Jumanne, 02 Rabi' al-awwal 1444 | 2022/09/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  17 Safar 1444 Na: 1444 H / 05
M.  Jumanne, 13 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kutangaza Maombolezi ya Kitaifa Juu ya Kifo cha Malkia Elizabeth II, Serikali ya Hasina Ilifichua Utiifu wake Halisi kwa Waingereza na Kusaliti Damu na Muhanga wa Watu Waliopigania Ukombozi kutoka kwa Ukoloni wa Kiingereza

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Hasina ilitangaza Maombolezi ya kitaifa ya siku tatu kutokana na kifo cha Malkia wa Uingereza Elizabeth II. Bendera ya taifa itawekwa nusu mlingoti katika mashirika yote yanayomilikiwa kikamilifi na serikali, yenye kumilikiwa nusu na serikali na mashirika huru, taasisi za elimu, majengo yasiyo ya serikali, na balozi za Bangladesh ng’ambo, kulingana na arifa iliyotolewa na Kitengo cha Baraza la Mawaziri. Pia, maombi maalum yatapangwa kwa ajili ya ‘kuutafuta wokovu’ wa roho ya mwendazake Malkia, taarifa hiyo ilisema! Hasina pia aliamua kuzuru Uingereza kutoa heshima zake kwa Malkia. Huku bado tukikumbuka ukatili wa ukoloni wa Waingereza katika ardhi za Waislamu, Sheikh Hasina hakusita kudhihirisha utiifu wake wa kweli kwa mkoloni Uingereza na ufalme wake wenye kiu ya kumwaga damu kwa tangazo kama hilo, hata kwenda kinyume na hisia za wananchi. Huu pia ni usaliti dhidi ya watu wa Bara Dogo la India ambao walipigania ukombozi kutoka kwa utawala dhalimu wa Waingereza na kujitolea damu yao dhidi ya ukoloni wa Waingereza.

Enyi Watu, mnajua, Himaya ya Uingereza ilikuwa imeindoa ngao ya Ummah - Khilafah tukufu - ambayo nyuma yake tulilindwa kutokana na maadui mwaka 1924 kwa ushirikiano wa msaliti, msekula Mustafa Kemal. Waliuondoa mfumo wa utawala wa Uislamu ambao tuliachiwa na kipenzi chetu Mtume (saw) na wakaweka mfumo wa utawala wa Kikafiri pamoja na maisha yao ya kuchukiza. Tangu wakati huo walikuwa wamewaua watu wetu, wakapora mali zetu, na kuleta mateso makubwa juu yetu kwa ukatili wao. Baada ya kuivunja Khilafah, walizigawanya ardhi zetu kwa kuegemea mipaka bandia ya utaifa ili Ummah huu kamwe usiweze kuungana tena kama dola moja yenye nguvu na kwenda kinyume na maslahi yao ya kibeberu. Kwa ujanja walichochea mifarakano ndani ya ardhi za Waislamu na wakatuingiza kwenye vita vya kimadhehebu ili tuvuje damu hadi tufe. Hasina msekula ni mithili ya kibaraka wa Uingereza - msaliti mhalifu Mustafa Kemal, ambaye anafanya kazi usiku na mchana kudumisha ukoloni wa Waingereza katika ardhi yetu na kuzuia kuibuka kwa Ukhalifa. Kwa kutangaza Maombolezi ya Kitaifa juu ya Kifo cha Malkia Elizabeth II na kufanya 'maombi maalum' kwa Malkia ambaye alikuwa alama ya Ukoloni, utawala wa Hasina unatutaka tusahau miaka 200 ya historia ya uhalifu wa bwana wake katika bara hili dogo ambayo ilianza na ushindi wao katika Vita vya Plassey (Palashi) mnamo 1757 kwa njia ya usaliti na udanganyifu.

Enyi Watu, baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Uingereza ilisema kulazimishwa kuacha ukoloni kwa jina, lakini bado inadumisha ukoloni mamboleo katika ardhi zetu kupitia watawala watumwa; Maombolezi ya serikali ya Hasina kwa Malkia ni ushahidi wa ukweli huu. Ndio maana tunaona, watumwa hawa hawaiachi nafasi yoyote ya kuonyesha utiifu kwa mabwana zao wa kikoloni wa kikafiri hata kama hilo linahitaji kwenda kinyume na fikra na hisia za watu wao wenyewe. Ukweli ni kwamba, Malkia Elizabeth II alichukua kiti cha ufalme mwaka wa 1952, mara tu baada ya Milki ya Uingereza kuondoka Bara Hindi mnamo 1947. Tangu wakati huo Elizabeth aliwatunza vibaraka wao watiifu wa Bara hili Dogo kama vile Jinnah wa Pakistan, Neheru wa India, na Sheikh Mujib wa Bangladesh kwa niaba ya Himaya yake. Akiuweka hai urithi wa mtangulizi wake, Hasina pia hapa analinda maslahi ya Waingereza, jinsi mtumwa mwaminifu anavyolinda nyumba ya bwana wake. Hivyo, Hasina hakujali kwamba kumuomboleza ‘msimamizi’ wake (Malkia Elizabeth II) kungekuwa tusi kubwa kwa Ummah. Kwa sababu kamwe hakosi kupaka chumvi kwenye kidonda cha Waislamu. Elizabeth binafsi alimtunuku Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, mhalifu wa kivita katika vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Iraq na Afghanistan, cheo cha juu zaidi cha ushujaa. Pia alimtukuza Salman Rushdie aliyelaaniwa kwa ushujaa huko nyuma mwaka wa 2007 ili kuunga mkono matusi yake kwa mpendwa wetu Rasul (saw). Hakika, Malkia Elizabeth na Mfalme wa Uingereza ni ishara ya ukoloni ambayo serikali ya baada ya ukoloni ya Uingereza inataka kuuweka hai ili kuonyesha kiburi chao. Na kwa kumuunga mkono mfalme huyu na kuashiria Malkia kama 'msimamizi wake wa kweli' (katika barua ya rambirambi), Hasina ameunga mkono bila aibu historia ya giza ya bwana wake Uingereza.

Enyi Waislamu, kila kifo ni funzo kwetu; kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth II tumejifunza kwamba watawala wa kisekula wa ardhi yetu bado wanaendeleza urithi wa ukoloni, na kile kinachoitwa uhuru si chochote bali ni fikra ya kindoto ya kutudanganya. Himaya ya Uingereza kimwili iliondoka ardhi yetu lakini bado wangali wanacheza na hatima yetu ya kisiasa na kiuchumi. Masekula wanakichukulia kifo cha Malkia kama kielelezo kilichoanguka cha umoja na utiifu lakini Waislamu ambao wanaweza kujifungamanisha na hukmu na roho ya Uislamu, kifo cha Malkia na jinsi watawala wa kisekula wanavyofanya maombolezi waliwakumbusha kwamba bado wanaishi chini ya kivuli cha wingu jeusi la ukoloni. Tunatakiwa kuondokana na kivuli hiki cheusi na kukombolewa kutoka katika makucha ya watawala na wanasiasa wa Magharibi mkoloni kwa kushiriki katika mapambano ya kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili yanaoongozwa na uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir. Ni hapo tu ndipo tutaweza kweli kukombolewa kutoka katika urithi wa ukoloni na kurudisha historia tukufu ya Umma katika dunia hii. Ummah huu unatamani kuishi chini ya kivuli cha Khilafah ambayo ndiyo mlinzi wetu na nembo yetu ya umoja. Mtume (saw) amesema,

«السُّلْطَانُ ظِلُّ اللَّهِ فِي الْأَرْضِ»

“Sultan (khalifa) ni kivuli cha Mwenyezi Mungu ardhini” (al-Bayhaqi).

 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu