Jumatatu, 04 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  24 Rabi' I 1446 Na: H.T.L 1446 / 05
M.  Ijumaa, 27 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Anayetafuta Hifadhi katika Umoja wa Mataifa na Mfumo wa Kimataifa ni kama Yule Anayetafuta Hifadhi kutoka kwenye Kikaango hadi ndani ya Moto!
(Imetafsiriwa)

Huku umbile la Kiyahudi likishambulia Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na Lebanon bila majibu yoyote, isipokuwa kutoka kwa watu binafsi au vikundi, wenye nguvu zisizolingana hata ushuri moja ya zile ambazo wahalifu wakubwa wa mfumo wa kimataifa walizotoa kwa umbile la Kiyahudi; Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati leo ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulishinikiza umbile la Kiyahudi kukomesha uvamizi dhidi ya Lebanon, na anashukuru Ufaransa na Amerika kwa mpango wao wa kusitisha mapigano, na Waziri wake wa Mambo ya nje Abdallah Bou Habib alimtangulia kwa kutangaza kwamba Amerika ndio ufunguo wa wokovu wetu na tumaini limeegemezwa juu yake.

Je, viongozi hawa wanapuuza au kusahau ukweli wa Umoja wa Mataifa na matendo yake ambayo ni adui kwa Waislamu na yenye upendeleo kwa umbile la Kiyahudi?! Au pengine wamesahau kuwa maamuzi ya msingi katika uasisishwaji wa umbile hili yalikuwa ni matokeo yake, na matokeo ya nchi hizi wanazozishukuru na kuziwekea matumaini! Je, umbile hili halikulipua Gaza, Syria na Lebanon kwa silaha za Amerika, Ufaransa na Uingereza?! Je, nchi hizi kubwa hazikuzuia maazimio yaliyotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayolaani umbile la Kiyahudi?! Hivyo tunawezaje kuziomba zile nchi kuu za uhalifu zilizoliunda na kulifadhili umbile hili kusimama dhidi yake?! Je, zabibu zinaweza kuchumwa kwenye miiba?! Na je mwenye hekima hukimbilia kwa mpinzani wake?! Mna shida gani? Mnahukumu vipi?! Au je muna kitabu cha kujisalimisha na kutegemea Magharibi ambacho munakisoma?!

Enyi Waislamu: Kauli fupi na zenye manufaa kuhusu wokovu wenu kutokana na uvamizi wa Mayahudi iko katika kuyakusanya majeshi yenu ili kuwatokomeza, ama katika kuziomba nchi kubwa, Umoja wa Mataifa na mfumo wa kimataifa, ni kutupa vumbi machoni mwenu, na kukuhadaeni kuwa kila tu walichonacho watawala wenu ni kuomba kwenye milango ya wahalifu hawa. Ikiwa hili linaashiria chochote, linaashiria ulaji njama wa watawala wenu bila kumbagua yeyote pamoja na Mayahudi dhidi yenu, kwa njia ya moja kwa moja na ya wazi kama Imarati, Misri na Jordan, au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na ya wazi kama Saudi Arabia, Iran na Uturuki.

Kila mtu ameitelekeza Gaza na kuiacha iangamizwe, na vilevile Lebanon, na walitosheka kukimbilia mipango ya Amerika au Ufaransa, ambayo lengo kuu lilikuwa ni kuasisisha umbile hili, na kujaribu kufanya uwepo wake kuwa wa kawaida, huku wakiyafungia majeshi kambini mwao na kuziacha silaha zimefinikwa na kutu ya uoga na kujinyenyekesha. Ama Iran ambayo inadai kuwapinga Mayahudi, na ambayo haiachi kuasisi mzunguko wake ndani ya mzunguko wa Amerika, huku Gaza ikiharibiwa na Lebanon ikiharibiwa, viongozi wake wanatangaza kuwa wao ni ndugu wa Amerika, na kwamba hawataki vita, na wanazitaka nchi kubwa zijadiliane kuhusu suala la nyuklia la Iran, na wao ndio waliotishia na kuapa kwa miaka na vikaka kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye ramani iwapo litaishambulia Lebanon au Iran!

Enyi Waislamu: umbile la Kiyahudi ni zao la ukoloni, waungaji mkono wake ni nchi kubwa, na walinzi wake ni watawala wenu madhalimu. Kilichotokea mnamo 7 Oktoba 2023 kilifichua udhaifu wa kweli wa umbile hili la kinyama. Uvamizi wake sasa juu ya Gaza na Lebanon, kwa kuungwa mkono na makafiri wakoloni wa nchi za Magharibi na mikia ya nchi za Kiarabu, ni kuregesha fahari yake ya kirongo na kulionyesha kama mmiliki wa nguvu isiyoweza kushindwa, ingawa ni dhaifu kuliko utandu wa buibui, na hili limekuwa wazi kwa wapiganaji watiifu kwa Dini na Ummah wao.

Enyi Waislamu: Lau kama dola ya Khilafah ingesimamisha amri ya Mola wake Mlezi ingesimamishwa miongoni mwenu, ingetangaza jihad dhidi ya umbile hili na waungaji mkono wake, na ingekusanya majeshi na kuandaa njia za kuliondoa. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuahidini ushindi juu ya Mayahudi, na hakitofika Kiyama mpaka muwaue, na pengine matukio ya Kimbunga cha Al-Aqsa yatakuwa ndio mwanzo wake. Basi simameni imara, shikaneni, na yaunganisheni mambo yenu, na yakusanyeni majeshi na mregeshe uongozi wenu, na wapindueni madhalimu wanaowalinda Mayahudi na mabeberu wa Magharibi mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu mikononi mwenu, na jueni kwa yakini kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi, wala msisahau ahadi yake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” [Muhammad 47:7-8]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu