Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  23 Rabi' II 1446 Na: Afg. 1446 H / 10
M.  Jumamosi, 26 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Makala ya Hivi Punde ya New York Times ni Mfano Mwingine wa Mkakati wa Kugawanya wa Marekani Miongoni mwa Mujahidina wa Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Mnamo Oktoba 24, The New York Times ilichapisha makala kutokana na mahojiano na Waziri wa Mambo ya Ndani wa sasa wa Afghanistan, ikiwa ni pamoja na moja yenye kichwa, “Je, Mwanamgambo Aliyetafutwa Zaidi Afghanistan Sasa Ni Tumaini Lake Bora la Mabadiliko?” Makala hizi zinalenga kuleta mgawanyiko na kuwaelekeza baadhi ya Mujahidina katika maslahi ya Marekani.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan hapo awali ilitahadharisha kuhusu sera kama hizo za Marekani na Magharibi. Mapema mwaka wa 2023, Hizb ilifanya kampeni iliyopewa jina la “Simulizi Mpya na Hatari ya Magharibi Dhidi ya Mujahidina,” ikiangazia mkakati hadaifu wa Marekani wa kuwagawanya Mujahidina katika “Taliban yenye msimamo mkali” na “Taliban yenye msimamo wa kati na kati.” Waraka wenye kurasa 11 pia ulisambazwa ana kwa ana, ukielezea jinsi vyombo vya habari vya Magharibi na wasomi wa kifikra hufuata mkakati huu wa mgawanyiko.

Marekani inauona umoja wa Mujahidina wa Afghanistan kama kikwazo kwa ushawishi wake wa kisiasa, kijasusi na kimfumo. Kwa hivyo, inatafuta kuwagawanya kuwa “Taliban mbaya na yenye msimamo mkali” na “Taliban nzuri na yenye msimamo wa kati na kati,” wakishirikiana na “Taliban yenye msimamo wa kati na kati,” ambao Marekani inawaona kuwa “wa kawaida na wazuri.” Makala hayo ya New York Times pia yanatumia lugha ya kutia motisha ili kushajiisha ushirikishwaji mkubwa na watu fulani, na kuwaita “wenye busara” na “wa wastani.”

Maneno yanayotumiwa na wanasiasa wa Magharibi na vyombo vya habari kwa mamlaka za serikali inayotawala kamwe hayajawahi kuwa rahisi au yasiyo na maana - nyuma ya maneno haya kuna ajenda muhimu ya kisiasa. Dola za kikoloni kihistoria zimegawanya makundi chini ya lebo mbalimbali kwa kuunda vitambulisho vya uongo kwa kila moja ili kuimarisha utawala wao. Lengo ni awali kupanda mbegu ya mgawanyiko katika akili za watu na kufungua njia kwa ajili ya hatimaye ‘mizozo na kupigania madaraka’. Mbinu hii ni mfano wa wazi wa sera maarufu ya “gawanya na utawala”.

Wakati wa Vita Baridi, Marekani ilitumia mbinu hii kutofautisha makundi ya kikomunisti “ya wastani” na “yenye msimamo mkali”, wakitaka kushirikiana na “viongozi wa wastani” katika nchi za kikomunisti ili kukabiliana na ushawishi wa Usovieti. Mkakati huu pia ulitumika dhidi ya Mujahidina nchini Palestina, Syria, na Afghanistan wakati wa Usovieti, wakiwagawanya katika “watu wa wastani” na “wenye msimamo mkali,” kudhoofisha na kupotoa ajenda yao ya Kiislamu kwa kushirikiana na wale wenye msimamo wa wastani.

Tunafahamu kwamba hakuna mwanajihadi anayeunga mkono mgawanyiko, lakini ni muhimu kuwa macho dhidi ya ajenda za Magharibi na kuziepuka. Nchi za Magharibi zinajishughulisha na kudekeza na zinalenga kuwafanya Mujahidina kufanya vivyo hivyo. Wanalenga watu fulani, wakiwaona kama madaraja kati ya Afghanistan na Magharibi, wakizingatia watu hao kuwa “tumaini bora zaidi la mabadiliko.” Hata hivyo, Hizb ut Tahrir/Wilayah Afghanistan, bila ya kumuidhinisha na/au kumtakasa mtu yeyote (Tazkia), inachukulia kwamba baadhi ya viongozi wa Mujahidina, kwa uaminifu wao, wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kimsingi—mabadiliko ambayo yangepelekea kuanzishwa kwa Khilafah ya Rashida ya Pili kwa njia ya Utume, utabikishaji kamili wa Uislamu, kueneza Uislamu kote duniani, na kuunganisha Ummah.

[فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ]

“Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, Mtapitapi, apitaye akifitini, Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi.” [Al-Qalam:8-12]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu