Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa Nini Wafungwa wa Kisiasa wa Zamani Wanakamatwa Tena?

(Imetafsiriwa)

Leo, raia 23 wanahukumiwa huko Tashkent, kila mmoja wa hawa Mashababu (wanaume) alikuwa amefungwa gerezani wakati wa enzi ya dhalimu Karimov na alibaki gerezani hadi kifo chake. Walihukumiwa mnamo mwaka 1999-2000 kwa uanachama wao katika Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislamu. Walikuwa na vifungo vya ziada viliyoongezwa mara kadhaa wakiwa kizuizini, wakivumilia hali ngumu sana kwa miaka 20 au zaidi. Katika kipindi hicho, kutokana na kukamatwa kwa watu wengi mwaka 1999, maelfu ya wabebaji da’wah wanaume na wanawake kutoka maeneo mbalimbali nchini Uzbekistan walikamatwa. Katika miaka hiyo ya giza, na kwa sababu ya mateso yaliyopelekea kwenye mauaji, kupigwa gerezani, na hali mbaya sana zisizo za kibinadamu, miili ya mamia ya ndugu zetu ilirudishwa kwa familia zao. Miili yao, iliyojaa michubuko, ilisimulia kimya kimya hadithi ya kutisha ya mateso ndani ya korokoro. Miili ya ndugu zetu waliouawa kwa kuchomwa na maji yaliyokuwa yakichemka, kung’olewa kucha zao, vifua vyao kupasuliwa wazi, na kuachwa makwao maiti zao zikiwa nyeusi kutokana na kupigwa, ziliatua nyoyo za familia za wazazi na watoto wao.

Na wakati Mirziyoyev, ambaye aliingia madarakani baada ya kifo kibaya cha dhalimu Karimov, alipoanza kuwaachilia huru Mashababu wa Hizb ut Tahrir waliokuwa gerezani baada ya hukumu zao kuisha, ilionekana kana kwamba furaha iliregea kwenye nyumba za waliodhulumiwa. Lakini furaha hii ilikuwa ya muda mfupi, kwani Mirziyoyev alikubali maagizo ya wakoloni kama Urusi na ushauri wa magenge ya wasaliti yaliyomzunguka, akianzisha tena mashini ya ukandamizaji ya mwalimu wake Karimov. Uchunguzi, mauaji, mateso, na kukamatwa tena katika vituo vya uzuizini yalianza kuongezeka. Wakati wa uchunguzi huo, shinikizo liliongezeka, na baadhi ya ndugu zetu waliotajwa hapo juu walilazimika kutia sahihi ungamo kwa vitisho vya kubakwa wake zao na kukamatwa kwa watoto wao.

Vijana 23 wanaoshtakiwa kwa sasa huko Tashkent wote wamekuwa gerezani kwa zaidi ya miaka ishirini na hawajaregea kwa familia zao kwa muda mrefu. Ni wanaume mashujaa wa zama zetu waliotaka kufuata Dini yetu kikamilifu, hawakukaa kimya mbele ya ukandamizaji, na kisha wakatuhumiwa kwa sababu ya fikra na imani zao, wakistahamili karibu robo karne ya mateso yasiyo ya kibinadamu kizuizini. Ikumbukwe kuwa hawa Mashababu hawana uhusiano wowote na ugaidi. Mashtaka dhidi yao sasa hayana tofauti na yale yaliyoletwa dhidi yao mwaka 1999. Hakuna hata mmoja wao anayehusika na uhalifu ulioainishwa katika Kifungu cha 159 na 244 cha Kanuni ya Kitaifa ya Adhabu; hawakuzuia shughuli za mamlaka za kikatiba wala kujaribu kupindua mfumo wa katiba kwa nguvu. Wanaamini kwamba watu wote wa dunia, wakiwemo watu wa Uzbekistan, watapata furaha na ustawi ikiwa tu wataishi kulingana na mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imani na ukinaifu kama huo haimaanishi jaribio la kupindua kwa nguvu au kuharibu utaratibu wa kikatiba! Ama kuhusu kitendo cha kigaidi kilichotokea Tashkent mnamo Februari 16, 1999, ni suala jengine kabisa, na Hizb ut Tahrir ya kisiasa haina uhusiano wowote na vitendo kama hivyo. Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha kilimwengu, na njia yake ya kufikia lengo lake inafuata tu mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa.

Na sasa, tukiregea katika tuhma za utawala wa Uzbekistan dhidi ya Mashababu, hakuna hata moja ya tuhuma hizi iliyothibitishwa katika uchunguzi. Mashtaka ya “kupindua mfumo wa kikatiba...” ni uzushi tu, kama ilivyokuwa wakati wa utawala uliopita. Ili kuthibitisha hili, inatosha kuangalia programu za kimfumo na vitabu vya kifikra na kisiasa vya Hizb ut Tahrir, pamoja na kauli zilizotolewa na Mashababu wakati wa uchunguzi. La kusikitisha, serikali haijafanya uchunguzi huo usio na upendeleo kwa robo ya karne, na inaonekana kutokuwa na uwezekano kwamba itafanya hivyo katika siku zijazo. Kwa hiyo, inaweza kusemwa kwamba mamlaka za sasa hivi leo zinapigana dhidi ya wale wanaoamini kuishi kwa mujibu wa mfumo wa Kiislamu, wakifuata nyayo za watawala wajinga katika historia. Mlango ulio wazi wa uasherati leo, unaoenea kama tauni katika nchi za Kiislamu, ni ushahidi wa wazi wa ukweli huu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu. Zaidi ya hayo, aina mbalimbali za kupigana dhidi ya wema na matendo mema yaliyoamrishwa na Dini yetu ni ushahidi kwamba serikali inayotutawala pia iko upande huu.

Je, ina maana gani kwa rais kuwaacha huru vijana hawa walio na msimamo thabiti katika fikra zao kutoka magerezani baada ya kumalizika kwa vifungo vyao, na baada ya miaka mingi kuwarudisha gerezani kwa sababu ya fikra na maoni hayo?! Mashababu hawa ni watetezi tu wa  kheri (khair) kwa watu wetu na ardhi yetu, sio waharibifu hata kidogo. Ikumbukwe kuwa, vitendo vya utawala wa Uzbekistan hivi leo vinatazamwa na kujadiliwa na Waislamu kote duniani...

Sisi katika Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa, tunatoa wito kwa serikali ya Uzbekistan kujiepusha na kurudia ukatili huo. Kwa mara nyengine tena tunaonya dhidi ya kutekeleza mauaji mapya sawa na yale yaliyotokea chini ya utawala wa Karimov mwaka wa 1999. Uhalifu huu utapelekea serikali kuwekewa doa baya zaidi katika kurasa za historia. Komesha kuwakandamiza watu wema wa Uzbekistan! Waacheni huru wafungwa! Acheni kushambulia na kutesa watu wema na waongofu katika nchi yetu! Msiwarudishe gerezani wale watu wasafi na wacha Mungu ambao muliwatesa na kuwafunga kwa zaidi ya miaka ishirini ya maisha yao!

#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД

#PleaFromUzbekistan

#صرخة_من_أوزبيكستان

H. 29 Dhu al-Hijjah 1445
M. : Ijumaa, 05 Julai 2024

Hizb-ut-Tahrir
Uzbekistan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Barua kwa Raisi wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu