Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  4 Rabi' I 1445 Na: 1445 H / 06
M.  Jumanne, 19 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Hasina Haipotezi tu Pesa za Watu Pekee lakini pia Inawasaliti Waislamu kwa Kununua Ndege na Satelaiti kutoka Ufaransa, Adui Mkubwa wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Huku watu wakilipia gharama kubwa kwa janga la maambukizi ya homa ya dengue nchini, na uhaba usio wa kawaida wa vitanda katika mahospitali, ukosefu wa vifaa vya kutosha vya matibabu na hata chakula cha ziada cha maji ya saline, serikali imechukua miradi miwili mipya ya uporaji. Imetangaza kununua ndege kumi za A350 na satelaiti ya Bangabandhu-2 kutoka kwa kampuni ya Ufaransa ya Airbus. Baada ya mkutano wa nchi mbili na Sheikh Hasina, katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari mnamo Jumatatu Septemba 11, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliishukuru serikali ya Hasina kwa kuwa na imani na sekta ya ndege ya Ufaransa na kwa kuahidi kununua ndege na satelaiti kutoka kwao. Ndege na miradi ya satelaiti ni dhihaka kamili kutoka kwa watawala hawa wa kisekula hadi kwa watu. Hawajali kuhakikisha miundombinu msingi ya afya kwa watu lakini wako tayari kuweka mzigo zaidi kwa watu kwa madeni mapya zaidi. Hapo awali, Serikali ya Hasina ilizindua satelaiti ya Bangabandhu-1 kwa gharama ya Taka bilioni 30 ya pesa za watu, lakini watu wangali gizani ni kiasi gani cha pesa Bangladesh imepata kupitia mradi huu; Badala yake waliona mzigo wao wa deni umeongezeka. (Satellite ya Bangabandhu: Je! Kuna haja gani ya satelaiti ya pili wakati ya kwanza haina faida? BBC Bangla, 3 Februari, 2022).

Wakati huo huo uporaji wa miradi inayotegemea madeni ya kigeni (dolari bilioni 100) imeitumbukiza nchi ndani ya bahari ya madeni. Bado serikali ya Hasina, iliyolewa na ashiki ya uporaji, imechukua miradi mpya kutoka kwa Mwanakruseda Mkoloni Ufaransa, ambayo ina historia ndefu ya uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ufaransa iliivamia Ardhi ya Waislamu Algeria mnamo 1830 na kuwauwa na kuwachinja Waislamu bila huruma yoyote. Ufaransa ilicheza dori kubwa mnamo 1924 pamoja na Uingereza kuivunja Khilafah Uthmani. Tangu wakati huo, Ufaransa imekuwa ikiongoza vita vya kithaqafa kujenga chuki na hasira dhidi ya Uislamu. Imekuwa akichochea chuki dhidi ya Uislamu kwa kuichafua Quran Tukufu, ikionyesha katuni za kuchukiza za Charlie Hebdo katika majengo ya serikali ya Ufaransa kumtukana Rasulullah (saw) wetu mpendwa, ikipiga marufuku swala za mitaani, ikifunga shule kadhaa za kibinafsi za Kiislamu na mamia ya misikiti kote nchini Ufaransa kwa jina la kupambana na 'Uislamu wenye msimamo mkali’! Mnamo mwaka wa 2011, Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji hijab, ikiwemo burka na niqab, katika maeneo ya umma. Na chini ya uongozi wa Rais Emmanuel Macron, nchi hiyo ni adui zaidi kuliko hapo awali katika vita vyake vya kimfumo dhidi ya Uislamu. Macron hapo awali alisema kuwa 'Uislamu uko kwenye mgogoro kote ulimwenguni' na aliapa waziwazi kupigana na Uislamu na aliwaomba watu kufanya vivyo hivyo. Katika kuendeleza shambulizi hili, katika mwezi huu, serikali yake imepiga marufuku uvaaji hijab wa wasichana wa Kiislamu katika shule za Ufaransa.

Enyi Waislamu! Kihistoria, Ufaransa ni muuaji wa kikoloni wa Waislamu na mvamizi wa ardhi za Waislamu. Na vita visivyo na mwisho vya Ufaransa dhidi ya Waislamu sasa vinaongozwa na Rais wa sasa wa Ufaransa Macron, adui mkubwa wa Mwenyezi Mungu (swt) na Waislamu. Kwa hivyo, mahusiano na Ufaransa yanapaswa kuwa mahusiano ya kivita. Lakini Sheikh Hasina, ambaye utiifu wake (Al Wala) sio kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jal lakini kwa wakoloni wa makafiri, sio tu amemtandikia zulia jekundu adui wa Mwenyezi Mungu, lakini pia sasa anafuja pesa nyingi za Ummah kutimiza maslahi ya Ufaransa. Watawala hawa wa kisekula ni dhalimin (madhalimu) hawatii amri ya Mwenyezi Mungu:

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Mumtahanah, 60:9].

Enyi Waislamu! Watawala hawa wa kisekula ni funza wanyonyaji damu ambao wamezaliwa kutoka katika tumbo la Mfumo wa Kilimwengu wa Wakoloni wa Magharibi. Wapo kutumikia mabwana zao wa Magharibi wanaochukia Uislamu kwa gharama ya watu wao wenyewe. Wanapora utajiri wetu na kufuja pesa zetu kwenye miradi isiyo na maana kama kununua ndege na miradi ya satelaiti ili kufurahisha mabwana zao wa Magharibi. Hizi ndizo siasa zao ambazo mizizi yake ya kina ni ulafi, khiyana na udanganyifu. Wanajua kuwa hawawajibiki kwa watu lakini kwa wakoloni Makafiri wa Magharibi. Hivyo, wanatafuta kupata na kudumisha utawala kupitia maadui wa Mwenyezi Mungu na waumini. Kwa hivyo, lazima mujitahidi kurudisha usimamizi wa kweli wa Uislamu, Khilafah Rashida iliyoahidiwa kwa njia ya Utume, na kuwakana watawala hawa wanaoungwa mkono na Magharibi ambao wamedhaminiwa aibu na giza na Mwenyezi Siku ya Kiyama. Rasulallah (saw) amesema,

«لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لَهُ بِقَدْرِ غَدْرِهِ أَلَا وَلَا غَادِرَ أَعْظَمُ غَدْرًا مِنْ أَمِيرِ عَامَّةٍ»

“Kila msaliti atakuwa na bendera Siku ya Kiyama. Itanyanyulia kwake kwa kadiri ya khiyana yake. Jueni basi! Hakuna msaliti mkubwa kuliko mtawala anayetawala watu.” (Muslim)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu