Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  5 Rajab 1445 Na: 1445 / 06
M.  Jumatano, 17 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hakuna Ubwana Isipokuwa katika Khilafah
(Imetafsiriwa)

Jana, Jumanne, Januari 16, 2024, Jeshi la Mapinduzi la Iran lilitangaza kwamba lilikuwa limepiga mabomu maeneo lengwa ya kigaidi nchini Syria na eneo la Iraq la Kurdistan kwa makombora ya balistiki wakati wa usiku wa manane mnamo Jumatatu, Januari 15, 2024. IRNA iliripoti kwamba Jeshi la Mapinduzi “liliharibu makao makuu ya upelelezi” na “mkusanyiko wa makundi ya kigaidi yaliyo dhidi ya Iran” huko Erbil, likielezea kwamba “ulipuaji mabomu hayo ulijiri kujibu jinai za hivi karibuni zilizofanywa na maadui”. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kikurdi, karibu makombora kumi yalishambulia zaidi ya eneo moja huko Erbil, na baadhi ya makombora haya yalishambulia nyumba ya mfanyibiashara Peshraw Dizayee wa Kampuni ya Falcon Group, ambayo inafanya kazi katika sekta za usalama, nyumba, na mafuta, na kupelekea mauaji yake na binti yake, pamoja na kujeruhiwa wengine 17, akiwemo mkewe na wanawe wawili. Vyombo vya habari vya Iran hapo awali vilimtuhumu Dizayee kwa “kuifanyaa kazi Mossad ya 'Israel' kama mshirika wa kibiashara wa 'Israel' kwa kuipatia mafuta na kuajiri wanajeshi wastaafu wa Marekani kwenye misheni za usalama.”

Wakati wa mahojiano yaliyofanywa na yeye, mnamo Jumanne, 16/01/2024 katika kongamano la Davos nchini Uswizi, Waziri Mkuu wa Iraq Muhammad Shia Al-Sudani, kulingana na tovuti ya Bloomberg ya Marekani, alilielezea shambulizi hilo kama uchokozi, na akasema: “Serikali ya Iraq ina haki yake kwa taratibu zote za kidiplomasia na kisheria zilizopewa na ubwana wake.”

Mbali na uchambuzi na nia zao, iwe madai ya Iran ni kweli, au kwamba operesheni hii ilikuja kwa idhini ya Marekani kutia shinikizo kwa umbile la Kiyahudi, ambalo ukaidi wake umezidi kwake, au kwamba kuna ukosefu wa itifaki ndani ya Jeshi la Mapinduzi na mzozo uliozuka baada ya kuuawa kwa Kamanda wa Kikosi cha Quds Qasem Soleimani, au jaribio la Tehran la kufinika kashfa yake kuu baada ya kupenya kwa huduma zake za usalama, kufikia katikati ya vifaa vyake vya nyuklia, na kuuawa kwa wanasayansi wake na umbile la Kiyahudi, ambalo hivi karibuni zaidi lilipenya eneo lake na kuua na kujeruhi mamia mnamo Jumanne, Januari 3, 2024, wakati wa ukumbusho wa Jenerali Qasem Soleimani ... Kando na yote hayo, kuna Ukweli mmoja wazi, ambao ni kwamba Iraq imepoteza ubwana juu ya ardhi, bahari, na anga yake. Makombora yaliyorushwa yalipenya anga ya Iraq kutoka kusini hadi kaskazini, na kutoka mashariki hadi magharibi!

Enyi Waislamu nchini Iraq na Nchi zengine zote za Kiislamu: Hii ndio hali ya nchi za Waislamu baada ya kuanguka kwa Khilafah na kugawanywa kwake katika vijidola, vilinavyotawaliwa na vibaraka Ruwaibidha ambao wanajali tu kuridhika kwa mabwana zao, ni nchi ambazo zimepoteza ubwana ambapo maadui zao hufanya chochote wanachotaka wakati wowote wanapotaka!

Enyi Umma wa Kiislamu: Kuweni na yakini kuwa ubwana, uhuru, na kuhifadhi mipaka hakuwezi kupatikana isipokuwa nchi zote za Waislamu ziwe ni majimbo yaliyojumuishwa ndani ya dola moja na kusimamiwa na Imam mmoja ambaye Ummah anampa Bay’ah (utiifu) kwa ridhaa na chaguo la kutawala kulingana na Sharia wa Mwenyezi Mungu, ambaye analinda mipaka, na kulazimisha mamlaka yake juu ya mipaka yote ya nchi hii, ardhi yake, anga yake, na bahari yake.

Daima tumekulinganieeni kwenye utukufu huu, na tutaendelea kukulinganieni hadi Mwenyezi Mungu afungue nyoyo zenu kufanya kazi ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, na kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu kupitia hiyo pekee uadilifu utapatikana, dhulma itazuiwa, haki zitahifadhiwa, na mizizi ya makafiri itakatwa.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu