Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  26 Jumada II 1440 Na: 1440/021
M.  Jumapili, 03 Machi 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kumbukumbu ya 98 ya Kuvunjwa kwa Khilafah
Khilafah ni Radhi ya Mola Wenu, Ni Izza Yenu na Mafanikio Yenu

(Imetafsiriwa)

Tarehe ishirini na nane ya mwezi Mtukufu wa Rajab, ndio kumbukumbu ya ukumbusho mchungu, na janga kuu lililowaangukia Waislamu. Ni kumbukumbu ya kuvunjwa Khilafah Uthmaniya kupitia mhalifu wa Kiyahudi Mustafa Kamal kwa usaidizi wa Waingereza.

Mnamo tarehe ishirini na nane Rajab, mwaka wa 1342 H, ikiafikiana na tarehe 3 Machi 1924, dola ya Khilafah, alama ya izza ya Waislamu, ilivunjwa. Lilikuwa ni jukumu la Waislamu wakati huo, kusimama na kuiregesha kwa nguvu ya upanga. Si ruhusa kwa Waislamu kuishi pasi na Khilafah kwa zaidi ya siku tatu. Ni miaka tisini na nane sasa na Shari’ah ya Mwenyezi Mungu imeondolewa na mpangilio wa maisha wa Khilafah umekosekana, na ushahidi wetu kwa wanadamu umeondolewa. Ni miaka tisiini na nane sasa na Waislamu wanateseka chini ya mateso ya urasilimali.

Katika kipindi hiki kirefu, Waislamu wamekabiliwa na aina zote za madhila; hali ya Ummah wa Kiislamu leo iko wazi kwa kila mtu: umegawanyika, mnyonge, umeshindwa, umetawaliwa, umekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, rasilimali zake zinafujwa, nguvu zake imedhoofishwa, ubwana wake na uongozi wake umekosekana, unashikilia mkia nyuma ya mataifa yote, watawala wake ni watumwa wa dola za kikoloni za Kimagharibi, hawana nguvu na wameshindwa. Ummah haukuunganishwa pamoja na Kiongozi mmoja na hauongozwi na majeshi jasiri, haukuunganishwa na dola moja, ni maiti na dhaifu, ukiwaomba makafiri “makombo” ya rizki, licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ameubariki kwa hazina zote duniani, na unabeba itikadi ya “La Ilaha Illa Allah”, mikononi mwake ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Muhammad (saw), na haukukosa idadi wa ala.   

Wallahi inavunja moyo kuona kuwa Ummah huu wa Kiislamu unaishi maisha ya ng’ombe, chini ya kanuni za Kikafiri na nidhamu zake fisidifu zilizotungwa na wanadamu zinazotekelezwa na watawala watumwa wanao sababisha hali chungu ya maisha na madhila kwa watu kwa kuondoa hukumu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutupilia mbali Sunnah za Mtume wake.

Haya ndiyo yanayojiri katika Ummah wa Kiislamu kutokana na majanga na ugumu wa maisha, hii ni kwa sababu pekee ya kubeba kwake fahamu na sera fisidifu batili za kikafiri, na kutupilia mbali silaha kuu itakayo regesha nguvu, izza na mamlaka yake: mfumo wa Kiislamu pamoja na itikadi, fikra, fahamu na sera yake.

Enyi Ummah bora mulioletwa kwa wanadamu, Enyi mashahidi juu ya watu; Mwenyezi Mungu ametumiliza Manabii na Mitume, kila mmoja kwa watu wake kabla ya Nabii Muhammad (saw). Walibeba ulinganizi wa Mwenyezi Mungu kwao na watatoa ushahidi kwa ajili yao Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu (swt) asema: 

(وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطاً لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيداً)

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Ummah wa kati na kati ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu.” [Al-Baqara: 143]

Enyi Ummah adilifu, Enyi Ummah wa haki, je hamuna fahari kuwa Mwenyezi Mungu  amewachagua nyinyi kuwa wabebaji ulinganizi wake kwa watu. Mithili ya Nabii Muhammad (saw)? Je, haitoshi kwenu nyinyi kuwa na fahari kuwa mashahidi juu ya wanadamu? Je, hamuna fahari kuwa Mola wenu amewakirimu nyinyi kwa kuwaweka daraja sawa kama mitume katika ubebaji ulinganizi huu? Je, hamuna fahari kuwa mitume na malaika watakuwa na wivu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwenu?

Vipi basi munapotoka katika njia hii? Vipi munakataa kubeba ulinganizi huu wakati hii ni risala yenu?! Vipi munalala na Mola wenu ameangaza njia kwenu kwa Dini hii yenye thamani, isiyochafuliwa na batili yoyote?

Maanswari wa Dini hii, wasaidizi (Hawaris) wa zama hizi, muko wapi? Ni nani atakaye inusuru Dini hii? Ni nani atakaye uleta Uislamu katika utekelezwaji? Ni nani atakaye wasaidia wajane? Ni nani atakaye simamia watoto mayatima? Ni nani atakaye simama kwa ajili ya waliokufa na majeruhi, kwa ajili ya Palestina iliyo vamiwa, kwa ajili ya Al-Aqsa, kwa ajili ya miti na mawe?  

Tangu kutoweka kwa jua la Uislamu, kupitia kutoweka dola ya Khilafah, hali yenu kama muionavyo haihitaji ufafanuzi, mumepoteza dira yenu, hivyo basi dau lenu lilipotea baharini, na kupiga pondo zaidi hakutawasaidia, makafiri wanadhibiti muelekeo wenu, kwa usaidizi wa watawala wajinga (Ruwaibidhah), wanao wasalimisheni kwao, mithili ya kondoo kwa mchinjaji wao. Wamewaadhibu kwa adhabu kali zaidi, wamewachinja vijana na wanawake wenu, na kufuja mali zenu. Watawala hawa wameiuza Akhera yao kwa Dunia ya wengine. Hawaheshimu kizazi wala mikataba walio nayo kwa waumini. Vipi munavumilia madhila haya na fedheha na hasara hii?

Tangu kuvunjwa kwa dola ya Khilafah tumekuwa wanyonge, je wakati haujawadia kwa vijana wa Ummah huu bora kuuokoa Ummah wao? Je, wakati haujawadia kwa kizazi cha Khalid, Salahuddin na Abu Ubaida kuregesha utukufu wa mababu zao watukufu kupitia kusimamisha Khilafah itakayokomboa biladi na watu, itakayosimamisha Dini hii, kulinda heshima?

Ndio, Wallahi sasa ndio wakati au vyenginevyo ni nani atakaye wasaidia Waislamu leo mashariki na magharibi isipokuwa Khilafah?

Waambieni makafiri kuwa Khilafah ndio kadhia yetu nyeti, ima tuwe na Khilafah au tufe. Hatutaachana na ubebaji ulinganizi huu kwa gharama yoyote ile. Waambieni: Wallahi lau watakita nguzo kubwa kabisa ili tuachane na kazi ya Khilafah, hatutaiwacha hadi Mwenyezi Mungu aisimamishe au tufe bila yake. Hatutakuwa kama wana wa Israel ambao walilaaniwa. Na kamwe hatutapoteza maono ya jukumu letu baada ya leo, tumeijua njia na kupata dira katika Kitabu cha Mola wetu na Sunnah za Mtume wetu (saw), tutaregesha izza ya Ummah huu na fahari yake, tutasimamisha Khilafah yetu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Khilafah itasimamishwa na itaeneza uadilifu wake na itatimiza haki na kubeba kheri kwa wanadamu wote.    

Sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunawaalika kushiriki katika amali za kumbukumbu ya kuangushwa Khilafah zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir katika Wilaya na maeneo tofauti tofauti, ili kuhamasisha Ummah kufanya kazi nasi ili kuregesha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wake (saw).

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mulio amini, muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume pindi wanapokuiteni kwa lile linalokupeni uhai. Na jueni kuwa hakika Mwenyezi Mungu anazunguka kati ya mtu na moyo wake na hakika kwake Yeye mutakusanywa” [Al-Anfal: 24]

 

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu