Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  14 Dhu al-Hijjah 1443 Na: H.T.L 1443 / 18
M.  Jumatano, 13 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon
Yahuisha Siku Kumi za Mwanzo za Dhul Hijjah 1443 H
(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya amali ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon ya kuhuisha siku kumi za Dhul Hijjah, hizb ilifanya mikutano ya kusherehekea Sunnah ya Mtume (saw) katika miji ya Sidon na Tripoli mnamo siku ya Alhamisi tarehe 8 Dhul Hijjah na Ijumaa 9 Dhul Hijjah. Matembezi haya yalitembea barabara kuu za jiji na masoko yake, yakisindikizwa na takbira na tahlil. Nyuso za watazamaji barabarani, kwenye magari yao, na kwenye roshani za nyumba zao, wakipiga picha za amali hizi, wakitamka takbira na tahlil, zilijawa na furaha. Ikiwa hii inaashiria chochote, inaashiria utukufu wa Uislamu na ibada zake katika nyoyo za watu licha ya kampeni zote za Magharibi na majaribio ya kuwaweka mbali na Uislamu, na hata majaribio ya kupotosha hukmu na amri zake. Utukuzaji huu unaakisi maneno ya Mola wetu Mlezi (swt):

 [ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ]

“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” [Al-Hajj: 32].

Nyoyo za Waislamu zimejaa Uislamu, lakini wanasubiri tu mtu awaongoze katika njia sahihi na kurudisha izza ya Uislamu na watu wake.

Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Lebanon kilikuwa na washiriki wachangamfu katika maandamano haya, ambayo yaliakisi dori halisi ambayo Shariah ilimkabidhi mwanamke wa Kiislamu, bila kugongana na haya yake, dori yake changamfu katika mchakato wa mabadiliko, na dori yake ya awali katika kukuza vizazi. Hili liliwafanya wanawake kuwa na ujumbe maalum katika khutba ya Mtume (saw), kwa Ummah wake katika Hijja ya Kuaga katika mwaka wa kumi wa Hijra (kuhama) “...kuweni na huruma kwa wanawake,” hii inapinga miito yote ya dhambi ya kumhujumu mwanamke wa Kiislamu, hijabu yake na dori yake; iliyojaribiwa na zile zinazoitwa harakati za utetezi wa mwanamke za Magharibi.

Miongoni mwa amali zao, walifanya amali ya maingiliano katika afisi ya Hizb ut Tahrir katika eneo la Mirayata, chini ya kichwa "Katika Siku Kumi Zilizobarikiwa za Dhul Hijjah" mnamo tarehe sita ya Dhul Hijjah, ambayo ilijumuisha ufafanuzi wa aya za Hijja, ibada kuu zaidi katika siku hizi kumi, na shairi la mtu binafsi lenye kibwagizo “Kwako, Bwana wangu, nimekuja kuitikia.” Na kalima yenye kichwa "Masiku Kumi", kisha hotuba yenye kugusa moyo kwa anwani, "Enyi Waislamu, Hajj bila Amiri?!" Ndani yake, mmoja wa wanawake wanachama wa Hizb ut-Tahrir alizungumza juu ya ulazima wa kumteua mtawala kwa ajili ya Hijja ambaye ndiye anayeamua siku ya Hijja yao na kuwaongoza katika ibada au kumteua atakayefanya hivyo, ambaye mwangalifu kutoharibu Hijja zao. Kukosekana kwa Dola ya Khilafah na Amiri wa Hijja hakubadilishwi na waongozi na wakuu wa dola, na chochote kinachopelekea katika wajib (ulazima) kinakuwa ni wajibu vilevile. Waislamu lazima washirikiane na wanaofanya kazi ili kusimamisha Khilafah na Khalifa. Amali hii ilihitimishwa kwa kaswida iitwayo “Mola Wangu ni Mwingi wa Ukarimu na ni Mola wa Nyumba na Patakatifu” na dua na maingiliano kutoka kwa waliohudhuria pamoja na tahlil na takbira.

Hitimisho la amali za hizb katika vitengo vyake viwili (wanaume na wanawake) lilikuwa ni swala ya pamoja ya Idd katika kuhuisha ibada ya Swala ya Idd katika uwanja wa wazi, ambao hizb imezoea kuutumia kuswali katika mji wa Tripoli kaskazini mwa Lebanon, nchini Lebanon. Uwanja wa Shira' huko Abu Samra, ambapo Ustadh Ahmad Al-Qasas alitoa hotuba na akazingatia miito ya kimatata ambayo imeanza kuonekana katika jamii, chini ya majina potofu kama vile "ushoga" na mengineyo, akionyesha hatari yake na haja ya kukabiliana na mambo haya machafu na wale wanaoyatetea katika nchi za Kiislamu kwa jumla na hasa nchini Lebanon.

Kwa kutamatika siku kumi na siku ya Idd na siku za Tashriq, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt), kwamba Idd inayokuja itakuwa chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na chini ya bendera ya Khalifa wa Waislamu na Imam wao, ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amemsifu kama:

«...وإنَّما الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن وَرَائِهِ ويُتَّقَى بِهِ»

“Na hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo, Na tunarudia tena wito wetu kwa Waislamu wa Lebanon washirikiane na Hizb ut Tahrir kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume katika njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo Hizb ut Tahrir inaifuata ili kufikia bishara yake njema (saw):

«...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Hili ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kulitimiza

[إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3].

Mwenyezi Mungu (swt) azikubali ibada zenu, Idd Mubarak na kila mwaka muwe karibu na Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu