Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  9 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 020
M.  Jumamosi, 03 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Familia za Afghanistan Zawalevya Watoto wao ili Kukabiliana na Njaa

(Imetafsiriwa)

Mnamo Novemba 24, 2022, BBC iliripoti juu ya uhaba mkubwa wa chakula ambao unakumba Afghanistan. Mgogoro huo ni kiasi kwamba Abdul Wahab, baba mmoja wa kijijini, ananukuliwa akisema, "Watoto wetu wanaendelea kulia, hawalali, hatuna chakula. Kwa hiyo tunakwenda kwenye duka la dawa, tunachukua vidonge na kuwapa watoto wetu, hivyo wanahisi kusinzia." Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilitoa takwimu kwamba zaidi ya watu milioni 20 - nusu ya wakaazi - wanakabiliwa na "mgogoro" wa kiwango cha 3 au kiwango cha 4 cha "dharura" cha uhaba wa chakula. Zaidi ya watoto milioni moja walio chini ya umri wa miaka 5 wako katika hatari ya kufa kutokana na kuongezeka kwa viwango vya kunyimwa chakula na kukabiliwa na utapiamlo kwa muda mrefu. Madhara ya njaa kwa vijana hayawezi kubadilishwa kwa kuongeza tu chakula. Ukweli ni kwamba, kimatibabu, watoto wanapodumaa ukuaji wao, hata wakibakia hai, hukumbana na matatizo makubwa ya kiafya. WFP iliripoti kwamba makumi ya maelfu ya watu katika mkoa mmoja, Ghor, wametumbukia katika "janga" la utapiamlo wa kiwango cha 5, mtangulizi wa njaa. Kwa ujumla, zaidi ya asilimia 90 ya Waafghani wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa chakula tangu Agosti  2022. Kitendo cha kuruka milo au siku nzima ya kula na kujihusisha na mbinu kali za kukaa bila chakula, ikiwa ni pamoja na kupeleka watoto kufanya kazi, imekuwa kawaida. Kitendo cha hivi punde cha kuwalevya watoto ni ushahidi wa hatua za kutapatapa za watu za kupunguza mateso kwa watoto wadogo walio hatarini. Katika mkoa wa Herat, ndugu mmoja Ghulam Hazrat aliwaonyesha waandishi wa habari kipande cha tembe za alprazolam anazotumia. Dawa hizi za kutuliza hutibu matatizo ya wasiwasi. Hata hivyo, wanapopewa watoto wanaweza kusababisha ugonjwa wa figo na ini. Escitalopram na sertraline zinapatikana pia kwa bei ya kipande cha mkate.

Hali hii ya kutisha ya kuwatia watoto sumu badala ya kuwalea inatokana na kukosekana uongozi wa Kiislamu wa Khilafah kwa njia ya Utume. Marekani na serikali zengine, pamoja na Benki ya Dunia, zilifutilia mbali sifa za Benki Kuu ya Afghanistan ili kuadhibu uchukuaji mamlaka wa Taliban mnamo Agosti 15, 2021. John Sifton, mkurugenzi wa Asia wa Human Rights Watch, alisema: "Njaa ya Afghanistan inayozidi na Mgogoro wa afya ni wa dharura na mzizi wake ni mgogoro wa benki. Bila kujali hadhi ya Taliban au heshima yake kwa serikali za nje, vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa bado vinasababisha janga la nchi hiyo na kuwaumiza watu wa Afghanistan." Benki Kuu ya Afghanistan haiwezi kufikia akiba yake ya fedha za kigeni na haiwezi kushughulikia au kupokea miamala mingi ya kimataifa. Kutokana na hali hiyo, nchi inaendelea kukumbwa na mgogoro mkubwa wa pesa taslim na ukosefu wa noti. Kwa kuongezea, biashara, makundi ya misaada ya kibinadamu, na benki za kibinafsi zinaendelea kuripoti vizuizi vingi juu ya uwezo wao wa kufanya kazi. Wakati huo huo, kwa sababu wafadhili wa nje wamepunguza ufadhili wa kusaidia afya, elimu, na sekta zengine muhimu za Afghanistan, mamilioni ya Waafghani wamepoteza mapato yao.

Msaada na fedha nyingi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita zilikwenda kwa wakandarasi wa Marekani na Ulaya, na hakuna miundombinu yoyote iliyojengwa nchini Afghanistan, ambayo ni sehemu ya sababu kwa nini nchi hiyo kwa sasa ni maskini na inakabiliwa na uhaba wa chakula licha ya kwamba wavamizi walitumia utajiri wao mkubwa katika vita vyao dhidi ya Uislamu na Waislamu. Zaidi ya hayo,machache yamefanywa ili kudhamini uchumi endelevu na usalama wa chakula ambao ungeweza kufanya kazi bila ya utegemezi wa msaada wa Magharibi. Afghanistan ni mfano bora wa yale anayosema Mwenyezi Mungu (swt) kuhusu wafalme wanaovamia na kudhalilisha taifa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّةً وَكَذَلِكَ يَفْعَلُونَ]

“Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.” [An-Naml: 34].

Mwenyezi Mungu (swt) kamwe hakubali kwamba Waislamu waishi huku mambo yao yanadhibitiwa na serikali zisizokuwa za Kiislamu ambapo Mwenyezi Mungu (swt) asema: 

[وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisaa: 141].

Kwa hiyo, ni lazima tufanye kazi kwa ajili ya kuregea kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo itatabikisha Uislamu kwa ukamilifu na kurudisha uchungaji na ulinzi kwa Ummah huu, wakiwemo watoto wetu wapenzi na kuwaokoa kutokamana na mateso. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu