Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  10 Safar 1442 Na: 1442/01
M.  Jumapili, 27 Septemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi watu wa Kinana! Je! Hamtaivunja Serikali Hii Ambayo Imezivunja Nyumba za Mwenyezi Mungu na Nyumba Zenu?

Sisi tunaishi katika mazingira ya kupanuliwa kwa mapinduzi ya Januari ambayo hayakuisha, kama Magharibi na wanaume wake miongoni mwa wanajeshi waliochukua madaraka baada ya mapinduzi walivyodhani, tunaona mawimbi ya mapinduzi mfululizo ambayo yanaibuka na wakati mwingine kufifia, yakizuiwa kufikia mizizi yake na kilele cha kupasuka kwake kupitia kizuizi cha hofu ambacho serikali imekiregelea kupitia mauaji ya Rabaa, al-Nahda na kwengineko na kwa ala za ukandamizaji wake ambazo daima huelekezwa kwa watu bila ya ubaguzi wakati wa makabiliano yake na watu wa Misri na dini yao juu ya haki, na kutofaulu kwa watoto wao kutoka katika jeshi kwa kutosimama na jamaa zao dhidi ya twaghut.

Serikali hii, au tuseme genge hili tawala, lilifanya kazi kuonyesha mvutano huu kuwa ni kati ya serikali na kikundi cha watu, na kuwafanya wale wote wanaopinga maamuzi yake kana kwamba ni katika kundi hilo, wakati ukweli ukiwa wao hawawakilishi dola, lakini badala yake wao waliinyakua na kuiba rasimali na neema zake na kuzipeleka Magharibi bila gharama yoyote. Na kundi hilo haliwakilishi watu wala mapinduzi, bali wao walikuwa ni sababu ya moja kwa moja ya kurudi kwa genge la jeshi katika uhai wao baada ya mapinduzi ya Januari kwa ulimbukeni wao.

Genge hili la majenerali wa Amerika linatambua kuwa halimiliki suluhisho kwa shida za watu na halijui kwamba maamuzi yake mabaya yatasababisha mlipuko, ambapo hautafaa utumiaji wa chuma na moto kukandamiza watu au kipimo cha dawa za kutuliza maumivu ambazo hutangaza kwenye vyombo vya habari ili kuwatuliza watu, wala safari ya kusafiri kati ya wanaonufaika na wadau wa maslahi ili kujaribu kuwadhibiti wanamapinduzi. Na laiti udhibiti huu ungekuwa wa kihakika kwa vitendo na zawadi zenye kushikika, bali kwa maneno matamu na matamanio yaliyotawanyika hapa na pale, kana kwamba kuna mtu anasambaza mangati kwa watu!

Wakati serikali ikiendelea kwa ukali na kiburi kilichoonyeshwa na mkuu wa genge hilo akitishia jeshi kuteremka katika kila kijiji nchini Misri kutekeleza maamuzi yake ya kubomoa nyumba na misikiti, na hakuthubutu kushambulia kanisa hata moja huku akibomoa zaidi ya misikiti sabiini kwa kisingizio kwamba iko kwenye ardhi ya serikali, hii ni baada ya miaka mingi ya misikiti kufungwa moja kwa moja baada ya kila swala na kutoruhusiwa pia ndani yake shughuli yoyote, huku makanisa yakifunguliwa kwa saa nzima na genge hili likiwa halithubutu kupunguza dori zake au kuyazuia kutangaza fikra yake. Kwa hakika, hili haliwakeri, bali Uislamu ambao unatafuta kurudisha haki za watu ambazo wanazisulubu na kuzipora, ndio unaowakera.

Kisha wanajitokeza kwetu Masheikh watiifu wa serikali, wakidai ubatilif wa swala katika misikiti hiyo, na ulazima wa kuibomoa bila ushahidi wowote na ulazima wa kuzibomoa nyumba za watu ambazo zinawasitiri na ambazo wamezijenga kwa kazi yao na jasho lao kwa miaka mingi na kuweka mali zao zote na akiba ndani yake, katika hali ya kutokuwepo kabisa kwa dola ambayo ni wajibu juu yake kuwachunga, hadi genge likaja kuzibomoa nyumba hizo juu ya vichwa vyao na kuwatupa nje wao na watoto wao, huku wakiwa wamejikunyata ...

Huku majumba, hoteli, maduka, sehemu za biashara na maeneo mengine yakiwa yamejengwa kwa ajili ya wanachama wa genge hili na wale waliokusanyika kwenye ardhi hiyo inayomilikiwa na serikali, kama wanavyodai, na hakuna mtu aliyesubutu kuyagusa, achilia mbali kuyabomoa, na huku serikali ikiweka hali ya ukali kwa watu wote isipokuwa wanajeshi, ambao huwaongeza mishahara yao na pensheni mara nyingi, mbali na kuwapa fadhila ya kufurahia huduma ambazo watu wengine hawazifurahii, labda wao ni jamii nyingine isiyokuwa ya kibinadamu, na pengine kwa hili ndio maana wanashiriki katika kuua watu!

Na mbele ya ubomoaji wa nyumba na misikiti juu ya vichwa vya watu, walitoka nje na kusema haki na kweli (hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na al-Sisi ni adui wa Mwenyezi Mungu), hata ikiwa yeye sio adui pekee, bali genge lote la majenerali na wale wanaowasaidia wote ni maadui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, dini yake na Ummah wake.

Enyi watu wa Kinana! Hakika katika jukumu la dola kwa raia wake ni kushibisha mahitaji ya kila mmoja wa raia wake kwa kiwango cha kutosha katika vitu tatu: chakula, mavazi na makazi, na kumpa mahitaji ya ziada kadri inavyowezekana, na katika hili hakuna tofauti kati ya Muislamu na asiyekuwa Mwislamu, badala yake kila mtu ni sawa, na lazima iidhamini jamii kwa ujumla wake vitu vitatu kwa kiwango cha juu kabisa na ikiwezekana bila malipo: usalama, elimu na huduma za afya, kwa usalama inamaanisha kusalimika maisha yao, pesa na akiba, na kuhifadhi dini yao na utu wao, sio kubomoa nyumba zao, kukiuka utu wao na kuwaibia akiba yao kama genge hili linavyofanya sasa. Kwa katika elimu, ni kudhamana kiwango cha juu kabisa cha elimu ikiwezekana bila malipo kwa wote. Hakuna tofauti kati ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu, wala matajiri na maskini, wala hakuna shule za matajiri na zingine kwa masikini. Badala yake, dola inaondoa utabaka na uaswabiya na kila kitu kinachozalisha haya. Ama katika usimamizi wa afya, itatoa madaktari na madawa kwa watu wote kwa kiwango cha juu kabisa na ikiwezekana bila malipo. Hakuna tofauti baina ya tajiri na masikini wala Muislamu na asiyekuwa Muislamu, bali kwa watu wote kwa usawa. Inajishughulisha yenyewe na inafanya muamala yenyewe, hakuna muamala spesheli kwa wasomi, majenerali, wala utofauti kwa wanajeshi au wengine, bali kila mtu ni sawa.

Lakini, haya yote hayatimizwi kwa ahadi za genge la majenerali, wala hayamilikiwi na urasilimali ambao wanatawala kwao. Badala yake, yanamilikiwa na Uislamu, ambao wanaupiga vita na mfumo wake, ambao wanatafuta kuuzuia katika kurudi kutawala ndani ya dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi watu wa Kinana! Yeyote anayevunja nyumba za Mwenyezi Mungu na nyumba zenu hastahili kuwatawala, na kumuasi kwenu ni wajibu, na hakika mapinduzi yenu hayakamiliki na kamwe hayatakamilika isipokuwa kwa kuubeba Uislamu na mradi wake wa kihadhara ambao unahakikisha utu wenu, uhuru wenu na ustawi wenu, na unakuhakikishieni uadilifu kama uadilifu wa Umar ambao mnaujua. Basi msikubali chochote kisichokuwa Uislamu na mfumo wake na dola yake Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, dola kamili inayotabikisha Uislamu kwa ukamilifu wake na kwa uadilifu wake. Hii ni haki yenu basi idaini wala msikubali chochote chini yake ili msirudi kwenye nukta ile ile na kutawaliwa na genge lile lile kwa majina tofauti!

Enyi wenye ikhlasi katika jeshi la Kinana! Basi na upooze kila mkono ulioshiriki katika kubomoa misikiti na nyumba za wanyonge miongoni mwa watu na wasio na usaidizi, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَى فِي خَرَابِهَا أُوْلَـئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلاَّ خَآئِفِينَ لهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

"Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa." [Al-Baqara: 114] kwani ni nani aliye na dhalimu zaidi kuliko serikali hii unayovunja nyumba za Mungu?! Serikali hii ambayo mnaihami ndiyo ambayo ni wajibu ivunjwe, sio misikiti na nyumba za watu ambazo zimebomolewa chini ya masikio, macho, na uchungaji wenu, bali kwa mikono yenu wenyewe, mtakutana vipi na Mola wenu kwa mikono iliyochafuliwa na damu ya watu wasio na hatia na kwa nyuso ambazo hazikugubikwa kwa vumbi la Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu, bali zimegubikwa vumbi la vifusi vya misikiti na nyumba za watu?!

Basi andaeni jibu lenu na hoja yenu, au tangazeni kuwa mbali na genge hili la maafisa wa jeshi la Amerika na liacheni lizame bila yenu, kwa sababu Amerika haitajilinda na watu hawataionea huruma, kwa hivyo msiwe katika kundi lake, na mjue kuwa yote ambayo serikali hii unakupeni ili kuhakikisha uaminifu wenu ni kiasi kidogo cha baadhi ya haki zenu, kwa hivyo msizichukue kama hongo na kisha mkawapa watoto wenu pesa chafu (Al-Suht), na chukueni haki zenu kamili kwa kuwapendelea jamaa zenu katika mapinduzi yao na mnusuru mradi pekee wa Ummah wa kihadhara ambao Hizb ut-Tahrir unauwasilisha na ni dhamana ya haki, uhuru na utu wa watu kwa kutabikisha Uislamu kikamilifu na kwa upana katika dola yake ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe yale yaliyotangulia na akakubali kutoka kwenu na akafungua mikononi mwenu na Misri ikaokoka na hata Ummah mzima kupitia nyinyi. Je! Mtakuwa na furaha iliyoje lau mtafanya hivi, na Misri itakuwa na utukufu ulioje, na Uislamu na Waislamu, kupitia nyinyi, na mtayakumbuka haya tuyokuambieni sasa na tunalikabidhi jambo letu kwa Mwenyezi Mungu.

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu