Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  13 Jumada II 1444 Na: 1444 / 08
M.  Ijumaa, 06 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Baghdad Yazama na Serikali Inaburudika na Kucheza
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo watu wa Iraq wanaishi katika hali mbaya zaidi za maisha, na wananyimwa haki zao za kimsingi zinazohusiana na utunzaji, katika ngazi zote; kwa upande wa afya, elimu, miundombinu, ulinzi na usalama, tunaona wale wanaodhibiti shingo zao wakiburudika na kucheza, na kuandaa mashindano ya mpira wa kandanda, na ni aibu kwamba vyombo vya habari vinatoa mwanga juu ya mambo haya madogo, na kuwashughulisha watu na wale wanaohudhuria na wale ambao hawahudhurii miongoni mwa wasanii kufufua sherehe ya ufunguzi, kuvuruga saa rasmi za kazi huko Basra, na kupoteza pesa ili kufanikisha mashindano haya, bila kujali mateso ya watu hawa waliojeruhiwa. Siku mbili zilizopita, Baghdad na miji kadhaa ya Iraq ilifurika baada ya mvua kunyesha kutokana na uchakavu wa miundombinu, na licha ya maombi mengi, hakukuwa na masikio ya kusikiliza, wakati kuiandaa nchi kwa dharura kama hiyo ni mojawapo ya vipaumbele na majukumu ya mtawala, na haki ya raia juu yake, na wakati huo huo tunaiona serikali ya Iraq ikijishughulisha na uangaziaji wa vyombo vya habari wa Kombe la Ghuba, na hamu yake ya kwanza na ya mwisho ni mashindano haya na mafanikio yake!!

Enyi Waislamu: Yale tunayoyaona leo Iraq, na kabla ya hapo katika Kombe la Dunia la Qatar, vyombo vya habari kuangazia kwa namna hii ya kutia chumvi, si jambo la kawaida, bali ni sera inayofuatwa na kusomwa na maadui wa Ummah, kuufanya Ummah kuwa mjinga na kuwaourukusha kutokana na wajibu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwawekea, pamoja na kuwapora kitambulisho chao kwa njia ya kuzipigia mnada fahamu za hadhara ya Magharibi zinazolingania kuvunjika na kusambaratika. Haider Aufi, afisa katika Chama cha Soka cha Iraq, alisema, kwa mujibu wa Washington Post, kwamba "Iraq imepata msukumo kutoka kwa Qatar kuandaa Kombe la Dunia," na anaongeza: "Michezo imekuwa moja ya shughuli muhimu zaidi duniani... Tamaduni na hadhara lazima zihamishwe kupitia kuandaa michuano na mashindano, na hili ndilo tuliloshuhudia katika maandalizi ya Qatar ya Kombe la Dunia la 2022."

Enyi Waislamu: Mtume (saw) amekuongozeni kwenye mambo matukufu na amewaonya dhidi ya maovu kama katika kauli yake (saw):

 «إِنَّ اللهَ يُحِبُّ مَعَالِيَ الأُمُورِ وَأَشْرَافَهَا، وَيَكْرَهُ سَفْسَافَها»

“Hakika Mwenyezi Mungu anayapenda mambo ya juu kabisa na anachukia yaso maana”.

Mwenyezi Mungu Mtukufu hupenda kile kitakachokuleteeni heshima, hadhi na mwinuko, na anachukia mambo madogo madogo na yasiyo na maana ambayo yanaleta unyonge na udhalilifu, na hapana shaka kwamba mtu wa kwanza kujumuisha sifa hii ni mtawala. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «أَحَبُّ النَّاسِ إِلَى اللهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَدْنَاهُمْ مِنْهُ مَجْلِساً إِمَامٌ عَادِلٌ، وَأبْغَضَ النَّاسِ إِلَى اللهِ وَأَبْعَدَهُمْ مِنْهُ مَجْلِساً إِمَامٌ جَائِرٌ»Hakika mtu anayependwa zaidi na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na aliye karibu Naye kwa hadhi ni Imam (kiongozi) mwadilifu. Na mtu anayechukiwa zaidi na Mwenyezi Mungu na aliye mbali na Yeye kwa hadhi ni Imam (kiongozi) jeuri.”

Nyinyi ndio Umma mtukufu kabisa ambao Mwenyezi Mungu ameutukuza kwa Aqida (itikadi) tukufu zaidi na akakufanyeni mashahidi kwa watu, basi ni bora kwenu kuwa miongoni mwa wenye azma ya hali ya juu, malengo ya juu, na maadili ya hali ya juu, na kutii amri ya Mola wenu Mlezi kubeba wito wake na kuwaokoa wanadamu kutokana na ufisadi wa tawala na watawala.

Basi kwa yale yanayomridhia Mola wenu Mlezi, na yale yanayokuleteeni fahari na utukufu, kufanya kazi ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu, tunakulinganieni, enyi Waislamu, ili kuchora ramani ya dunia na kubainisha msimamo wa kimataifa, na kuikata mizizi ya makafiri, kwa ujumbe wa haki na rehma.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu