Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  16 Rajab 1441 Na: 1441/09
M.  Jumatano, 11 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jamhuri, Demokrasia na Chaguzi za Kidemokrasia Zimeshindwa Nchini Afghanistan; Muendelezo wowote wa Juhudi hii itakuwa ni marudio ya jaribio hili lililoshindikana

(Imetafsiriwa)

Baada ya miezi sita ya machafuko ya uchaguzi juu ya matokeo yake, wagombea wawili wa mbele waliapishwa kama maraisi wa Afghanistan katika sherehe tofauti za kiapo. Wote wameuita ushindi wao kama "ushindi wa Jam huri na Demokrasia".

Siku zote tumewakumbusha Waislamu na watu Mujahid wa Afghanistan kuhusu matokeo yasiyotakikana na mabaya ambayo yanatarajiwa kutokana na michakato ya kidemokrasia na inayoongozwa na Amerika. Kwa mfano, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari iliyopewa jina la “Chaguzi za Kidemokrasia Zimeipelekea Afghanistan katika Mgogoro Mkubwa wa Kisiasa” iliyochapishwa mnamo 28 Septemba 2019, tulitaja kuwa “Uchaguzi wa Urais nchini Afghanistan huwa kama kaa la moto ambalo lenyewe ndani yake lina miale kwa majanga ya kisiasa ya ndani ambayo karibuni yatahisika na watu wa Afghanistan baada ya kuanza kuchoma mifupa na miili yao kwa njia ile ile kama walivyofanya katika uchaguzi wa 2009, 2014 na 2018.”

Baada ya kupuunzwa kwa tahadhari na ushauri wa kikundi cha Waislamu walio thabiti na wenye kutambua, watu wa Afghanistan sasa wanashudia watu wawili wakiapa kama marais. Wakati wote wawili waliapa na Qur’an tukufu, badala ya kujitolea kwa utekelezaji wake, kulinda hadhi yake na neema, wote ni watiifu kwa Amerika na wamejitolea kuitekeleza demokrasia na katiba zao zisizokuwa za Kiislamu. Inaonekana kabisa kutokana na kutangaza kujitolea kwao kutekeleza michakato ya amani ya Amerika nchini Afghanistan. Kwa kuwa Afghanistan haina kiongozi wa kweli wa kisiasa, kila kitu chamalizikia kuwa ni msaada kwa maslahi ya Amerika.

Hata hivyo, kinachovutia zaidi kutambua, japokuwa, ni kweli kuwa baada ya Ukomunisti, ni Jamhuri, demokrasia na maadili yote yaliyowekwa pamoja na chaguzi zao za kidemokrasia ambazo zimeshindwa na kudharauliwa nchini Afghanistan. Ni kwa sababu ya ukweli kwamba maadili yao yote yanapingana na imani ambazo ni muhimu kwa watu wa Afghanistan, kwa sababu ambayo maadili kama hayo hayataweza kukita mizizi katika jamii ya Afghanistan. Kwa hivyo, wanaelekea kutumia nguvu ya jeshi na njama kutekeleza maadili yao kwa muda mfupi juu ya watu hawa adhimu, haijalishi wanaweza kuwa dhaifu jinsi gani. Matokeo yake ambayo ni kuleta mgogoro wa kisiasa na machafuko.

Kwa hivyo, kupokea msaada kutoka kwa wavamizi Waamerika, wanasiasa duni wamewadandia Waislamu wa Afghanistan, ambao wamepata shida ya kila aina ya udhalimu huko nyuma kutoka kwa kila mvamizi anayejulikana katika historia ya hivi karibuni, na kupoteza hisia zao, nguvu na damu kwa njia ya kutamausha.

Watu wa Afghanistan lazima wajue kuwa uovu unawasubiri kila moja na kila mfuasi wa hatua ambazo zinaongoza kwa utekelezaji wa maamuzi ya Amerika, ajenda za kisiasa na wanasiasa wao vibaraka. Wema tu wanaotarajia kupokea katika maisha haya na baadaye, uko tu katika kuifufua nidhamu ya Kiislamu, fikra na maadili kupitia kuisimamisha tena Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu