Jumatano, 08 Shawwal 1445 | 2024/04/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  15 Rajab 1445 Na: 1445 / 10
M.  Jumamosi, 27 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ushindi wa Mujahidina katika Operesheni ya Al-Maghazi na Mauaji ya Makumi ya Wanajeshi wa Uvamizi ni Pigo Uchungu kwa Umbile Duni la Kiyahudi na Kofi Katika Nyuso za Watawala wa Udhaifu na Utegemezi
(Imetafsiriwa)

Jeshi la umbile la Kiyahudi lilikiri kwamba wanajeshi wake 24 waliuawa, na pengine zaidi, katika operesheni moja iliyofanywa na Mujahidina huko Gaza karibu na kambi ya Maghazi baada ya kulipua kifaru na kuharibu majengo ambayo ilikuwa imeyawekea mtengo wa mabomu, ambamo askari wa uvamizi wa Kiyahudi walizikwa chini ya vifusi. Viongozi wa Kiyahudi waliielezea kuwa ni maafa na siku ngumu yenye hasara kubwa zaidi tangu kuanza kwa vita hivyo, lakini ilikuwa, shukrani kwa Mwenyezi Mungu, siku ya ushindi katika uthabiti na jihad.

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini [At-Tawbah 9:14].

Baada ya siku 109 kupita tangu Vita vya Gaza, ambapo idadi ya mashahidi na majeruhi inaendelea kuongezeka na mahitaji yote ya maisha kuharibiwa, vikosi vya Mujahidina bado vinapigana kwa ujasiri wote, kuwashinda adui katika pande zote, na kufanikiwa kuwapa pigo zito Mayahudi kwa mauaji na uharibifu, kuwafanya wawe salama katika ardh ya Gaza.

Kwa kuzingatia operesheni hii ya kijasiri, ushindi wa Mwenyezi Mungu kwa mujahidina, na uthabiti wa watu wake wenye subira, tunathibitisha yafuatayo:

1- Katika wakati ambapo serikali zinazotawala katika nchi za Kiarabu na Kiislamu zinafanya kila juhudi na mashirika ya jumuiya ya kimataifa ambayo yanasita kuleta usitishaji vita, ili kuzuia aibu yao, ikiwa wataaibika, na kuondoa mashinikizo ambayo yanaongezeka kila siku ambapo vita dhidi ya vyombo vyao vinadumu, kichapo hiki ni sawa na kofi la usoni mwao na kuondoa shaka juu ya kushindwa kwao kuwanusuru watu wa Palestina na Gaza.

2- Hapana shaka kwamba jeshi la Kiyahudi na umbile lao ndio viumbe waoga zaidi wa Mwenyezi Mungu,

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِنَ اللهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ]

“Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge.” [Aali Imran 3:112]. Ummah umeshuhudia uoga huu, ambapo wazo la watawala kuwatisha Ummah kwa nguvu ya kindoto ya jeshi hili, ili kuhalalisha kushindwa kwao kufikia suluhisho la kijeshi na kupigana na Mayahudi, liliporomoka bila kubatilishwa.

3- Ni fursa kwa watu wenye nguvu na majeshi ya Ummah wanaoona ushindi wa mtu mmoja mmoja wa mujahidina licha ya uchache wao na vifaa, wajihakiki nafsi zao na kuwanusuru ndugu zao Waislamu kutoka watu wa Gaza, ili kwamba hata mmoja wao asijute baadaye kupoteza fursa hii, kama yale yaliyotokea katika vita bandia ambayo hawakuyashuhudia kwa umbile la Kiyahudi.

4- Licha ya kuangamizwa na mashahidi, Ummah hautaki usitishaji vita, bali wanataka kupigana na Mayahudi ili kuikomboa Palestina yote kuanzia baharini hadi mtoni, wakisaidiwa na wana wao miongoni mwa majeshi ya Kiislamu ili kuwapindua wale wanaosimama katika njia ya kuelekea ushindi, katika wakati ambapo umbile la Kiyahudi linatangaza kwamba vita vitaendelea kwa miezi kadhaa na halitaki usitishaji wa mapigano, kwa hivyo majeshi ya Ummah yanangoja nini kuchukua hatua ya kuwapa Mayahudi funzo litakalowafanya kusahau minong'ono ya Shetani na kuwafukuza na walio nyuma yao?!

5- Ushujaa ambao Ummah unaushuhudia, unaofanywa na Mujahidina kwa uthabiti, subira, na ustadi wa kupigana, na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, umeimarisha kujiamini kwake na uwezo wake mkubwa, hasa kwa vile haujashuhudia mapigano ya kweli na jihad pamoja na maadui zake kwa zaidi ya karne moja.

6- Juhudi za jumuiya ya kimataifa, Magharibi mkoloni kafiri, akiungwa mkono na Marekani na Ulaya, na watawala wa Umma wa Kiarabu na wasiokuwa Waarabu, kutafuta kile kinachoitwa suluhisho la dola mbili, si chochote ila ni dhana tu na machukizo, mbwembwe za wazi, zilizokataliwa vikali na umbile la Kiyahudi lenye kiburi kwanza. Pili, halina uhalisia wa kivitendo, pamoja na kuwa ni kumsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na watu wa Palestina.

7- Aqidah ya Ummah wa Kiislamu ingali hai katika undani wake, na operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imeifasiri katika utekelezaji wa kivitendo katika hamu ya jihad na kifo cha kishahidi. Imeaminika kuwa mwenye kumnusuru Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamnusuru.

[كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللهِ]

Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. [Al-Baqarah 2:249]. Na wale wanaosimama dhidi yake ni watawala wake, vibaraka wa ukoloni, ambao wamefichuliwa na ambao uongo wao, pamoja na wafuasi wao, ni wafisadi wa ndani katika duru zao za kisiasa za kila aina.

8- Mipaka baina ya nchi za Kiislamu imechorwa na makafiri wa kikoloni maadui wa Ummah, bila ya takhsisi, na ndiyo inayozuia ushindi kwa Waislamu nchini Palestina, Gaza na nchi za Kiislamu, na ndiyo inayodumishwa na watawala wa aibu na utumwa. Lau majeshi ya Kiislamu yangekusanya zana na mali zao zilizoporwa, yangeunda kikosi kikubwa zaidi duniani ambacho kingeogopwa na maadui wote wa Mwenyezi Mungu duniani.

9- Ushindi anaoutaka Mola Mtukufu kwa Umma wa Kiislamu ni utukufu wa dini ya Kiislamu.

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawbah 9:33]. Ushindi huu, utaoukomboa Ummah kutoka kwa wakoloni na watawala vibaraka wao, na kuliondoa umbile la Kiyahudi kutoka katika mizizi yake, na kuzitoa Marekani na Ulaya kutoka katika nchi za Kiislamu, hautapatikana kivitendo isipokuwa kwa kuwepo kwa Khilafah Rashida na kusimamishwa upya kwa Njia ya Utume, baada ya kuondolewa kwake duniani miaka 103 iliyopita mikononi mwa maadui wenyewe. Ni kadhia nyeti ambayo kwayo Waislamu hushinda katika vita vyao vyote, na hata rehema na uadilifu ambao ulimwengu ulipoteza kwa kukosekana Khilafah na uongozi wake wa kifikra wa kisiasa utaregea.

Inatosha kwa Umma wa Kiislamu kuwa chini ya mataifa kwa zaidi ya miaka mia moja, ukitawaliwa na kundi la vibaraka wa Magharibi, na kumiliki itikadi ya kiwahyi ambayo huchipuza mfumo. Ulipokuwa ukitekelezwa, Ummah ulikuwa katika izza na ustawi. Hakuna katika adui yake angeshambulia hata mmoja wa raia zake, na hakuna nguvu kubwa au ndogo ambayo ingesubutu kugusa upande wake. Wakati umefika wa kuregea katika khari yake kwa kutabikisha Dini yake na kueneza ujumbe wa Uislamu katika dola kama ile aliyoiasisi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), mjini Madina.

[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللهِ]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aali Imran 3:110]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu