Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  5 Muharram 1446 Na: 01 / 1446 H
M.  Alhamisi, 11 Julai 2024

Maoni ya Habari
Kujadili Yasiyoweza Kujihami

(Imetafsiriwa)

Baada ya juhudi zilizoratibiwa za Wazayuni zenye lengo la kukashifu sauti zinazoiunga mkono Palestina, zilizoundwa na mfululizo wa makala ya magazeti ya udaku na vipindi vya TV vinavyofafanuliwa kwa batili na dosari, ilidhihirika kwamba wengi wao hawakustahili jibu la heshima hata kidogo.

Hata hivyo, katikati ya kelele hizi, tulichagua kujihusisha na kipande cha maoni kilichochapishwa katika ‘The Australian’ na Anthony Bergin wa Uchambuzi wa Kimkakati wa Australia, kupigia debe kupambana badala ya kupiga marufuku fikra za Hizb ut Tahrir.

The Australian inajiwasilisha kama jukwaa la kujadili fikra, ikituhimiza kuwasilisha majibu yetu. Licha ya shauku ya awali ya wahariri, na kinyume na maadili yao yaliyotangazwa, tuliona ukosefu wa shauku ya kuchapisha kipande chetu. Hii inatofautiana sana na uchapishaji wa mara kwa mara, uliofuata, wa makala nyingi za chuki dhidi ya Uislamu zilizofuata, mara nyingi zikiruhusu muda mfupi wa jibu la mada. Kwa ajili ya hivi sasa na kurekodi, tunasambaza kipande chetu hapa chini.

__________________________________

Kujadili Yasiyoweza Kujihami

Iwapo fikra zitapambanishwa, Hizb ut Tahrir yote iko ndani. Lakini mkono mmoja ulionyooshwa kwenye mjadala huku mwingine ukiwa na tishio la “kupigwa marufuku” unazungumzia tu ukosefu wa usalama wa mwenye usalama.

Mnamo Juni 28, gazeti la ‘The Australian’ lilichapisha ufafanuzi wa Anthony Bergin, ukipendekeza, miongoni mwa mambo mengine, “Hizb ut Tahrir itakuwa tu tishio kubwa kwa njia yetu ya maisha ikiwa tutapoteza vita vya mawazo.”

Kilimwenguni, Waislamu hawajanunua mafuta ya nyoka ya mfumo wa Magharibi wala madai yake matakatifu kwa maadili ya kiliberali. Tunajua tu manufaa ya kisiasa, ambayo yametungwa moja kwa moja au kupitia mataifa yanayofuata kandamizi, ambayo hayajaleta chochote isipokuwa kukosekana kwa utulivu katika ulimwengu wa Kiislamu. Haishangazi Waislamu kutamani nguvu ya kisiasa inayowaunganisha, ambayo ni mwakilishi wa kweli wa imani zao, inayotanguliza utulivu wa kisiasa na kiuchumi.

Ni ndani ya orodha ya jinai za Magharibi ambapo kukaliwa kwa mabavu Palestina kunaingia kwenye vita. Sio suala tata kama wengine wangependa uamini; kila binadamu mwenye staha anaweza kuitambua jinsi ilivyo. Palestina ni ardhi inayokaliwa kwa mabavu, iliyoibwa na Waingereza, na kukabidhiwa kwa Wazayuni ili waanzishe nchi ya Kiyahudi, yote kwa ajili ya kutimiza malengo ya kifalme ya Uingereza. Tofauti pekee leo ni dori ya Uingereza imebadilishwa na Marekani.

Upinzani dhidi umbile hilo la Kizayuni ulifanywa kuwa ni jinai wakati wa kuasisiwa kwake na katika miongo yote iliyofuata. Watu walipoteza maisha yao, nyumba zao na uhuru wao kwa kuchukua msimamo wa kanuni dhidi ya uvamizi, bila kujali msimamo huo. Hakujawahi kuwa na tofauti kati ya upinzani wa kisiasa na kijeshi chini ya uvamizi, na sasa kuanguka kwa makundi haya mawili kunachezwa katika nchi za Magharibi.

Majibu ya kizembe ya kupinga uvamizi wa Kizayuni ni yale ambayo yanaulinganisha na ukatili dhidi ya Mayahudi. Mashtaka ya chuki dhidi ya Mayahudi hutumika tu kuweka upya upinzani dhidi ya uvamizi kama uchokozi. Ili kuwa wazi, umbile la Kizayuni linapingwa nchini Palestina sio kwa sababu ni Mayahudi, lakini kwa sababu ni wavamizi.

Vyovyote iwavyo, suala la uhalali au maisha marefu ya umbile linalokalia kimabavu kwa kiasi kikubwa halina maana, kwani mabadiliko katika masuala mapana ya siasa za kieneo yamewalazimu watunga sera - wakiwa pamoja na wale walio ndani ya uvamizi huo - tayari kujiandaa kwa ajili ya Mashariki ya Kati ya baada ya “Israeli”.

Mazungumzo ya marufuku nchini Australia yanaibuka kwa sababu ya kukosekana kwa hoja yoyote ya kulazimisha ambayo inaweza kutoa uhalali wa uvamizi huo – waziwazi, kwa sababu hakuna yoyote. Kwa hivyo, kinyume na dhana ya ushiriki wa kiliberali, fikra hazikabiliwi kwa fikra, bali kwa jitihada za kisiasa zinazolenga kunyamazisha au kufanya upinzani kuwa uhalifu. Ikiwa Waislamu watapigwa vita kwa fikra, nchi za Magharibi zitapoteza nafasi kubwa.

Ili kuhalalisha masuala ya kupiga marufuku, tuhuma za uwongo za vurugu zinatolewa kwa urahisi. Lakini kwa sababu Hizb ut Tahrir inajulikana duniani kote kwa kazi yake isiyo ya vurugu, kigawanyo cha ‘vurugu’ lazima kichorwe upya kwa ubunifu, tena, zaidi ya uliokwisha kuwa nayo chini ya sheria iliyopo ya kupambana na ugaidi, ili sasa ijumuishe uelezaji tu wa msimamo wa kisiasa wa mtu. Mtazamo ulioungwa mkono na Anthony Bergin tangu angalau mwaka 2007, alipokubali katika karatasi yenye kichwa ‘Kujibu Itikadi ya Uislamu Mkali - kesi ya Hizb ut Tahrir Australia’, kwamba kazi ya Hizb ut Tahrir haivunji sheria yoyote, lakini badala ya kukubali sisi sote tunafanya kazi chini ya kiwango kimoja cha kisheria, alipendekeza kutungwa kwa sheria mpya iliyoundwa kwa uwazi ili kuharamisha fikra ambazo hakubaliani nazo.

Tukizungumza juu ya dhana, msimamo wa udanganyifu na unafiki wa kimakusudi unaochukuliwa na dola za Magharibi unahitaji uchunguzi wa kina. Madai ya unyanyasaji yanayoelekezwa kwa mashirika yanakabiliwa na marufuku zilizopendekezwa, ilhali vurugu halisi ya idadi ya maovu ya kihistoria hutuzwa. Msimamo unaotaka kugeuza uvamizi usio halali umekithiri, lakini uvamizi halisi - uliosisitizwa na kutambulika kimataifa - unaweza kudumishwa kwa kudumu. Kutoa wito kwa Palestina kuwa huru kuanzia mtoni hadi baharini ni chuki dhidi ya Mayahudi, lakini eneo ambalo limeporwa na umbile linalokalia kwa mabavu - na linaloenea kutoka mtoni hadi baharini - ni uhalisia wa kisiasa unaokubalika kabisa.

Mjadala mkali wa kifikra, haswa wa aina isiyofurahisha, unakaribishwa na Waislamu wote. Tuna historia ndefu na ya kujivunia isiyo ya kisekula ya kukabiliana na fikra na kuweka ukweli usioridhisha. Hatuhitaji kuthibitisha nafsi zetu au kuhalalisha misimamo yetu, lakini tuko tayari na tunaweza kufanya hivyo kwa ari ya mazungumzo ya kikweli. Ulimwengu wa Magharibi ndio ambao lazima uhalalishe kutazama mauaji ya halaiki yakitokea kwa wakati halisi. Kulazimika kujibu msimamo kama huo wa kulaaniwa ndio shitaka lenyewe.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu