Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  29 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 043
M.  Ijumaa, 01 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je! Mauaji na Jinai Hizi Zote Hazijachochea Hisia ya Wajibu kwa wale wenye Vyeo na Medali Kusonga katika Ulinzi wa Watu wa Gaza?!
(Imetafsiriwa)

Alfajiri ya mnamo Jumanne, Oktoba 29, 2024, vikosi vya Kiyahudi vilifanya mauaji mengine ya kutisha kwa kulipua jengo la orofa tano la familia ya Abu Nasr, ambalo lilikuwa lahifadhi watu waliokimbia makaazi yao katika Mradi wa Beit Lahiya kaskazini mwa Gaza. Mauaji haya yalisababisha vifo vya watu 93, wakiwemo watoto wasiopungua 25, huku zaidi ya 40 wakipotea na kadhaa kujeruhiwa, wengi wao wakiwa wamenaswa chini ya vifusi.

Mauaji haya ya kutisha ni sehemu ya kampeni ya mauaji ya halaiki ambayo Mayahudi wanaendesha kaskazini mwa Gaza, huku mashambulizi ya angani na mizinga yakilenga misikiti, hospitali, timu za madaktari, kuua na kuwaweka kizuizini makumi kadhaa, na kulemaza ambulensi na mifumo ya ulinzi wa raia kwa kulenga magari yao, makao makuu, na wafanyikazi kwa kuwaua na kuwawekwa kizuizini. Makaazi, nyumba, na vituo vya dharura pia vinalengwa, na kulazimisha watu kukimbia mara kwa mara huku kukiwa na kizuizi kamili ambacho kinazuia kuingia kwa chakula, dawa, na mafuta. Haya yote ni sehemu ya mpango wa uhalifu wa kuwaondoa wakaazi wake kaskazini na kuiunganisha kwa umbile la Kiyahudi, chini ya kile kinachojulikana kama “Mpango wa Majenerali.”

Uhalifu huu wote unaoendelea na mauaji ya kutisha usiku na mchana, pamoja na miito na vilio vya kuomba msaada kutoka kwa Gaza kwa jumla na hasa kutoka kaskazini mwake, havijaamsha hisia ya wajibu miongoni mwa wale wenye vyeo na medali kuchukua hatua katika utetezi wao! Je, mishipa yao haichemki kwa hasira wanaposhuhudia mauaji haya ambayo yangepasua mawe, achilia mbali nyoyo na akili za wanadamu? Maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yamethibiti kuhusu wao:

[ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُمْ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللهِ وَمَا اللهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ]

“Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya.” [Al-Baqara:74].

Wanawezaje kuishi kwa amani huku viongozi wa Mayahudi wakijigamba kufanya mauaji makubwa, ambayo wengi wa waliouawa ni wanawake na watoto? Wanawezaje kustarehe huku Mayahudi wakitangaza kwa kiburi kwamba mkono wao unafika kila kona ya Gaza na kwengineko, bila kuzuiwa na chochote au mtu yeyote? Wanazungumza juu ya kutimiza kile kinachoitwa ndoto zao za kibiblia na kuanzisha dola yao ya madai. Je, hakuna miongoni mwenu atakaye wazuia na kunyamazisha ndimi zao za kiburi, na kuwakomesha baada ya dhulma yao na kuichafua nchi? Wameinajisi Masrah ya Mtume wetu (saw) na kumwaga damu iliyoharamishwa, ambayo kumwaga kwake, kwa mujibu wa Mwenyezi Mungu, ni kukubwa zaidi kuliko kuiangamiza Al-Kaaba.

Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, tujibuni: kwa madhumuni gani mulijiunga na jeshi, mukabeba silaha, na mukapata mafunzo ikiwa sio kulinda ardhi za Waislamu, kunusuru wanaodhulumiwa, na kuitikia maombi na vilio vya ndugu zenu wanaoteseka? Au mlichukua silaha kwa ajili ya kulinda tu tawala za wahalifu, za khiyana ambazo zimeuza ardhi na watu wake, zikakabidhi Masrah ya Mtume wenu (saw) kwa Mayahudi, na zipo pekee kwa ajili ya kulinda usalama wao tu? Tujibuni na muangalie matendo ya kishujaa ya watu wachache waaminifu na wenye rasilimali chache. Waangalieni wale ambao damu yao inachemka kwa mateso ya ndugu zao na wanaofanya operesheni za hapa na pale kwa njia hafifu zaidi. Je, ni upi udhuru wenu, nyinyi mnaomiliki mizinga na ndege? Tujibuni na muandae jibu kwa Mola wenu Mlezi Siku ya Kiyama atakapokuulizeni kwa nini mulitii viumbe na mukamuasi Muumba:

[فَاللهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]

“Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [At-Tawba:13]. Je, hamuogopi kwamba Mwenyezi Mungu atakuteremshieni ghadhabu yake na adhabu yake katika maisha haya kabla ya Akhera kwa khiyana hii?

Na Wallahi, enyi Waislamu, mnangoja nini kuchukua hatua kali baada ya mauaji haya yote? Kwa nini muchelewe kufanya kazi ya kuzing'oa tawala hizi za kihaini, za kihalifu na kuwahimiza wana wenu katika majeshi kusonga dhidi ya umbile la Kiyahudi ili kuwanusuru watu wa Gaza na Palestina yote?

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. (38) Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawba:38-39].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu