Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Waislamu, Mapambano Yenu ya Kiitikadi ndio Chimbuko la Nguvu Yenu!

 (Imetafsiriwa)

Msururu wa uchomaji Mshafu Mtukufu (Quran) unaendelea nchini Uswidi, huku polisi wakimpa Salwan Momika idhini nyingine ya kuichoma Quran katika Jiji la Malmo mnamo Jumapili, Septemba 3, 2023. Kituo cha Uswidi (SVT) kiliripoti kwamba watu wawili walijaribu kuvuruga tukio lake kwa nguvu, lakini polisi wakafanikiwa kuwadhibiti. Vituo kadhaa vya habari, likiwemo gazeti la Aftonbladet na kituo cha televisheni cha SVT, viliripotiwa mnamo Jumapili usiku kwamba watu waliojifinika uso  waliwashambulia polisi kwa mawe na kuchoma moto magari kadhaa katika jiji la Malmo.

Uswidi inaendelea kufuata sera ya uoanishaji mkali, ambayo serikali imekuwa ikiifuata kwa miaka kadhaa. Dola ya Uswidi imekuwa ikitekeleza sera kali ya uoanishaji inayolenga kufuta kitambulisho cha Kiislamu cha Waislamu na kuwatia usekula kwa nguvu. Katikati ya kampeni yake dhidi ya Uislamu na kitambulisho cha Waislamu, serikali imejaribu kupiga marufuku hijab, kuzuia ufadhili wa kigeni kwa misikiti, kuondoa msaada kutoka kwa mashirika ya Kiislamu, na kufunga shule za Kiislamu.

Kwa kuongezea, serikali imewalenga watoto wa Waislamu na imeongeza msururu wa uchomwaji Quran. Serikali pia imefuata sera ya kuwashinikiza Waislamu kupitia suala la heshima ambalo linawazuia wazazi wa Kiislamu kulea watoto wao kulingana na kanuni za Kiislamu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا]

“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqara: 217].

Chaneli ya Uswidi ya SVT ilitaja mnamo Jumamosi ya pili ya Septemba 2023 kwamba uchomaji Quran katika kipindi cha mwaka huu iligharimu serikali karibu milioni 4.7 Kronor za Kiswidi. Kwa kuongezea, redio ya Uswidi iliripoti mnamo Agosti mwaka uliopita kwamba msururu wa uchomwaji wa Quran nchini Uswidi uligharimu serikali zaidi ya milioni 40 Kronor za Uswidi. Dola ya Uswidi inaendelea kubeba gharama kubwa kwa sera yake ya uoanishaji, kwani imeigharimu mamilioni ya Kronor, iliharibu sifa yake nje ya nchi, na iliweka hatari kwa usalama wa raia wake na utullivu wa kijamii.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ]

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal: 36].

Mfumo wa kibepari, ambao unaweka uhuru safu ya mbele, hakika umeonyesha kutokuwa na uwezo wake na kufeli katika kuongoza ulimwengu na kujenga jamii inayokubali watu wote. Jamii za kisekula zinaugua chini ya uzito wa misiba ya kisiasa na kiuchumi, kuoza kwa maadili, kuvunjika kwa familia, magonjwa ya akili, na uhalifu. Hapa, watetezi wa demokrasia wanakubali kushindwa kwa maadili yao wakati wanapolegeza msimamo kanuni zao.

Kufilisika kwa fikra ya Kimagharibi kunadhihirika wakati hawawezi kukabiliana na Uislamu kifikra. Badala yake, wanageukia kejeli na uchafuzi. Nguvu ya kifikra ya Uisilamu haina mfanowe, kwani inato changamoto kwa wanadamu kutoa kitu mfano wa Quran. Kufeli kwa Magharibi kupambana na Uislamu kiakili kunawasukuma kuichoma moto Quran na kuwachokoza vijana wa Kiislamu kutoa majibu yenye vurugu mbaya, ambazo wanaweza kuzitumia kwa madhumuni ya kisiasa katika vita vyao dhidi ya Uislamu.

Enyi Waislamu:

Tunakusihini kutojihusisha na makabiliano au majibu ya vurugu ambazo zinakwenda kinyume na Sharia. Vitendo kama hivyo havisuluhishi shida badala yake hutumiwa dhidi yetu. Wito wetu ni wa kifikra na wa kisiasa, na lazima tuunusuru Uislamu kwa msingi huu, haswa katika zama zetu, ambapo ulimwengu unatafuta wokovu kutokana na ufisadi wa urasilimali. Uislamu ndio suluhisho la pekee kwa wanadamu, na dhamira yetu ni kuunganisha juhudi zetu na kuwaelekeza kuelekea usimamishwaji wa Khilafah, tukijumuisha Uislamu badala ya kuvutiwa kuingia kwenye miitiko tasa ambayo hailindi Quran na mwamko wa Waislamu. Tunawasihi Waislamu wote kuzielekeza hasira zao na kutoridhishwa katika hatua kubwa ya kisiasa ili kuyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kupambana na itikadi zengine zote huku wakieneza Uislamu.

Sera ya uoanishaji wa lazima inakusudia kuhujumu imani ya Waislamu na maadili yao matukufu. Msidanganyike na msiibadilishe kwa maadili ya Magharibi ambayo yametelekezwa na watu wao wenyewe. Badala yake, jiboresheni dhidi yao kwa kushikamana na maadili ya Kiislamu. Maadili ya Kiislamu sio miito tu na ibada; Ni fahamu zinazojidhihirisha katika tabia na mtindo wa maisha. Jifunzeni mafundisho ya Uislamu kwa undani ili muweze kubeba Uislamu kifikra na kusimama dhidi ya majaribio haya ya uoanishaji. Pambaneni na maadili ya Magharibi kifikra na muonyeshe utukufu wa Uislamu.

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawba: 33].

H. 19 Safar 1445
M. : Jumatatu, 04 Septemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Sweden

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu