Jumanne, 05 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa ya Hizb ut Tahrir / Ukraine Kuhusiana na Matokeo ya Hivi Majuzi ndani ya Crimea

 (Imetafsiriwa)

Mnamo 27 Februari, majumba ya serikali yalivamiwa na watu wasiojulikana. Wanajeshi wa Urusi wanatembea huru ndani ya peninsula na ripoti zinaendelea kuwasili kuhusu uvamizi wa kijeshi na kiraia katika makao makuu na mfano wake. Mnamo Februari 28, mwanachama wa Bunge la Ukraine Jenerali. Gennadiy Mascal alisema kwamba Hizb ut Tahrir, iliongoza na kuungwa mkono na Urusi inalenga kutekeleza mashambulizi ya kijeshi ili kuihalalishia Urusi kuivamia Crimea. Kiongozi wa harakati ya Milli Firka Wasfi Abdul Rahimov alisema kwamba Hizb ut Tahrir ilishiriki katika mapigano yaliyotokea mnamo Februari 26. Vyombo vya habari vilichapisha ripoti kwamba mkuu wa ujasusi mpya ndani ya Crimea Peter Zeemi ametangaza vita dhidi ya shirika la kigaidi la Hizb ut Tahrir ambalo limepigwa marufuku ndani ya nchi nyingi duniani.

Hatimaye, Hizb ut Tahrir / Ukraine inatangaza wazi yafuatayo:

1. Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa, hakitumii nguvu katika njia yake; hakijawahi kutumia nguvu ndani ya miaka 60 ya kazi zake pamoja na kufanyakazi ndani ya Ukraine kwa miaka 20. Chama kimepigwa marufuku ndani ya nchi za kidikteta za kidhalimu za kiuhalifu; kazi ya Hizb ut Tahrir ndani ya Ukraine ni kuwajenga na kuwaelimisha watu juu ya Uislamu.

2. Hizb ut Tahrir haina mahusiano ya mzozo wa kimadaraka ndani ya Crimea na Ukraine, hii ndio maana hatuhusiki na upande wowote; hii inajumuisha matukio ya hivi majuzi.

3. Matukio ya hivi majuzi ni ya kiuchokozi ya Urusi kwa serikali mpya ya Ukraine, ambapo Ukraine imekuwa mateka ndani ya mikono ya pande husika tatu nazo ni Urusi, Ulaya na Amerika ambao wote wanajali maslahi yao tu na maisha ya watu hayana thamani kwao.

4. Ulinzi wa umoja na uhuru wa dola unabakia kwa serikali na taasisi zake na sio watu binafsi.

5. Ulinzi wa maisha, hadhi na utajiri wa watu, hakuna shaka dola imefeli kufanya hivyo, ni haki ya mtu binafsi iliyodhaminiwa na Shari’ah, desturi, akili na sheria na nidhamu zote. Tunamatumaini kwamba hatutofikia katika hatua hii.

6. Tunaona uwezekano wa kiuchochezi kufanyika, ima ni mashambulizi juu ya vikosi vya usalama au raia na watu wasiojulikana na kisha kulaumiwa Hizb ut Tahrir ili kuhalalisha uwepo wa Urusi ndani ya Crimea. Tunapinga waziwazi yote haya mapema na lau na kama yatatokea basi tutawahesabu wale watakaoivamia Crimea.

 

H. 1 Jumada I 1435
M. : Jumapili, 02 Machi 2014

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu