Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  26 Sha'aban 1443 Na: 1443/09 H
M.  Jumanne, 29 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunapongeza Umma wa Kiislamu kuingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Hizb ut- Tahrir Kenya kwa furaha inatuma salamu za pongezi kwa Waislamu nchini na kote ulimwenguni kwa ujumla kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunapoingia kwenye mwezi huu wa Rahma, Msamaha na kuachwa huru na moto, tunamuomba MwenyeziMungu (swt) atupe nguvu na afya za kutelekeza ibada tukufu ya swaum ambayo sio faradhi tu bali pia ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.

Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala ameufanya uchaMungu kuwa ndio lengo hasa katika ibada hii tukufu. Uchamungu ndio msingi wa utambulisho wa Kiislamu unaopaswa kudhihirika na kuonekanwa katika matendo yote ya waumini katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake. Na ili jamii nzima iweze kuwa na uchaji Mungu kunahitajika dola inayowajibika katika kutekeleza Uislamu katika nyanja zote za maisha. Tunaeleza bayana kwamba dola hii sio nyengine bali ni Khilafah ambayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu itasimamishwa katika mojawapo ya nchi za Kiislamu.

Jamii ya Kiislamu inapoingia katika mwezi huu uliobarikiwa, bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia, mafuta, unga wa ngano, sukari ni ghali sana. Huku wananchi wakiendelea kuteseka na wengine kufariki kutokana na njaa kali katika baadhi ya maeneo nchini, wanasiasa wa mirengo yote ya kisiasa wamejikita katika kampeni za domo kaya kujitafutia vyeo huku wakiwaahidi Wakenya maskini ahadi tupu! Hili linafaa kuwa ukumbusho tosha kwa jamii ya Kenya kwamba uongozi wa kibepari haujali maslahi ya raia wake.

Ingawa vita vya Ukraine vimeathiri uchumi wa dunia kwa kiasi fulani kwa kuzingatia hali ya soko ya bei ya mafuta duniani kwani  vita hivi  vinazunguka mataifa yanayoongoza, hii hata hivyo, sio sababu kuu kabisa ya mfumko wa bei wa sasa wa kimataifa. Mfumo wa uchumi wa kibepari umefanya bei kuwa msingi wa uzalishaji na usambazaji wa mali. Zaidi ya hayo, Mfumo hutumia sera ya fedha za makaratasi bila thamani ya ndani katika sarafu yake kuifanya iwe ya kupunguka kwa bei kila mara.

Twamoumba Mwenyezi Mungu SWT atakabali amali zetu na kuupa Umma huu mlinzi na kinga halisi nayo ni Khilafah kwa mfumo wa Utume. Khilafah ndio kwa mara nyengine tena itawanasua wanadamu kutoka majanga haya ya Kiuchumi.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu