Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  13 Rabi' I 1442 Na: 1442/04 H
M.  Ijumaa, 30 Oktoba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Kenya yafanya maandamano baridi kutetea hadhi ya Mtume (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie)

Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020,wanaharakati wa Hizb ut-Tahrir/ Kenya walifanya msururu wa maandamano baridi ya kutetea hadhi ya bwana Mtume Muhammad (Rehema na Amani za MwenyeziMungu zimshukie Yeye na Aali zake). Maandamano haya  yalifanywa baada ya swala ya Ijumaa katika Miji mikubwa ya Nairobi na Mombasa sambamba na miji mengine ya ukanda wa pwani.

Kwenye maandamano hayo wanaharakati wa Hizb ut-Tahrir walinyanyua mabango yaliyokuwa na ujumbe usemao:

Khilafah: Kutetea Mtume wetu ni kutetea Imani yetu

Khilafah ndio itakayolinda Heshima ya Mtume wetu

Maandamano haya yaliandaliwa kama hatua ya kupinga vikali matamshi yanayoabiri chuki dhidi ya Uislamu ya rais wa Ufaransa Emanuel Macron kudunisha Uislamu na matukufu yake sambamba na kuunga mkono vibonzo vya kumtusi Mtume mtukufu (saw). Nao wazungumzaji walibainisha bayana fikra ya kikafiri ya uhuru wa maoni ambayo Macron na wandani wake huunga mkono wahuni wao kueneza chuki dhidi ya Uislamu na matukufu yake.

Uhuru wa kuzungumza ambao wamagharibi wameifanya kuwa ni fikra yenye kukubalika kiulimwengu, humaanisha kuwa mwanadamu ana haki ya kueleza wazi na kulingania rai yoyote ile juu ya chochote kile au jambo lolote lile pasina na mipaka. Kwa mantiki hii, kitendo cha hivi karibuni cha Samuel Paty mwalimu wa shule huko Ufaransa kumtukana Mtume (saw) kikaungwa mkono na viongozi wote wa kimagharibi ‘walinzi wa fikra ya uhuru wa kuzungumza. Kinaya ni kwamba viongozi hao hao wameunda kanuni za kinyama na sera mbovu zinazolenga kunyamazisha Waislamu na harakati zao wanaopinga dhulma na unyanyasaji wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Fauka ya haya wale walinganizi wa suala la kuisimamisha upya Khilafah na sheria na masuala mengine ya Kiislamu basi huitwa ni wenye misimamo mikali!

Mtume Muhammad (saw) anachukua sehemu kubwa katika imani ya Waislamu kiasi cha kwamba Uislamu wa mtu haukubaliki ila baada ya Kumwamini Mwenyezi Mungu pia analazimika kuamini utume wa Mtume Muhammad (saw). Ni kosa kubwa kihakika kuivunja heshima ya Mtume Muhammad (saw) kwani Mwenyezi Mungu yeye mwenyewe ametangaza kuwa Mtume (saw) yupo katika tabia njema. Kwa maana hii, Waislamu huwajibishwa kumpenda zaidi Mtume (saw) kuliko watu wote.

Katika hadith aliyoipokea Anas Bin Maalik (ra) kuwa Mtume (saw) alisema:

«لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ»

 “Hawi na Imani mmoja wenu hadi mimi niwe kwake ni mwenye kupendwa zaidi kuliko hata anavyopenda wanawe, wazazi wake na watu wote kwa ujumla.

Hizb ut-Tahrir/ Kenya, kwenye maandamano hayo ikakariri kwamba ni Khilafah pekee ndio itakayolinda na kutetea heshima ya Mtume Mtukufu Muhammad (saw)

Shabani Mwalimu

Mwakililishi kwa Vyombo Vya habari Hizb ut-Tahrir Kenya 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu