Tunataka Haki kwa Mahabusu Sio Ahadi za Kilaghai Ambazo Kamwe Hazitekelezwi
- Imepeperushwa katika Tanzania
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mahakama kwa mara nyingine imewabwaga chini ndugu zetu: Ust Ramadhan Moshi Kakoso (45), Waziri Mkaliaganda (37) na Omar Salum Bumbo (55) wanachama wa Hizb ut Tahrir Tanzania ambao walitekwa, wakabambikiwa kesi ya ‘ugaidi’ na bado wako kizuizini kwa miaka minne na nusu sasa kwa kisingizio cha ‘uchunguzi unaendelea’ huku wakinyimwa haki zao za msingi kama kutembelewa na ndugu zao na kuletewa chakula cha nje ya mahabusu.