Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  3 Jumada II 1443 Na: 1443 H / 01
M.  Alhamisi, 06 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kyrgyzstan Yakoleza Vita vyake dhidi ya Uislamu chini ya Kisingizio cha “Misimamo Mikali”
(Imetafsiriwa)

Mnamo 2021, katiba mpya ilipitishwa nchini Kyrgyzstan. Tangu wakati huo, juhudi zimefanywa kuoanisha sheria na katiba mpya. Ndani ya muundo wa kazi hii, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa sheria "kupambana na shughuli za watu wenye msimamo mkali," na kuwasilisha rasimu ya sheria hiyo kwa ajili ya majadiliano ya umma kuanzia tarehe 29/12/2021 hadi 28/1/2022.

Inajulikana kuwa makafiri wa kikoloni wanaficha vita vyao dhidi ya Uislamu kwa kisingizio cha "misimamo mikali". Katika nchi za Kiislamu, vibaraka wao hutekeleza njama za Makafiri kwa kutabanni na kutabikisha sheria hizo. Ni dhahiri kutokana na rasimu ya sheria hiyo hapo juu kwamba serikali inakusudia kutoa sheria hii ili kuwaridhisha mabwana zake makafiri.

Kwa mfano, mswada huu unajumuisha vifungu vifuatavyo:

Kifungu 1 - Msingi wa kisheria wa kupambana na shughuli za misimamo mikali

Msingi wa kisheria wa kupambana na shughuli za misimamo mikali ni kanuni na sheria zinazotambulika kiulimwengu za sheria ya kimataifa, pamoja na mikataba ya kimataifa.

Kifungu 5 – Ushirikiano wa Kimataifa katika Kupambana na Misimamo Mikali

Asasi za serikali ya Jamhuri ya Kyrgyzstan zinashirikiana na mashirika ya Haki za Kibinadamu ya nchi za nje kwa misingi ya makubaliano ya kimataifa ya Jamhuri ya Kyrgyz, pamoja na mashirika ya kimataifa.

Sio siri kwa mtu yeyote kwamba sheria ya kimataifa, mashirika ya kimataifa na mikataba ya kimataifa ni kamba ambayo makafiri wakoloni wameifunga shingoni mwa nchi yetu.

Kwa hakika, sheria hii dhidi ya Uislamu haikutolewa kwa mara mmoja nchini Kyrgyzstan, bali ni mwendelezo wa sheria za awali kwa ukamilifu zaidi. Mswada wa sasa unatofautiana na iliyoutangulia katika mambo matatu yafuatayo:

1- Serikali ya sasa ya Kyrgyzstan inajaribu kuuleta mswada huu kuafikiana na Mkataba wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai kuhusu Kupambana na Misimamo mikali. Hii ina maana kwamba itazifuata Urusi na China katika "vita dhidi ya misimamo mikali". Kwa maana nyengine, maafisa wanaiga hatua kali zinazochukuliwa na Urusi na China katika kuupiga vita Uislamu na Waislamu na kuwaridhisha nazo mabwana zao makafiri.

2- Kupanua uainishaji wa "Misimamo mikali" kujumuisha washindani "wa kisekula" kwa serikali ili kuwashinikiza kwa sababu ufafanuzi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai wa misimamo mikali inaruhusu. Ndiyo maana makundi ya upinzani yanayoegemea Magharibi yamekuwa yakifanya mjadala wa meza ya pande zote kwa miaka miwili mjini Bishkek na wataalamu wa kimataifa kuhusu "Haki za Binadamu katika Kupambana na Misimamo mikali". Kwa kufanya hivyo, makundi ya upinzani yanayoegemea Magharibi yanajaribu kujilinda kutokana na tuhuma za misimamo mikali. Hata hivyo, ikiwa sheria hiyo itaanza kutumika, matendo ya makundi yanayoegemea Magharibi hayatawasaidia. Kwa sababu kabla ya sheria hii kupitishwa, serikali ilianza kuwatuhumu baadhi ya wanachama wa upinzani kuwa na msimamo mkali. Ikumbukwe kwamba wakati fulani masekula walifurahi wakati Waislamu wenye ikhlasi walipotuhumiwa kuwa na msimamo mkali na kuadhibiwa vikali. Sasa tuhuma za misimamo mikali zimewafikia wao.

3- Kufikia sasa, mashirika 21 ya kidini yamepigwa marufuku kuendesha shughuli nchini Kyrgyzstan na washiriki wao wamekabiliwa na adhabu mbalimbali. Sheria hii sasa inawalenga "Waislamu wenye misimamo wastani" ambao shughuli zao hazijapigwa marufuku hapo awali, kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani: "Shughuli za uasi za mashirika ya kidini na baadhi ya raia zinafanywa nchini Kyrgyzstan kwa kisingizio cha hisani, elimu au kazi nyingine zenye umuhimu wa kijamii. Ingawa hakuna dalili za misimamo mikali na vurugu katika hatua fulani, zinatishia maisha ya raia, jamii na nchi nzima." Kauli hii ina maana kwamba - wakati utakapofika - taasisi za misaada za Salafi na Jumuiya ya Tabligh zitapigwa marufuku. Hata kutoka kwa Gülenist.

Kwa hakika, hatua hizi zilianza kabla ya sheria hii kupitishwa. Wagombea wamepigwa marufuku kutumia lugha ya kidini katika chaguzi zilizopita za ubunge. Wagombea waliojitambulisha kuwa "Uislamu wa wastani" walishiriki katika uchaguzi huo bila hata mmoja wao kusema neno lolote kuhusu Uislamu. (Walikaa kimya kuhusu marufuku hii, kwa hivyo wanawezaje kuitumikia Dini mbele ya marufuku hii baada ya kufika Bungeni?). Kinyume chake, milango iko wazi kwa "wahubiri" wanaojadili Uislamu kwa mtazamo wa falsafa ya Magharibi. Kwa mfano, baadhi yao walisema siku iliyotangulia, "Sherehe ya mkesha wa Mwaka Mpya sio tu inaruhusiwa, lakini ni wajibu,"

Hizi ndizo nukta kuu za sheria hii. Ni wazi kwamba serikali ya Kyrgyz inakusudia kuzidisha vita vyake dhidi ya Dini yetu. Zaidi ya hayo, lengo hili linaakisiwa katika fahamu mpya ya kidini iliyotabanniwa na sheria iliyosasishwa ya jinai juu ya "misimamo mikali".

Lakini haya yote, Mwenyezi Mungu akipenda, yatafeli; kwa sababu pengo la kimfumo na kisiasa nchini Kyrgyzstan linazidi kuongezeka, kama ilivyo ulimwenguni na katika eneo hilo. Uislamu utaliziba pengo hili la kimfumo, na Waislamu wenye ufahamu wa kisiasa watalijaza pengo la kisiasa, Mwenyezi Mungu akipenda, na njama za makafiri wakoloni na vibaraka wao zitawageuka.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ]

“Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.” [Al-Anfal: 30].

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu