بسم الله الرحمن الرحيم
Enyi Maulamaa Waheshimiwa! Simameni Imara Pamoja na Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Mapambano ya Kuhuisha Uislamu kama Mfumo Kamili wa Maisha
(Imetafsiriwa)
Enyi Maulamaa waheshimiwa, Mwenyezi Mungu (swt) amekupandisheni hadhi kutokana na elimu ya Dini, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema ndani ya Quran Tukufu,
[يَرۡفَعِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ دَرَجَٰتٖۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ]
“Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Surah Al-Mujadila 11]. Tunakuhutubieni kwa msingi wa hadhi hii iliyoinuliwa, kwani cheo cha juu huleta wajibu mkubwa zaidi. Tunakuhutubieni kwa matumaini na Dua kwamba sisi sote tunasimama miongoni mwa wanaosimamisha haki, na hatumuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt).
Baada ya kuvunjwa Khilafah, matukio yaliyofuatana ambayo yalitokea katika karne iliyopita ya Hijri, na matokeo yake ya mwamko katika Ummah, yaliyozaliwa kutokana na imani ya Kiislamu (Aqida), ni dhahiri kwa kila mtu. Kuanzia mitandao ya kijamii hadi mikusanyiko ya kila siku, kurudi kwa utawala wa Uislamu imekuwa mada ya mjadala. Kutokana na kutojali na usaliti wa watawala wa Waislamu, mauaji yanayoendelea nchini Palestina yanayofanywa na umbile la Kiyahudi yamemlazimu kila Muislamu makini kutafakari juu ya ukombozi wa Ardhi hiyo Iliyobarikiwa, na njia za kuilinda dhidi ya uvamizi wa dola za Magharibi.
Katika hali hii, katika wadhifa wenu kama warithi wa Mitume (as), ni jukumu zito juu yenu kupaza sauti zenu kutoka misikitini, kuhusiana na kadhia ya uhai na kifo ambayo Umma wa Kiislamu unakabiliana nayo leo. Kadhia hii ni kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inalinda umoja wa Umma wa Kiislamu, nusra ya kijeshi kwa Waislamu wanaodhulumiwa, na kuanzishwa kwa mfumo wa kilimwengu wa Kiislamu.
Tunakuombeni kwamba katika kadhia hii, mutaungana nasi kuwalingania Waislamu wa Pakistan kuhusiana na masuala yafuatayo, bila kuogopa lawama za yeyote mwenye kulaumu mnaposema ukweli. Kama Mtume (saw) alivyosema,
«لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوْفَ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْکَرِ أَوْ لَيُسَلِّطَنَّ اللهُ عَلَيْکُمْ شِرَارَکُمَ. ثُمَّ يَدْعُوْ خِيَارُکُمْ فَـلَا يُسْتَجَابُ لَکُمْ»
“Lazima muamrishe mema na lazima mukataze maovu, au Mwenyezi Mungu atakusalitini kwa waovu wenu zaidi. Kisha walio bora miongoni mwenu wataomba, lakini dua zao hazitajibiwa.” (Al-Tabarani katika Al-Mu'jam Al-Awsat).
1. Kutawala kwa mujibu wa amri zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu ni faradhi:
Mwenyezi Mungu (swt) amewajibisha Waislamu kwamba utawala wao lazima uwe juu ya maamrisho na makatazo ya Uislamu pekee. Katiba na sheria za dola yao lazima zivuliwe kwenye Shariah ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliiteremsha kwa Muhammad (saw). Hili linaweza kufikiwa tu pale dola ya Kiislamu, Khilafah, itakaposimamishwa. Mtawala, aliyeteuliwa kupitia Bay’ah ya utiifu ya Kisharia, anatekeleza Uislamu kwa watu, anatekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu katika mambo yote ya maisha, anaunganisha rasilimali za Waislamu, na anaweka sera za kigeni kwa misingi ya Da’wah na jihadi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفٰسِقُونَ]
“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” [Surah Al-Ma'idah: 47]. Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha,
[فَاحۡكُمۡ بَيۡنَهُمۡ بِمَاۤ اَنۡزَلَ اللّٰهُ وَلَا تَتَّبِعۡ اَهۡوَآءَهُمۡ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ الۡحَـقِّؕ] “Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Surah Al-Ma'idah: 48].
Katika wadhifa wenu kama warithi wa Mitume, ni wajibu kwenu kuungana mikono na vijana (Mashababu) wa Hizb ut Tahrir ili kuwadhihirishia Waislamu wa Pakistan haja ya kuchukua kuubadilisha mfumo wa sasa wa demokrasia ya kisekula, kwa mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt). Hili lazima lifanywe kwa namna ambayo wataiona kama jambo la kukatikiwa la uhai na kifo, na kujitolea wenyewe kwa mapambano ya kuendelea katika njia hii.
2. Kukataa Mfumo wa Kilimwengu, Ambao kwa Kweli ni Taghut, ni Faradhi
Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha kukataa kila aina ya Taghut (batili au udhalimu). Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ]
“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo!” [Surah An-Nisa: 60].
Mtu yeyote au taasisi yoyote inayotunga sheria kinyume na amri zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu inachukuliwa kuwa ni Taghut. Watawala wa Pakistan kupeleka maamuzi kuhusu Waislamu kwa taasisi kama vile Umoja wa Mataifa, Baraza lake la Usalama, IMF, Benki ya Dunia, na FATF ni kitendo cha utiifu kwa Taghut. Ambapo Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّـٰغُوتَۖ]
“Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni shetani (Taghut)’” [Surah An-Nahl: 36].
Katika wadhifa wenu kama warithi wa Mitume (as), lazima muungane mikono na vijana wa Hizb ut Tahrir katika kufikisha wito huu kwa Waislamu wa Pakistan: kwamba imani juu ya Mwenyezi Mungu, Muumba wa ulimwengu, inalazimu kukataa ukuu wa aina zote za ndani na nje za Taghut. Badala yake, ukuu wa sheria za Mwenyezi Mungu lazima usimamishwe kupitia mfumo wa Khilafah.
3. Kuvunja Masanamu ya Utaifa na Uzalendo ni Faradhi:
Fahamu za utaifa na uzalendo zilienezwa miongoni mwa Waislamu ili kuvunja umoja wa Ummah na kukata mshikamano wa udugu ambao umekita mizizi katika imani ya Kiislamu (Aqida). Fikra hizi zinawatenga Waislamu wanaoishi katika eneo moja na ndugu zao katika sehemu nyingine za dunia, hata kama makafiri wanawaua bila huruma watoto wa Kiislamu, wanawake na wazee katika maeneo hayo. Hata hivyo, Uislamu unaona kuwa mauaji yanayotokea Palestina sio tu wasiwasi wa watu wa Palestina pekee, ukandamizaji huko Kashmir sio kadhia ya watu wa Kashmir pekee, na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Sudan sio tu tatizo la watu wa Sudan pekee, bali haya yote ni masuala ya Umma wa Kiislamu, na kuyatatua ni wajibu kwa Ummah mzima. Mwenyezi Mungu anasema,
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfal: 72].
Utaifa na uzalendo ni aina za asabiyyah (ukabila). Kuhusu Asabiyyah, Mtume wetu kipenzi (saw) amesema:
«مَنْ قُتِلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ يَدْعُو عَصَبِيَّةً أَوْ يَنْصُرُ عَصَبِيَّةً فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ»
“Mwenye kuuwawa chini ya bendera ya watu vipofu, akilingania asabiyyah au kuunga mkono asabiyyah, kifo chake ni cha Kijahiliyyah (ujinga)” (Muslim). Utaifa na uzalendo ni fikra hatari. Kuzikumbatia kunapelekea kutelekeza faradhi ya jihad kwa ajili ya kueneza Uislamu kwa wanadamu wote.
Enyi watukufu maulamaa! Lazima muungane mikono na vijana wa Hizb ut Tahrir kufikisha amri ya Mwenyezi Mungu kwa Waislamu wa Pakistan, mpaka waache kila mwito wa 'asabiyyah. Ni lazima watambue kwamba hakuna Muislamu aliye bora au duni kwa kuzingatia utaifa wao, iwe Afghanistan au Pakistan au Palestina. Ni lazima pia waelewe kwamba majaribio ya kuwagawanya ni sehemu ya ajenda ya ukoloni, na kujitenga kwa Balochistan kutoka kwa Waislamu wengine, kutazidi kudhoofisha Umma. Fikra za ukuu wa rangi au kabila hugawanya Ummah, na kuimarisha mshiko wa makafiri juu ya Waislamu.
Ni wajibu kwenu kuangazia umbile la kimataifa la imani ya Kiislamu (Aqida) miongoni mwa Waislamu wa Pakistan, mpaka nyoyo zao ziunganishwe mbali zaidi ya kabila, rangi, lugha, na eneo. Ni lazima wahamasishwe ili kufuta mipaka bandia ya utaifa iliyochorwa kati ya ardhi za Waislamu.
4. Kukusanya Majeshi Kukomboa Ardhi Zinazokaliwa Kimabavu na Kutoa Nusrah (msaada wa kimada) kwa Waislamu Wanaokandamizwa ni Faradhi:
Hakuna aliye na haki ya kusalimisha sehemu yoyote ya ardhi ya Kiislamu, au kukubali utawala wa makafiri juu ya ardhi za Kiislamu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَلَنْ يَّجْعَلَ اللّـٰهُ لِلْكَافِـرِيْنَ عَلَى الْمُؤْمِنِيْنَ سَبِيْلًا] “wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisa: 141]. Uislamu unaamuru kwamba uvamizi wa makafiri ukomeshwe kwa nguvu za kijeshi, na kwamba wafukuzwe katika ardhi za Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَاَخۡرِجُوۡهُمۡ مِّنۡ حَيۡثُ اَخۡرَجُوۡكُمۡ] “na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah: 191].
Ni wajibu kwa vikosi vya kijeshi vyenye uwezo na shujaa vya Pakistan kutumwa kuwasaidia Waislamu wanaodhulumiwa wa Gaza. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُوْنَ فِیْ سَبِیْلِ اللّٰهِ وَ الْمُسْتَضْعَفِیْنَ مِنَ الرِّجَالِ وَ النِّسَآءِ وَ الْوِلْدَانِ الَّذِیْنَ یَقُوْلُوْنَ رَبَّنَاۤ اَخْرِجْنَا مِنْ هٰذِهِ الْقَرْیَةِ الظَّالِمِ اَهْلُهَاۚ-وَ اجْعَلْ لَّنَا مِنْ لَّدُنْكَ وَلِیًّا وَّ اجْعَلْ لَّنَا مِنْ لَّدُنْكَ نَصِیْرًا]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [Surah An-Nisa: 75]. Kuondoa kikwazo chochote kinachozuia kutekeleza faradhi hii pia ni faradhi, kama kanuni ya Sharia inavyosema, مَا لَا يَتِمُ الْوَاجِبُ إِلَّا بِهِ فَهُوَ وَاجِبٌ “Chochote ambapo wajibu hautekelezeki isipokuwa kwacho huwa hicho pia ni wajibu.”
Enyi Maulamaa waheshimiwa! Mnafahamu vyema kwamba kizuizi kikubwa kinachozuia majeshi kutekeleza wajibu huu ni watawala wa ardhi za Waislamu, ikiwemo Pakistan, ambao wamemfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake (saw) na Umma kuhusu suala la Palestina. Enyi Maulamaa! Nyinyi ni warithi wa Maulamaa wakubwa kama Ibn Taymiyyah, Izz ad-Din Abd al-Salam, na Qadi Muhyi ad-Din Zaki, wakati wa uvamizi wa Matatari na Vita vya Msalaba, waliukumbusha Ummah wajibu wa Jihad na kuwawajibisha watawala. ili majeshi ya Waislamu yakusanywe kupigana na adui. Waliendelea kuhimiza majeshi na Ummah kuelekea jihad mpaka ardhi za Waislamu zikatwahirishwa kutokana na uchafu wa makafiri. Basi, ni nani miongoni mwenu atakayesimama kuwa mfuasi anayestahiki wa watangulizi wenu watukufu, ili vizazi vijavyo vikukumbukeni kwa heshima sawa na vile mnavyowakumbuka wale waliokuja kabla yenu?
5. Ni Faradhi Kusimamisha Utawala wa Uislamu Juu ya Dini Nyengine Zote:
Uislamu haukuteremshwa ili kuridhiana na dini nyingine au kuendeleza mifumo ya ukafiri. Badala yake, uliteremshwa ili kutawala dini nyingine zote, sheria, na mifumo ya maisha, na kuondoa batili. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[هُوَ الَّذِیْۤ اَرْسَلَ رَسُوْلَهٗ بِالْهُدٰى وَ دِیْنِ الْحَقِّ لِیُظْهِرَهٗ عَلَى الدِّیْنِ كُلِّهٖ وَ لَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُوْنَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surah At-Tawbah: 33]. Leo, Uislamu utatawala tu mifumo mingine pale mfumo wa sasa wa kibepari wa dunia utakapobadilishwa na mfumo wa kilimwengu wa Kiislamu, jambo ambalo linawezekana tu kupitia kusimamishwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah hii haikuegemezwa kwenye muundo wa dola za kitaifa, na sera yake ya mambo ya nje imejikita katika Da’wah (ulinganizi wa Uislamu) na Jihad. Pakistan, kwa sababu kadhaa, inafaa sana kuwa nukta ya nusra kwa ajili ya kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu.
Ni muhimu kwamba vijana wa Kiislamu wa leo wakumbushwe juu ya misheni waliokabidhiwa na Mtume wa mwisho (saw), na ukumbusho huu lazima utoke misikitini. Enyi Maulamaa, ni nani mwingine zaidi ya nyinyi anayeweza kutekeleza kazi hii muhimu? Enyi Maulamaa waheshimiwa, miaka mia moja iliyopita, makafiri Waingereza, kupitia kwa Mustafa Kemal, waliivunja Khilafah ya Waislamu. Hata hivyo, gurudumu la wakati limeregea kwenye nukta ile ile, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, karne hii wazi wazi ni ile ya mwamko wa Umma na Uislamu unaoinuka tena kama mfumo kamili wa maisha.
Wakati umefika wa sisi tuupe Ummah wetu ngao dhidi ya fikra na mifumo dhalimu iliyowekwa na makafiri. Wakati umefika sasa kwa sisi kuukomboa Umma wa Kiislamu, wakiwemo Waislamu wa Pakistan, kutoka kwenye udhalilifu na fedheha iliyowekwa na mfumo wa ulimwengu wa Magharibi kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Huu ndio wakati wa kufanya kazi na watoto wa Ummah waaminifu na waadilifu, kutekeleza Shariah iliyobarikiwa ya Mwenyezi Mungu kwa kusimamisha Khilafah, na kuunganisha nguvu za Waislamu dhidi ya maadui zao makafiri, kurudisha heshima na utukufu wa Ummah. Wakati umefika sasa kwa Uislamu kuongoza ulimwengu na kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika jinai na ukandamizaji wa mfumo wa kibepari.
H. 8 Rabi' II 1446
M. : Ijumaa, 11 Oktoba 2024
Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan