Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ujumbe Maalum ya Idd ul-Fitr

Hakika mwezi wa baraka umemalizika hivi punde na Mwenyezi Mungu (swt) ameitunuku siku hii ya Idd ul-Fitr maalumu kwa Ummah wa Muhammad (saw). Katika msimu wa sherehe hii, sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania tunawapongeza Waislamu nchini Tanzania haswa na ulimwengu mzima kwa jumla, na kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuzikubali saumu zetu, visimamo (Qiyaam) vyetu na Dua zetu. Hakika Yeye ndiye Mwingi wa kusikia na Mwenye kujibu Dua zetu.

Enyi Waislamu:

Katika mwezi wote wa Ramadhani tumewaona mukijitolea kwa kipimo cha halal na haram katika vitendo vyenu, makini katika saumu, visimamo (qiyaam), sadaka na kujizuia nafsi zenu na machafu, na pia tumewaona katika hali ya kujitolea kwa ikhlasi katika Uislamu … Yote haya ni kheri, lakini kujitolea kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiweka mbali na makatazo yake haikufungika tu katika Mwezi wa Ramadhani pekee. Bali ni wajibu katika mwaka mzima na haikufungika katika vitendo vya ibada, bali inajumuisha nyanja zote za maisha; swala ni sawa na biashara, saumu ni sawa na Ba'yah, na akhlaqi ni sawa na Hudud (adhabu). Zote hizi ni Hukmu za Kishari'ah ambazo ni wajibu kufuatwa, kwani zote zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujifunga nazo ndiko kufikia fahamu halisi ya utiifu na ibada ya ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala. Yeye anasema:

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً)

“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu.” [Al-Baqarah: 208] Pia Mwenyzi Mungu Mtukufu amesema: (وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ) “Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.” [Al-Hijr: 99]

Hivyo basi Uislamu ni lazima uchukuliwe wote na kwa ukamilifu, na ni lazime ututawale na kutudhibiti katika maisha yetu yote hadi kifo chetu. Hivyo munanini enyi Waislamu, muliojitolea katika Shari'ah ya Kiislamu katika mambo fulani pekee na kuipuza katika mambo mengine, au kuitekeleza nyakati fulani na kuitelekeza nyakati nyinginezo?!

Enyi Waislamu:

Jueni kuwa siku hii ya Idd ul-Fitr Mola wenu Mtukufu amewahalalishieni vizuri katika riziki. Kuleni na munywe katika siku hii na wala musivuke mipaka (israaf). Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kufanya israaf, na zidisheni usuhuba mzuri kwa familia zenu, leteni saada/furaha katika nyoyo za masikini, wajane na mayatima, watembeleeni jamaa zenu, muwajali wagonjwa na wafungwa, na mutende wema ili mupate kufanikiwa. Vilevile jueni kuwa Idd sio ya wale wanao vaa nguo mpya, bali ni ya wale wanaoiogopa Siku ya Ahadi.   

Hivyo basi, musiwaruhusu wake zenu na binti zenu kujiacha wazi hadharani kwa kuvaa nguo zisizo za heshima chini ya kisingizio cha furaha na kusherehekea Idd, kwani kufanya hivyo ni kuyavunjia heshima matukufu ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala.

(ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ عِنْدَ رَبِّهِ) Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi.” [Al-Hajj: 30]

Enyi Waislamu:

Hakika umepita mwezi wa Ramadhani wa tisini na nane pasi na kuwepo Khalifah anaye watawala kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala, anaye ziunganisha ardhi zenu na kubeba Uislamu kama ujumbe wa ulimwengu.

Ramadhani ya 98 imemalizika pasi na Khalifah anaye chunga mambo yenu, na kulinda damu zenu, mali zenu, majumba yenu na heshima yenu. Hivyo basi leo, nyinyi ni waathiriwa munao shambuliwa sehemu tofauti tofauti, damu yenu zina mwagwa, mali yenu kuporwa na heshima yenu kuchafuliwa … Na dalili waziwazi ya dhulma hii ni mateso ya Waislamu nchini Uchina eneo la Turkistan Mashariki, pamoja na hali mbaya nchini Yemen, Palestina, Afrika ya Kati, Myanmar, Kashmir, Afghanistan, Somalia, Mali, Libya, Al-Sham na kwengineko… Je, haya hayawafanyi kutafakari maana ya Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika kiongozi (Imamu) ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.” (Muslim)

Mwisho, sisi Hizb ut Tahrir / Tanzania tungependa kuwatakia baraka ya Idd hii tukufu. Tunatoa wito kwa watu wote kutovumilia ubepari wa nidhamu ya kirasilimali, na pia kufahamu na kutangaza hadharani uadilifu wa sheria za Uislamu na suluhisho lake la kudumu kwa matatizo ya wanadamu. Zaidi ya hayo, tunawahutubia na kuwasihi Waislamu haswa katika biladi kubwa za Waislamu kutekeleza jukumu lao tukufu la kubeba ulinganizi wa Kiislamu ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ili kuwakomboa wanadamu wote kutokana na dhulma na giza. Siku hiyo kwa hakika waumini watafurahi.

H. 1 Shawwal 1440
M. : Jumanne, 04 Juni 2019

Hizb-ut-Tahrir
Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu