wakati ambao Umma wa Kiislamu umeamka kwa ajili ya lengo lake katika Dunia hii, ibada kamili ya Mwenyezi Mungu (swt), kupitia utekelezaji wa Uislamu kama mfumo wa maisha, mamlaka na dola. Kwa kweli, wito wa Khilafah sasa ni hitaji kuu la Umma wa Kiislamu, ambao umekata tamaa kwa watawala wa sasa, ambao hawajaleta chochote isipokuwa mateso na fedheha kupitia upotofu na dhambi zao. Kwa kweli, bila uongozi wenye kuongoza, Umma wa Kiislamu ni kama yatima aliyetelekezwa, asiye na mwajibikaji wake au mlezi, kwa kuwa ardhi zake zimekaliwa, utajiri wake umeporwa na heshima ya Mtume (saw) inashambuliwa mara kwa mara bila majibu yanayofaa.

Enyi Wana wa Umar al-Farooq (ra) na Hamza (ra), Bwana wa Mashahidi! Kwa kweli, jamaa imekusanyika na inahitaji Imam wa kuiongoza. Ni sisi, watu wenye nguvu na ushawishi ambao tunapaswa kutekeleza wajibu wetu na kuwaongoza Waislamu kwenye mabadiliko ya kweli, bila kumcha yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) Ndugu yetu Naveed ndivyo alivyofanya na ni ukumbusho kwetu sote, kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hataleta Nasr (Ushindi) Wake bila kujitolea kwetu na kudumu kwetu juu ya haki. Kwa hivyo, ni juu yetu sote kuzungumza kwa niaba yake, tukitaka aachiliwe huru na kusimama badala yake kutaka kusimamishwa tena kwa Khilafah kwa Njia ya Utume (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ)

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo.” [Surah at-Tawbah 9:111].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

#FreeNaveedButt

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu